Kuhusu kuanzisha Day Care Centers katika mashirika ya Umma na sehemu za kazi

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,856
7,846
Nimekaa nimefikiria sana kuhusu matukio ambayo nayasikia na kuyashuhudia kila siku kuhusu vituko na unyama wa hawa wanaoitwa 'house girls" hasa kwa watoto wachanga na wadogo.

Hali hii imesababishwa na ukweli kuwa, wazazi wengi wanakuwa ni wafanyakazi na hivyo ni lazima waende makazini, na kuwaachia jukumu la kuwaangalia watoto hao ma haouse girl.

Kwa nchi za wenzetu ni kitu cha kawaida sana kwa maeneo ya kazi kuwa day care centers zao. Yaani kwa mfano labda hospitali au shule, utakuta ina day care yake, na wafanyakazi wenye watoto wachanga na wadogo huja nao wakati wakija kazini, na kuwaacha huko;

Kwa hiyo kwa mfano daktari anakuja na mtoto wake hospitali anayofanya kazi, halafu anaenda zake wodini au kliniki kuona wagonjwa wake, na baada ya muda mfupi anaweza kwenda kumcheki na hata kumnyonyesha mtoto wake (kama bado ananyonya), na kurudi tena kuendelea na kazi (kwa sababu hiyo day care center inakuwa ni jengo hilo hilo au karibu sana na hapo kazini). Na muda wa kutoka, anamchukua mwanae anarudi nae nyumbani.

Naona utaratibu huu ukianzishwa hapa kwetu utasaidia sana na kuokoa watoto wetu wapendwa na majanga mengi sana!
Wadau mnaonaje hii idea? karibuni kwa michango Preta gfsonwin The Boss Kaunga ladyfurahia ladyfocus Nifah warumi Senior Boss Evelyn Salt mshana jr tatty rubii Heaven Sent Katavi Tee Bag Pasco ladypepeta Nazjaz farkhina mamyake Pretty Dann94 idawa binti2013 Madame B madame na wengine wote
 
Wazo zuri mkuu! ila jee linatekelezeka??
Kwa nini lisitekelezeke mkuu?? Kunaweza kuwekwa utaratibu maalum ambapo kwa mfano kila mfanyakazi ambae anataka mtoto wake ahudumiwe na hiyo day care labda anachangia elfu 30 kila mwezi!! Siidhani kama watu watakataa, ukilinganisha na headaches na risks za wadada wa kazi!!
Mimi naona inawezekana kabisa, ni kujipanga tuu rubii
 
Wazo zuri mkuu! ila jee linatekelezeka??
Nimetafuta tafuta mitandaoni taarifa zaidi kuhusu hii idea, na nimekutana na article hii hapa... Hebu ipitie mkuu rubii meku7

Providing day care in the workplace can have many benefits for companies, including improving employee morale, lowering turnover and attracting a wider variety of applicants. Although providing workplace day care can be expensive, many companies find that it actually saves money in decreasing employee absenteeism and turnover. Several options exist, from bring-your-baby-to-work programs to on-site day care and cooperatives between small companies.

Ads by Google
Start Download
Convert Any File to a PDF. Get the Free From Doc to Pdf App!
www.fromdoctopdf.com
Employee Benefits
Workplace day care is an important benefit for many employees, allowing them to spend more time with their children during the workday. Some on-site programs allow employees to spend lunch and breaks with their children or for new mothers to pop in and breastfeed. Parents can travel to and from work with their children, increasing the amount of time they spend together. Workplace day care also decreases anxiety for some parents, improving their ability to concentrate on their jobs.

Company Benefits
Workplace day care can improve employee morale and lower absenteeism and turnover because fewer employees need to take time off to look after their children, according to an article in Bloomberg Businessweek. This leads to lower company costs. The same article cites a study in the book “Kids at Work: The Value of Employer-Sponsored On-Site Child Care Centers” in which two large companies saved $150,000 and $250,000 in wages through providing on-site day care. Another big savings is realized in bringing new mothers back to work sooner, allowing companies to save in hiring and training replacements.

Related Reading: What Do You Need to Open a Day Care Center?

Day Care Options
A large company with a high number of employees may opt to open an on-site day care center serving only its own employees. For other companies, a better option may be to partner with a local organization or school to provide services. For example, a shortage of affordable day care in Rochester, Minnesota, led to a partnership between day care provider Child Care Resource and IBM. A new day care facility was built adjacent to IBM, with IBM’s financial assistance. Smaller companies located near each other can consider joining to open a nearby day care cooperative. Another option is partnering with a local day care to accept employee children at a discount.

Disadvantages
Before opting for a workplace day care program, companies need to consider if it is indeed the best option. If too few employees take up the day care places, it could end up costing a lot of money. The day care center must have the flexibility to appeal to a wide variety of parents. On-site day care is not an option for parents with older children. Your company needs to think of ways to accommodate parents with younger school-age children who cannot use day care but still need supervision after school. Providing for workplace day care should be a comprehensive policy, which can take time and resources to develop.
 
