Kuhusu kuwanyima mikopo ya elimu ya juu wanafunzi waliotoka shule binafsi, hili halipo sawa

Wazolee

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
1,563
2,000
Hiki kitendo cha bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuwanyima mikopo wanafunzi ambao wametoka private school hakipo sawa hata kidogo kwa sababu zifuatazo:

Kwa mtazamo wangu Mimi huyu mzazi ameisaidia serikali kwa kuchukua jukumu la kumsomesha mtoto wake yeye mwenyewe kuanzia chekechea hadi kidato cha sita kiuhalisia jukumu la kumsomesha huyu mtoto lili kuwa ni la serikali hivyo hapa mzazi anakuwa ameisaidia serikali.

Huyu mzazi pia analipa kodi kama wananchi wengine hivyo na yeye anamchango wake katika huo mfuko wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu maana bodi ya mikopo inaendeshwa kwa kodi za wananchi sasa iweje walipa kodi wengine wafaidi matunda ya kodi zao na wengine wanyimwe kufaidi matunda ya kodi zao.

Nasema huyu mzazi ameisaidia serikali kwa sababu ikitokea Leo hii watoto wote wanaosoma private school kuanzia chekechea hadi kidato cha sita wazazi wao wakiamua kuwarudisha katika shule za serikali ina maana mzigo wa serikali kusomesha watoto wa wananchi utakuwa umeongezeka serikali itabidi ianze kuongeza vyumba vya madarasa na walimu pia hivyo kumbe hawa wazazi wanaisaidia serikali sasa kwa nini waadhibiwe kwa hilo.

Pia inawezeka huyu mzazi kipindi hicho alikuwa na mishemishe zake za kumuingia kipato akamua ni bora amsomeshe mwanawe private school lakini leo hi mtoto amemaliza kidato cha sita na mzazi mishe zimekata mtoto wake anakosa mkopo wa elimu ya juu na kushindwa kutimiza ndoto zake kwa kweli hili halipo sawa.
 
live on

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
484
1,000
Ni kweli hapa ipo shida hata hizo private school jinsi zilivyo jaziwa mikodi ya serikali yani utashangaa

Ni kama vile serikali ina discourage private school wakati hizi zipo kwa ajili ya kuisaidia serikali

Ongera Mzee Mwinyi kwa kuanzisha private school Tanzania ili ziisaidie serikali kutoa elimu na ajira kwa wananchi ila kwa sasa wamiliki wa shule binafsi, wazazi wanaosomesha watoto wao shule binafsi na watoto wanaosoma shule binafsi wanaadhibiwa kwa hilo
 
Lob

JF-Expert Member
Jul 24, 2017
491
1,000
Hiki kitendo cha bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuwanyima mikopo wanafunzi ambao wametoka private school hakipo sawa hata kidogo kwa sababu zifuatazo:

Kwa mtazamo wangu Mimi huyu mzazi ameisaidia serikali kwa kuchukua jukumu la kumsomesha mtoto wake yeye mwenyewe kuanzia chekechea hadi kidato cha sita kiuhalisia jukumu la kumsomesha huyu mtoto lili kuwa ni la serikali hivyo hapa mzazi anakuwa ameisaidia serikali.

Huyu mzazi pia analipa kodi kama wananchi wengine hivyo na yeye anamchango wake katika huo mfuko wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu maana bodi ya mikopo inaendeshwa kwa kodi za wananchi sasa iweje walipa kodi wengine wafaidi matunda ya kodi zao na wengine wanyimwe kufaidi matunda ya kodi zao.

Nasema huyu mzazi ameisaidia serikali kwa sababu ikitokea Leo hii watoto wote wanaosoma private school kuanzia chekechea hadi kidato cha sita wazazi wao wakiamua kuwarudisha katika shule za serikali ina maana mzigo wa serikali kusomesha watoto wa wananchi utakuwa umeongezeka serikali itabidi ianze kuongeza vyumba vya madarasa na walimu pia hivyo kumbe hawa wazazi wanaisaidia serikali sasa kwa nini waadhibiwe kwa hilo.

