Kuhusu kutumbuliwa kwa managers wa Tanroads mkoa wa Pwani na Lindi

Kejuu

JF-Expert Member
May 20, 2020
645
904
Ndugu zangu,
Kipekee, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu Muumba Mbingu na Nchi kwa kutupa uhai na chakula.
Hili suala la kumsubiri Mh. Raisi ndiyo atatue kero za wanachi katika eneo husika na huku wateule wake aliowateua ili kumsaidia hizi kazi, huwa linanipa maswali mengi sana. Mojawapo ya maswali hayo ni:
  1. Je watumishi hawa huwa hawajui Job description zao?
  2. Kama wanazijua, kwanini huwa hawapo proactive?
  3. Je kunauwezekano kukawa na poor reporting strategies za kazi zao?
  4. Au wengine ni watu ambao wapo tu pale kwa ajili ya kuihujumu nchi?
Kwa mfano, hawa managers wa Tanraoads, huwa hawana bajeti ya kufanya survey katika barabara zao wanazozisimamia? Kwa manager wa Tanroads makini, anayeijua kazi yake, sidhani kama anaweza akachukua zaidi ya siku 30 or 60 hajafanya survey ya kujua hali ya barabara zake mbali na reports anazopata kwa wasaidizi wake. Wateule wa raisi na wafanya kazi wengine wa umma, it's time to change, mnamtwisha zigo kubwa sana Mh. Raisi Magufuli.

Kumbukeni kuna vijana wengi sana wazuri tu wako mtaani hawajapata fursa kama za kwenu. Kwahiyo, fanyeni kazi kwa kujituma sana, msaidieni Mh. Raisi katika kutekeleza nia yake ya dhati ya kuleta maendeleo makubwa katika taifa letu. Tangia Mh. Raisi aingie madarakani, zama za business as usual, zimekwishapita, lakini watu bado wagumu sana kuelewa. Muda wa kuwachekea watu na kuwabebabeba zimekwishapita, na tena tumeingia kwenye uchumi wakati, mtu asiyeendana na kasi hii, bora piga chini na igiza new face. Kunauwezekano wa watu wameshakaa siku nyingi kwenye kazi mbalimbali za serikali mpaka wameshajisahau.

Katika kipindi hiki cha changamoto ya kupata ajira, nilitegemea watu wangekuwa wanafanya kazi to the excellence ili kumaintain kazi zao. Kuna haja ya kazi za serikali kuwa za muda mfupi, naamini mikataba inapokuwa mifupi, watu wangekuwa wanafanya kazi kwa bidii sana kama kwenye private sectors. Watumishi wa umma wanabweteka sana na high security ya kazi zao, na hii kitu ndo kinafanayanga watumishi wengi sana wa umma kuwa wazembe, it's time to review their contracts ziwe za muda mfupi. Mahali nipofanya kazi mimi huwa ni one year contract, but renewable depending on your performance. Ikioneka hujatimiza malengo yako uliyopewa, no renewal of your contract. Kwa kufanya hivi, mtu lazima ufanye kazi to the excellence.

Namalizia kwa kurudia tena, watumishi waumma mpunguzieni zigo Mh. Raisi, baadhi yenu mnatia aibu kabisa nendeni na kasi ya Mh. Raisi katika kuleta maendeleo katika taifa letu.

Asanteni sana,

Nawasilisha,

Kejuu
 
Kwanza wamepewa nafasi ya kujitetea tusikie upande wao kabla ya kufukuzwa?

Na hapa siongelei majibizano ya kustukizwa kwenye makamera na rais ambayo yanaweza kuwa kisiasa zaidi.

Naongelea formal due process ya kumuachisha mtu kazi imefuatwa?

Moja ya vitu ambavyo vilimfanya rais Kikwete awe anasita sana kufukuza watu kazi, ni ukweli kwamba aliwahi kufukuzisha mtu kazi bila kufanya uchunguzi makini, baadaye ikagundulika mtu yule hana makosa.