Tatizo ni kupata nafasi katika eneo la taasisi, otherwise watu wa kuendesha huduma kama hiyo ni wengi.
Mimi naamini nafasi inaweza kupatikana, hata kwa kuongeza jengo katika taasisi husika; au kuweka day care hiyo karibu na taasisi (umbali usiozidi dakika tano kwa mwendo wa mguu); Hii inawezekana kabisa Rene Jr.
 
Kwa hapa kwetu itakuwa ngumu kupata wateja, watu wamezoea kuajiri watoto wadogo il wawalipe mshahara kidogo na a kuwafanyisha kazi zote za nyumbani, mtu atoe 30,000/ day care bado shughuli za nyumbani zinamsubiri sidhani kama utapata, wengi wamezoea wakirudi nyumbani wanashika rimoti tu, kazi zote dada hata huyo mtoto wengi wananmshika wakiwa wana nyonyesha baada ya hapo dada, ukiangalia miaka ya huyo dada utachoka kabisa, kwa nchi hii utapata wateja watokao nje ya nchi si wazawa aisee.
 
Tatizo utamaduni wa watz ni wa kifigisu figisu ktk maswala ya malezi,cha ajabu utakuta pubs na bar ktk maeneo ya karibu na kazi kuliko huduma za afya na daycare :)
 
Kwa hapa kwetu itakuwa ngumu kupata wateja, watu wamezoea kuajiri watoto wadogo il wawalipe mshahara kidogo na a kuwafanyisha kazi zote za nyumbani, mtu atoe 30,000/ day care bado shughuli za nyumbani zinamsubiri sidhani kama utapata, wengi wamezoea wakirudi nyumbani wanashika rimoti tu, kazi zote dada hata huyo mtoto wengi wananmshika wakiwa wana nyonyesha baada ya hapo dada, ukiangalia miaka ya huyo dada utachoka kabisa, kwa nchi hii utapata wateja watokao nje ya nchi si wazawa aisee.
Umesomeka mkuu, loud and clear. Uko sawa kwa kiasi kikubwa....
Lakini inabidi Watanzania tubadilike kwa kweli, haka katabia ka kutopenda kabisa kujihusisha na malezi ya moja kwa moja ya watoto wetu sijui hata tumekatoa wapi!! Miaka ya nyuma hakakwepo kabisa!
Umeongea jambo la kweli kabisa, nimeshaona wamama ambao inapita hata wiki nzima hajamuogesha mtoto wake yeye mwenyewe, hajamlisha, wala kumbadilisha nepi; Yote hayo ni ya house girl, hata mama akiwepo!! mwasu
 
Yani siku hizi mambo ya kipuuzi yanapewa kipaumbele mpaka utashangaa, mama anatoka kazini anaoga haraka na kujiremba mtoto anamuona na kumlilia anagalau hata ambebe, ndio kwanza mama anamfokea dada kwa nini unamleta mtoto ndani mpaka kaniona hujui leo kuna kikao? unataka nichelewe sio? Nenda nae dukani kanunue pipi, hapo mtoto atalia weee mama huyooo kiguu na njia, sijui nini kimeingia akirudi mtoto kalala, sasa hiyo day care ya masaa nane tu unategemea mama wa aina hii atakuja hata kutaka kujua taratibu za kuleta mtoto?
 
wazo zuri, it is worth giving it a try, napenda sana watu wakiwa wabunifu kama hivi
 
Kwa nini lisitekelezeke mkuu?? Kunaweza kuwekwa utaratibu maalum ambapo kwa mfano kila mfanyakazi ambae anataka mtoto wake ahudumiwe na hiyo day care labda anachangia elfu 30 kila mwezi!! Siidhani kama watu watakataa, ukilinganisha na headaches na risks za wadada wa kazi!!
Mimi naona inawezekana kabisa, ni kujipanga tuu rubii
Hili ni wazo zuri na linawezekana na ni opportunity mpya. Ni suala la serikali kuweka vigezo na sifa za Day Baby Care Centres. Sifa kwa maana ya elimu ya wahudumu na umri wao na mazingira sitahiki ya kituo chenyewe.
 
Kama upo Daresalam unaweza kuanzisha Mazungumzo na wizara husika,ukapatiwa kipaumbele na kufanya pilot Centre maeneo ya Posta Mpya.
 
Kama upo Daresalam unaweza kuanzisha Mazungumzo na wizara husika,ukapatiwa kipaumbele na kufanya pilot Centre maeneo ya Posta Mpya.
Mimi niko Dar es salaam.Hii ni post ya zamani lakini nimeona niichangie, nikuambie mimi nimewahi kujaribu hili jambo tena kwenye Wizara inayoshughulikia watoto, tena jengo lao lina vyumba mbavyo havina wapangaaji . Lakini nilipata jibu ambalo siwezi hata kulisema humu maana kama wadau wa watoto hawawezi kuweka watoto nani atawaweka. Nilifikia wazo hilo baada ya kumaliza kozi yangu ya kulea watoto(ambayo ni moja ya vigezo vya kituo hasa kwa nchi za wenzetu) na pia kuona idadi kubwa ya wajawazito katika jengo na wanaohudumiwa wengi wanakuja na watoto nikafikiri naweza fanya hii huduma hata kwa kuwaweka watoto japo kwa masaa . Kama ukiona sehemu mjini kati mimi naweza kufanya hii huduma
 
Back
Top Bottom