Pia inawezeka huyu mzazi kipindi hicho alikuwa na mishemishe zake za kumuingia kipato akamua ni bora amsomeshe mwanawe private school lakini leo hi mtoto amemaliza kidato cha sita na mzazi mishe zimekata mtoto wake anakosa mkopo wa elimu ya juu na kushindwa kutimiza ndoto zake kwa kweli hili halipo sawa.
Haliko sawa ni wivu na roho mbaya tu
 
Mnyatiaji

JF-Expert Member
Dec 13, 2018
1,889
2,000
Mimi kuna rafiki yangu mzee wake alijitahidi kumpeleka private akiwa secondary lakini kufika chuo ananyimwa mkopo isitoshe mzee wake ni bodaboda alimsomesha private kwa kujibana tu
 
DA HUSTLA

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
2,033
2,000
Hiki kitendo cha bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuwanyima mikopo wanafunzi ambao wametoka private school hakipo sawa hata kidogo kwa sababu zifuatazo:

Kwa mtazamo wangu Mimi huyu mzazi ameisaidia serikali kwa kuchukua jukumu la kumsomesha mtoto wake yeye mwenyewe kuanzia chekechea hadi kidato cha sita kiuhalisia jukumu la kumsomesha huyu mtoto lili kuwa ni la serikali hivyo hapa mzazi anakuwa ameisaidia serikali.

Huyu mzazi pia analipa kodi kama wananchi wengine hivyo na yeye anamchango wake katika huo mfuko wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu maana bodi ya mikopo inaendeshwa kwa kodi za wananchi sasa iweje walipa kodi wengine wafaidi matunda ya kodi zao na wengine wanyimwe kufaidi matunda ya kodi zao.

Nasema huyu mzazi ameisaidia serikali kwa sababu ikitokea Leo hii watoto wote wanaosoma private school kuanzia chekechea hadi kidato cha sita wazazi wao wakiamua kuwarudisha katika shule za serikali ina maana mzigo wa serikali kusomesha watoto wa wananchi utakuwa umeongezeka serikali itabidi ianze kuongeza vyumba vya madarasa na walimu pia hivyo kumbe hawa wazazi wanaisaidia serikali sasa kwa nini waadhibiwe kwa hilo.

Pia inawezeka huyu mzazi kipindi hicho alikuwa na mishemishe zake za kumuingia kipato akamua ni bora amsomeshe mwanawe private school lakini leo hi mtoto amemaliza kidato cha sita na mzazi mishe zimekata mtoto wake anakosa mkopo wa elimu ya juu na kushindwa kutimiza ndoto zake kwa kweli hili halipo sawa.
Chonde chonde ,kama unaweza mlipia mwanao ada ya chuo mlipie....mkopo wa HESLB ni ulemavu wa kudumu ,mwanao atateseka sana narudia atateseka sana kwenye harakati za kuulipa
 
Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
4,857
2,000
Kiufupi Tu waliotoka private sjui fedha boys huko hawawez shindwa kulipa chuo , kuna vijana wengi Tu nimeshuhudia wanashindwa kujiunga na chuo sababu ya kukosa mkopo ili Hali kuna vijana wametoka private school za mamilion na wamepata hili Jambo linaumiza Sana , kuna kijana kamaliza sengerema boys kajipinda kapata one yake ya PCB , amechaguliwa bugando CUHAS ameshindwa kwenda sababu Hana mkopo , imebid asubir mwakan ajarbu bahati...... Serikal iliangalie Kwa makini hili swala
 
live on

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
484
1,000
Chonde chonde ,kama unaweza mlipia mwanao ada ya chuo mlipie....mkopo wa HESLB ni ulemavu wa kudumu ,mwanao atateseka sana narudia atateseka sana kwenye harakati za kuulipa
Vipi kama huna uwezo wa kumlipia ada ya chuo mwanao na amesoma private school
 
live on

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
484
1,000
Kigezo cha kupata mkopo wa chuo kinatakiwa kiwe ni ufaulu wa mwanafunzi na sio kuangalia shule aliyotoka kama ni ya private au government

Mishahara ya hao wafanyakazi wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu inatokana na kodi za wananchi wote haijalishi mwanao anasoma private au government
 
McMahoon

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
1,316
2,000
Lazima tuongee lugha moja tu. Ni suala la muda tu, utakutwa popote ulipo.
 
BabuMwerevu

JF-Expert Member
Feb 11, 2017
815
1,000
Asilimia kubwa wa waliosoma shule za serikali ni kutoka familua zisizojiweza.
Mzazi aliyemsomesha mwanaye st Mary's hawezi shindwa mlipia mtoto ada ya chuo.
Kwanza huo ni ubaguzi pili hizo ni pesa za walipa kodi wote siyo za wasiojiweza tuu kwa hiyo zitumike kwa wote kwa maana inawezekana uwezo wa sekondari alikuwa nao lakini chuo hana.
 
Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
1,226
2,000
Hapan bna .....wale wa private wanajiweza kdg.......serikali haina uwezo wa kuwapa wote mikopo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom