Kuhusu kughushi Serikalini, Je, Mtu anaweza kushtakiwa hata mfumo unaomlinda ukiondoka madarakani?

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,417
30,927
Kumekuwa na mawazo kwamba ofisi zenye mamlaka zinafanya fojari kwenye taarifa zake kwa faida za kisiasa. Japo hili halijathibitishwa.

Mfano
Mnyika wa CHADEMA amesema hajapeleka majina yoyote NEC ila NEC inasema Mnyika amesaini barua yenye majina ya Wabunge wa Viti Maalum hapa Kuna harufu ya fojari au Mnyika anadanganya.

Swali.

Je, Kama ikithibitika Mnyika hajapeleka majina hayo unaweza ukaitishwa uchunguzi wa kijinai baada ya huyo aliefoji sahihi ya Mnyika kudhaniwa analindwa na mfumo uliopo madarakani Sasa?

Je, Taifa si ni haki lijue mbivu na mbichi juu ya Mnyika vs NEC? Hata Kama ni baada ya 10+ years toka Sasa?
 
Hapa ni muhimu kujua kwamba kesi zote za jinai zinategemea nia ya kushitaki (intention to prosecute) ya serikali iliyopo madarakani kwa wakati huo.
Hivyo basi, ni jambo jema sana kujenga maridhiano na uadilifu kwa jamii na taifa kwa ujumla badala ya kuwaza mashitaka ya kulipizana.
 
Toka awamu hii ya tano imeingia madarakani kuna kugushi na upikaji mwingi wa data ili kuhadaa umma. Ile list ya ajira za waalimu ni aibu ya karne. Kundi lile lile liliondaa uchaguzi wa kugushi, ndio hilo hilo limegushi idadi fake ya ajira za waalimu, ili kuhadaa wananchi kwamba mambo ni mazuri.
 
Ukiona hivyo ujue wale watu waliobebwa au watalaam wa kudesa na waoingia na phantom kwenye mitihani.ndiyo wapepanda vyeo na kukalia ofisi ssa,Luna Haha ya kurudisha special school tuwaandae viongozi toka secondary na kazi ya usalama wa taifa nianze huko kuwafatia viongozi wajao,kuteua viongozi kama mchezo wa karata tatu uta angamiza taifa
 
Wametolewa watu kafara lakini mpango mzima watu wanao wote wale ni vimada wa vigogo wa chama!
 
Ni matendo ya aibu sana na hayapendezi. Tumuogope Mungu wa kweli na tuache Siasa kwenye masuala ya Msingi
Ni maoni yangu kuwa dhambi hii ya kughushi ikizoeleka na kukubalika, basi si maadili tu lakini mengi yata aathirika ikiwa ni pamoja na amani na demokrasia.
Tumwogope Mungu, kuggushi ni uongo na uongo ni sifa kuu ya Ibilisi.
 
Toka awamu hii ya tano imeingia madarakani kuna kugushi na upikaji mwingi wa data ili kuhadaa umma. Ile list ya ajira za waalimu ni aibu ya karne. Kundi lile lile liliondaa uchaguzi wa kugushi, ndio hilo hilo limegushi idadi fake ya ajira za waalimu, ili kuhadaa wananchi kwamba mambo ni mazuri.
Lakini mbona awamu hii wameshughulikia vyeti feki kwa umahiri?
Tatizo liko wapi?
 
Kumekuwa na mawazo kwamba ofisi zenye mamlaka zinafanya fojari kwenye taarifa zake kwa faida za kisiasa. Japo hili halijathibitishwa.

Mfano
Mnyika wa Chadema amesema hajapeleka majina yoyote NEC ila NEC inasema Mnyika amesaini barua yenye majina ya covid 19 hapa Kuna harufu ya fojari au Mnyika anadanganya.

Swali.

Je Kama ikithibitika Mnyika hajapeleka majina hayo unaweza ukaitishwa uchunguzi wa kijinai baada ya huyo aliefoji sahihi ya Mnyika kudhaniwa analindwa na mfumo uliopo madarakani Sasa?

Je Taifa si ni haki lijue mbivu na mbichi juu ya Mnyika vs NEC? Hata Kama ni baada ya 10+ yrs toka Sasa?
Kama jina la nchi lina makosa hayo mengine ni mwendelezo tu wa ujinga wa ccm
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom