Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,022
- 9,292
Hadi hivi sasa taarifa za Makusanyo ya kila mwezi kwa mwezi November haijatolewa.
Na kwa jinsi tunavyoona serikali ikiendelea kujifunga mkanda yenyewe, wananchi tungependa kujua, Je hali ya Makusanyo iko shwari?.
Tumeona hapa serikali ikisitisha vibali vya ajira, hapo mwanzo ikasema inasubiri zoezi la uhakiki lipite, hata hivyo zoezi limeisha na Wafanyakazi hewa 17000 wameonekana na kuondolewa kwenye payroll, Je ni kama serikali imesevu pesa nyingi baada ya kuwaondoa wafanyakazi hewa kwa nini haikurasimisha ajira za wale waliokwishapewa barua za ajira?. Hapo ndipo tunapoiuliza serikali je Makusanyo ya kila mwezi yako shwari?.
Tumeona bodi ya mikopo, ikisitisha mkopo wa tiketi ya ndege kwa vijana wanaopata scholarship katika nchi rafiki, China ikiwa ndiyo rejea, hii haijawahi kutokea katika serikali zilizopita, Tunaomba serikali itueleze, Je makusanyo ya kila mwezi yako Shwari?
Majuzi nilipita sehemu nikawakuta watu wanapiga soga,nikajibanza sehemu nikawa nawasikiliza, miongoni mwa mazungumzo yao ilikuwa ni kushuka kwa ukusanyaji wa mapato ya TRA, nikasikia mmoja akisema kwa hali anayoiona ni dhahiri TRA hawakusanyi hata shilingi bilioni 650 kwa mwezi!. Mimi nikashtuka sana kwa hilo, Sasa tunaomba serikali itupe majibu juu ya hali ya Makusanyo kwa mwezi, Je hali iko shwari?