Nchi yetu ina matatizo mengi, siasa, bajeti mpaka watu kutowajibika.

Tumejiridhisha vipi rais kachukua hatua sahihi?

Sisemi kwamba hajachukua hatua sahihi, ila tabia yake ya kusimamisha watu barabarani execution style inaweza kusababisha mtu akafukuzwa kazi kwa sababu kazidiwa maneno na rais tu, au kamuheshimu rais tu hakutaka kujibizana naye.
 
Kwnza wamepewa nafasi ya kujitetea tusikie upande wao kabla ya kufukuzwa?
Je?! Barabara mbovu hapa nchini ni hizo mbili tuu? Hebu waziri apite njia ya Dodoma Iringa ikoje, hebu waziri apite njia ya Mbarali kwenda wilaya ya Songwe kupitia Mkwajuni hadi Shanta Goldmine. kilomita Mia ni masaa matatu.. Kuna maamuzi mengine ya serikali sikubaliani nayo kabisa. Hebu Waziri apite barbara ya kutoka Tengeru kwenda Mererani Simanjiro inako toka Tanzanite.. Tuache uonevu na tumuogope Mungu..
 
Kitu cha msingi ni kama matengenezo ya kazi hizo yako kwenye bajeti na kama yapo, je fedha zilipelekwa huko?
 
Kwanza wamepewa nafasi ya kujitetea tusikie upande wao kabla ya kufukuzwa?
mkuu kwa hali ya barabara ile ya kutoka mavuji kuja nangurukuru haina haja ya kumpa mtu nafasi ya kujitetea ni uzembe wa SGR ule. Yaani wamesababisha mpaka nimeingia gharama ya kubadili tyre zote nne kwenye kimkweche changu, hovyo kabisa.
 
Hapo ndipo tunapokosea.

Ujue hata mwizi akiiba, halafu ukampiga bila kumpa nafasi ya kujitetea, unamtengenezea mazingira ya kupata msemo kwamba ameonewa kwa kuhukumiwa bila kupewa nafasi ya kujitetea.

Kwenye sheria kuna msemo, justice must not only be done, it must seem to be done.

Unajuaje barabara ni mbovu kwa sababu ya uzembe wa watendaji na si kwa sababu serikali haijatoa hela au haijakamilisha mambo fulani huko juu?

Unajuaje lawama zipo kwa huyu mtendaji na si wizarani?
 
sometime mwenye position ya juu anaamua kupiga kifua na kumtumia wa chini kama scape goat ili kulinda image/maslahi yake.
 
Nadhani kuna changamoto katika mfumo mzima wa usimamizi wa barabara. Ninachokiona ni uonezi kwa wasimamizi wa barabara. Kwanza ni kweli kuwa serikali kupitia wizara ya fedha haipeleki kwa wakati fedha za matengenezo na zikipelekwa ni kidogo sana kiasi kwamba haziwezi kufanya ya maana. Pili ni kwa viongozi wa kisiasa kupenda kick kupitia majukwaa ya kisiasa huku wakijua fika kuwa serikali ndiyo yenye tatizo la kukosa fedha. Tatu ni kwa viongozi kuingilia utendaji wa wataalam wake mfano kuwakingia kifua wafanyabisshara wakubwa wanaopitisha magari mazito barabarani kwa kisingizio cha ajira za wapiga kura wao.
 
Haya mambo magumu sana, imebaki siri ya mtumbuaji na mtumbuliwaji...

Ila kwa ushauri tu, wahusika wamhoji na ukweli ujulikane then watende kwa haki.
 
