Kuhusu majimbo 15 ya NCCR baada ya Uchaguzi Mkuu haya hapa

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
17,744
44,739
Kosa kubwa ni kumwamini Mtu anapokwambia atakupa majimbo 15, wakati na yeye ni mgombea, na chama chake kina wagombea kwenye hayo majimbo na wanamnadi yeye na kusaidia chama chake.

Lakini kosa kubwa zaidi ni kuhujumu wapinzani wenzako ambao mwanzo walikuamini na mkashirikiana. Sasa utajiuliza kwanini CCM wameweka wagombea kwenye majimbo yote, unadhani watawatosa?

Mbaya zaidi kwenye Jimbo lako mgombea wa CCM atakayepitishwa ni Charles Stephen Kimei, huyu ndiye aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB wakati ikifungua tawi lake Chato. Na jengo ambalo CRDB wanalitumia kule Chato ni jengo la Bosi kubwa.

Bado kuna mgombea wa CHADEMA ambaye anakubalika kuliko Chama chochote huko Vunjo.
Haya pambana sasa
 
Nani kakwambia Mbatia anagombea ubunge wa Vunjo? Inawezekana akagombea urais wa JMT, bado hajasema. Kuwa na subira. Kimei mwenyewe bado hajapitishwa na chama chake kuwa mgombea ubunge wa Vunjo.
 
Aaaah hoja nikutengeneza main opposition party.
Idadi ya kura alizopata mgombea uraisi kwenye uchaguzi mkuu zinawezesha chama kupata ruzuku kubwa ya fedha toka serikalini na hivyo kuimarisha chama. Hichi ndicho alikifanyia Lowasa chama cha chadema.

Pili Mbatia akigombea urais itamuwezesha kufanyia kampeni chama chake nchi nzima na hivyo kuwezesha chama chake kupata wabunge wengi. Akigombea ubunge wa Vunjo hatapata nafasi hiyo ya kuzunguka nchi nzima kunadi chama chake. Lowasa alipozunguka nchi nzima ndiyo alipoiwezesha CDM kupata wabunge wengi. ACT wanatamani Membe akifanyie hivyo chama chao ili angalao waweze kupata wabunge wawili toka Tanzania bara!
 
Back
Top Bottom