Kuhusu malipo ya gharama za matibabu aliyotumia marehemu

Mzinza wa town

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
347
368
Kwaza nianze kwa kutoa pole kwa wale waliofiwa ndugu zao na kushindwa kuzika kwa wakati kutokana na miili ya ndugu zao kuzuiliwa. Poleni sana.
Pili, nataka kuwalaumu wanasiasa kwa unafiki mkubwa katika hili swala. Hivi hao wanasiasa wakifa huko India huwa hawalipi gharama za matibabu?
Mwisho napendekeza yafuatayo ili kumaliza huu mgogoro
1. Hospitali zisitoe huduma kama mtu hajalipia matibabu kwani mara nyingi ndugu huziomba hospitali ndugu yao atibiwe wakipata hela watalipa, sasa amepona amekufa nani alipe gharama?
2. Serikali igharimie matibabu ya watu wote. Yaani mtu ukiumwa wewe nenda hospitali hutalipa chochote kama ilivyo elimu bure.
3. Wanasiasa acheni unafiki
 
kwanini ulipwe pesa za jambo uloshindwa kulitimiza? Mgonjwa amefariki wewe unataka pesa tu na jukumu la kumponya limekushinda. Wanadamu hatuthamiani ndo hayo HAMIS KIGWANGALA amejiapiza kutoa uhai wa mwanadamu mwenziye kisa twiga ama tembo.
 
Mtu akipona alipe gharama akifa ndugu wasamehewe gharama inakuwa kama adhabu ikizingatiwa matibabu yana weza kwenda mpaka mamilioni ya fedha ambazo wengi hawawezi kuzipata
Ndo maana nimesema mtu asipate huduma kama hajalipia au serikali ulipie gharama za matibabu kwa watu wote kama ilivyo elimu bure
 
kwanini ulipwe pesa za jambo uloshindwa kulitimiza? Mgonjwa amefariki wewe unataka pesa tu na jukumu la kumponya limekushinda. Wanadamu hatuthamiani ndo hayo HAMIS KIGWANGALA amejiapiza kutoa uhai wa mwanadamu mwenziye kisa twiga ama tembo.
Gharama za matibabu ni kitu kingine na outcome ya treatment ni kitu kingine
 
tunampeleka ndugu hospitali ili akatibiwe apone, akifa maana yake hospitali imefeli kutupa huduma tuliyokusudia ya kumponya mpendwa wetu, sasa tuwalipe hela za nini?
yaani nikupe kazi ya kutengeneza gari, mwisho wa siku kazi imekushinda alafu unanidai hela? ebo!
 
Ukipona ndio ulipe...
Ukifa deni lifutwe usilipe coz wanavyofanya sasa haileti motisha kwa hospitali kukupambania upone sababu wanajua hata ukifa watadai tu chao..

Ila tukisema ukipona ndio ulipe itasaidia wa fighr kukuokoa
 
Gari ni kitu kingine na mtu ni kitu kingine. Huwezi mfananisha mtu na gari argument yako ikawa sawa. Kama mtashindwa kuiambia serikali matibabu iwe bure kwa watu wote basi hospitali zitaendelea kuwadai. Hospitali nazo zinatumia pesa kijiendesha
 
Ukipona ndio ulipe...
Ukifa deni lifutwe usilipe coz wanavyofanya sasa haileti motisha kwa hospitali kukupambania upone sababu wanajua hata ukifa watadai tu chao..

Ila tukisema ukipona ndio ulipe itasaidia wa fighr kukuokoa
Kuna hospitali moja kama hujalipia matibabu hupati huduma na ukitaka msamaha mlolongo ni mrefu kuja kupata huduma inakuwa too late na outcome inakuwa sio nzuri.
 
tunampeleka ndugu hospitali ili akatibiwe apone, akifa maana yake hospitali imefeli kutupa huduma tuliyokusudia ya kumponya mpendwa wetu, sasa tuwalipe hela za nini?
yaani nikupe kazi ya kutengeneza gari, mwisho wa siku kazi imekushinda alafu unanidai hela? ebo!
KWANI KUNA HOSPITALI ZINATIBU WATU HALAFU WANAISHI MILELE?
 
Wawatibu tu wagonjwa wetu wakifariki sisi hatutadeal na mwili tutafanya msiba nyumbani.... Wakiishazika watupe taarifa tukajengee kaburi
 
Mtu akipona alipe gharama akifa ndugu wasamehewe gharama inakuwa kama adhabu ikizingatiwa matibabu yana weza kwenda mpaka mamilioni ya fedha ambazo wengi hawawezi kuzipata
Kuna ndugu yetu
jamaa wameshindwa kumtibu
baada ya kupoteza maisha
ndugu tumetandikwa bonge la bill isiyo na kichwa wala miguu.
 
Back
Top Bottom