Ndugu zangu,
Kipekee, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu Muumba Mbingu na Nchi kwa kutupa uhai na chakula.
Hili suala la kumsubiri Mh. Raisi ndiyo atatue kero za wanachi katika eneo husika na huku wateule wake aliowateua ili kumsaidia hizi kazi, huwa linanipa maswali mengi sana. Mojawapo ya maswali hayo ni:
  1. Je watumishi hawa huwa hawajui Job description zao?
  2. Kama wanazijua, kwanini huwa hawapo proactive?
  3. Je kunauwezekano kukawa na poor reporting strategies za kazi zao?
  4. Au wengine ni watu ambao wapo tu pale kwa ajili ya kuihujumu nchi?
Kwa mfano, hawa managers wa Tanraoads, huwa hawana bajeti ya kufanya survey katika barabara zao wanazozisimamia? Kwa manager wa Tanroads makini, anayeijua kazi yake, sidhani kama anaweza akachukua zaidi ya siku 30 or 60 hajafanya survey ya kujua hali ya barabara zake mbali na reports anazopata kwa wasaidizi wake. Wateule wa raisi na wafanya kazi wengine wa umma, it's time to change, mnamtwisha zigo kubwa sana Mh. Raisi Magufuli.

Kumbukeni kuna vijana wengi sana wazuri tu wako mtaani hawajapata fursa kama za kwenu. Kwahiyo, fanyeni kazi kwa kujituma sana, msaidieni Mh. Raisi katika kutekeleza nia yake ya dhati ya kuleta maendeleo makubwa katika taifa letu. Tangia Mh. Raisi aingie madarakani, zama za business as usual, zimekwishapita, lakini watu bado wagumu sana kuelewa. Muda wa kuwachekea watu na kuwabebabeba zimekwishapita, na tena tumeingia kwenye uchumi wakati, mtu asiyeendana na kasi hii, bora piga chini na igiza new face. Kunauwezekano wa watu wameshakaa siku nyingi kwenye kazi mbalimbali za serikali mpaka wameshajisahau.

Katika kipindi hiki cha changamoto ya kupata ajira, nilitegemea watu wangekuwa wanafanya kazi to the excellence ili kumaintain kazi zao. Kuna haja ya kazi za serikali kuwa za muda mfupi, naamini mikataba inapokuwa mifupi, watu wangekuwa wanafanya kazi kwa bidii sana kama kwenye private sectors. Watumishi wa umma wanabweteka sana na high security ya kazi zao, na hii kitu ndo kinafanayanga watumishi wengi sana wa umma kuwa wazembe, it's time to review their contracts ziwe za muda mfupi. Mahali nipofanya kazi mimi huwa ni one year contract, but renewable depending on your performance. Ikioneka hujatimiza malengo yako uliyopewa, no renewal of your contract. Kwa kufanya hivi, mtu lazima ufanye kazi to the excellence.

Namalizia kwa kurudia tena, watumishi waumma mpunguzieni zigo Mh. Raisi, baadhi yenu mnatia aibu kabisa nendeni na kasi ya Mh. Raisi katika kuleta maendeleo katika taifa letu.

Asanteni sana,

Nawasilisha,

Kejuu
Magu ameamua kuwatoa kafara hao mameneja kama kawaida yake ili kupata kiki, ila baadaye atawapatia kazi nyingine. Meneja hawezi kufanya ukarabati wakati fedha ni mbinde.
 
Hatari kuelekea uchaguzi huu wa 2020 ni tumbua tumbua nyingi kama upepo wa kisurisuri ila nao Tanroad wanapaswa kujitafakari na waache business as usual
 
Fedha za Road Fund ambazo huwa ni kwa ajili ya ukarabati wa barabara hazitoshi baada ya kuanzishwa kwa Tarura, ambayo pia inachukua hapo hapo. Kabla ya hapo barabara za mitaani zilihudumiwa na Halmashauri kutokana na mapato ya ndani.
 
Magavana wa hiyo mikoa kweli waliangalia tu hizo barabara bila kuhoji? Mameneja husika si huwa wanatoa taarifa kwenye kamati za mikoani na kwa maboss wao wa Makao Makuu ambapo zote zinapelekwa wizarani? Kama kweli kulikuwa na pesa za kutosha kuzikarabati kwa kiwango kinachotakiwa hawa wote wangewaangalia tu?

Amandla...
 
Back
Top Bottom