kuhusu malaria

Milton Mponda

Member
Apr 5, 2011
7
0
Habari wanajamii
mi nataka nifahamu kitu kinachosababisha malaria kuwa sugu na tiba yake ni nini.Vilevile kama kuna mtu
anafahamu madawa ya mitishamba ambayo yanatibu kweli malaria sugu na si usanii wa mjini hapa.Malaria yangu imekuwa haiishi ninapotumia dawa sasa sijui ndo usugu wenyewe au nini hasa.
please help me!
 
Milton Mponda,

Ungepitia baadhi ya thread kuhusu Malaria, katika moja ya thread(Malaria,kila mwezi, ni zaidi ya miaka 20 sasa naomba tiba) Dr. Riwa alijaribu kuelezea vizuri, pitia hiyo na ukiwa na maswali ndiyo urudi mkuu
 
Last edited by a moderator:
Inaelekea humalizi dozi, labda kama wewe ni mzee wa laga ukishaiona basi na dozi inasahaulika. pole.
 
Milton Mponda,

Ungepitia baadhi ya thread kuhusu Malaria, katika moja ya thread(Malaria,kila mwezi, ni zaidi ya miaka 20 sasa naomba tiba) Dr. Riwa alijaribu kuelezea vizuri, pitia hiyo na ukiwa na maswali ndiyo urudi mkuu

Mkuu nahisi hujamwelewa huyu jamaa yetu. Yeye anahitaji dawa za mitishamba,so ushauri wa dr riwa huenda usimsaidie(rejea uzi wake mwingine aliopost wa tatizo hili hili)!

Anyway,ninavyoona hapa,sasa watu wamishaanza kucheza na malaria,maana siku hizi kila mtu anajua kuitibu.Halafu mwisho wa siku akishindwa kupona ananza kulalamikia dawa.Kiukweli bado tuna safari ndefu kufika. Lakini sio mbaya,mi namtakia jamaa kila la kheri huko aendako.
 
Mkuu Mrimi, ahsante kunikumbusha hilo...anyway huko si taaluma yangu lakini natambua wapo wataalamu wengi katika forummf MziziMkavu n.k

Nadhani kuna shida fulani hasa katika utambuzi wa uginjwa(Diagnosis) wa Malaria..yaani kwa wengine Malaria ni
-Kuwa na homa au
-Kujisikia kuchoka au
-Viungo kuuma na kwa wengine
-Kujisikia vibaya.

na matokeo yake mtu huamua kwenda duka la dawa(pharmacy) kununua dawa Bila kupima(kuwa na uhakika), kisha linakuja tatizo lingine la matumizi ya dawa..

All in all, kutopona kwa ugonjwa kunaweza kusababishwa na

-Ugonjwa unaodhaniwa(Diagnosis) si sahihi.
-Kutopewa dawa/ dozi sahihi ingawaje ugonjwa umetambulika.
-Kutokuwa makini na matumizi mazuri ya dawa( kutotumia dawa kwa wakati, kutomaliza dozi hasa mara baada ya mgonjwa kupata unafuu)
-Madawa kutofanya kazi mwilini kwa sababu ya kuzoeleka( Resistance).

Muhimu, kufanya vipimo kujua hasa tatizo liko wapi na si kujaribisha dawa kila wakati.
 
Last edited by a moderator:
A poison in small doses is a drug, but a drug in big dose is a great poison! angalia!
 
Back
Top Bottom