Wazolee
JF-Expert Member
- Sep 1, 2018
- 2,699
- 3,088
Hiki kitendo cha bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuwanyima mikopo wanafunzi ambao wametoka private school hakipo sawa hata kidogo kwa sababu zifuatazo:
Kwa mtazamo wangu Mimi huyu mzazi ameisaidia serikali kwa kuchukua jukumu la kumsomesha mtoto wake yeye mwenyewe kuanzia chekechea hadi kidato cha sita kiuhalisia jukumu la kumsomesha huyu mtoto lili kuwa ni la serikali hivyo hapa mzazi anakuwa ameisaidia serikali.
Huyu mzazi pia analipa kodi kama wananchi wengine hivyo na yeye anamchango wake katika huo mfuko wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu maana bodi ya mikopo inaendeshwa kwa kodi za wananchi sasa iweje walipa kodi wengine wafaidi matunda ya kodi zao na wengine wanyimwe kufaidi matunda ya kodi zao.
Nasema huyu mzazi ameisaidia serikali kwa sababu ikitokea Leo hii watoto wote wanaosoma private school kuanzia chekechea hadi kidato cha sita wazazi wao wakiamua kuwarudisha katika shule za serikali ina maana mzigo wa serikali kusomesha watoto wa wananchi utakuwa umeongezeka serikali itabidi ianze kuongeza vyumba vya madarasa na walimu pia hivyo kumbe hawa wazazi wanaisaidia serikali sasa kwa nini waadhibiwe kwa hilo.
Pia inawezeka huyu mzazi kipindi hicho alikuwa na mishemishe zake za kumuingia kipato akamua ni bora amsomeshe mwanawe private school lakini leo hi mtoto amemaliza kidato cha sita na mzazi mishe zimekata mtoto wake anakosa mkopo wa elimu ya juu na kushindwa kutimiza ndoto zake kwa kweli hili halipo sawa.