Kuhusu kutumbuliwa kwa managers wa Tanroads mkoa wa Pwani na Lindi

Barabara zinazoharibika na zenye mashimo hatarishi zipo nyingi ikiwemo hiyo ya kusini.
Barabara ya kilwa ilijengwa kwa viwango duni baadhi ya sehemu na kukuwa magari yalikuwa mchache tatizo lilikuwa halijioneshi haraka (Sasa kuna malori ya Dangote).
Sidhani Kama kuna utamaduni au pesa za kumaintain barabara zetu kwa wakati.
Hata hivyo, Rais akiona tatizo lazima achukue hatua.
Mameneja watajieleza baadaye.
 
Barabara zinazoharibika na zenye mashimo hatarishi zipo nyingi ikiwemo hiyo ya kusini.
Barabara ya kilwa ilijengwa kwa viwango duni baadhi ya sehemu na kukuwa magari yalikuwa mchache tatizo lilikuwa halijioneshi haraka (Sasa kuna malori ya Dangote).
Sidhani Kama kuna utamaduni au pesa za kumaintain barabara zetu kwa wakati.
Hata hivyo, Rais akiona tatizo lazima achukue hatua.
Mameneja watajieleza baadaye.
Kwani alisema mameneja watumbuliwe?

Amandla...
 
Waziri Kamwele aliwahi kutoa taarifa ya kutowavumilia managers wote wa Tanroad mikoani ambao barabara zao za lami zitakazokuwa na mashimo.

Lkn bado tunaendelea kushuhudia mashimo kwa kiwango kikubwa.

Kongole JPM , ahadi na vitendo viongozi wengine wamebakia ahadi tu! Vitendo hakuna WAFUNDISHE
 
Ndugu zangu,
Kipekee, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu Muumba Mbingu na Nchi kwa kutupa uhai na chakula.
Hili suala la kumsubiri Mh. Raisi ndiyo atatue kero za wanachi katika eneo husika na huku wateule wake aliowateua ili kumsaidia hizi kazi, huwa linanipa maswali mengi sana. Mojawapo ya maswali hayo ni:
  1. Je watumishi hawa huwa hawajui Job description zao?
  2. Kama wanazijua, kwanini huwa hawapo proactive?
  3. Je kunauwezekano kukawa na poor reporting strategies za kazi zao?
  4. Au wengine ni watu ambao wapo tu pale kwa ajili ya kuihujumu nchi?
Kwa mfano, hawa managers wa Tanraoads, huwa hawana bajeti ya kufanya survey katika barabara zao wanazozisimamia? Kwa manager wa Tanroads makini, anayeijua kazi yake, sidhani kama anaweza akachukua zaidi ya siku 30 or 60 hajafanya survey ya kujua hali ya barabara zake mbali na reports anazopata kwa wasaidizi wake. Wateule wa raisi na wafanya kazi wengine wa umma, it's time to change, mnamtwisha zigo kubwa sana Mh. Raisi Magufuli.

Kumbukeni kuna vijana wengi sana wazuri tu wako mtaani hawajapata fursa kama za kwenu. Kwahiyo, fanyeni kazi kwa kujituma sana, msaidieni Mh. Raisi katika kutekeleza nia yake ya dhati ya kuleta maendeleo makubwa katika taifa letu. Tangia Mh. Raisi aingie madarakani, zama za business as usual, zimekwishapita, lakini watu bado wagumu sana kuelewa. Muda wa kuwachekea watu na kuwabebabeba zimekwishapita, na tena tumeingia kwenye uchumi wakati, mtu asiyeendana na kasi hii, bora piga chini na igiza new face. Kunauwezekano wa watu wameshakaa siku nyingi kwenye kazi mbalimbali za serikali mpaka wameshajisahau.

Katika kipindi hiki cha changamoto ya kupata ajira, nilitegemea watu wangekuwa wanafanya kazi to the excellence ili kumaintain kazi zao. Kuna haja ya kazi za serikali kuwa za muda mfupi, naamini mikataba inapokuwa mifupi, watu wangekuwa wanafanya kazi kwa bidii sana kama kwenye private sectors. Watumishi wa umma wanabweteka sana na high security ya kazi zao, na hii kitu ndo kinafanayanga watumishi wengi sana wa umma kuwa wazembe, it's time to review their contracts ziwe za muda mfupi. Mahali nipofanya kazi mimi huwa ni one year contract, but renewable depending on your performance. Ikioneka hujatimiza malengo yako uliyopewa, no renewal of your contract. Kwa kufanya hivi, mtu lazima ufanye kazi to the excellence.

Namalizia kwa kurudia tena, watumishi waumma mpunguzieni zigo Mh. Raisi, baadhi yenu mnatia aibu kabisa nendeni na kasi ya Mh. Raisi katika kuleta maendeleo katika taifa letu.

Asanteni sana,

Nawasilisha,

Kejuu
Yaani mkuu ungejua kinachoendelea huku chini wala usingekuwa na lawama hizo!! Hizo pesa wanazitoa wapi, mafungu mengi ya pesa yanaelekezwa kwenye mambo ambayo hayapo kwenye bajeti, na yaliyopangiwa yana kosa pesa!! Kuna baadhi ya ofisi za serikali hatua inafikia wanakuwa gizani kisa pesa ya kuweka LUKU, hakuna!!! Hapo utamlaumu mkuu wa idara wakati anakwambia hakuna fungu?!! Kama wizarani tu karatasi nyeupe za kutolea risiti tu hakuna kuna nini hapo?!! Hao wanakuwa ni mbuzi wa kafara tu.
 
Back
Top Bottom