#COVID19 Rais Samia Suluhu: Tutalichukulia kwa uzito suala la COVID-19

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,104
Rais Samia kuunda kamati kushughulikia COVID 19. Amesema ataunda kamati ya kushughulikia kitaalamu.

Amesema hatuwezi kujitenga kama kisiwa, lazima tuunde kamati ijulikane kama tunakubali au tunakaa na si kusikia habari tu za nchi nyingine na ikifika kwa Tanzania hamna kitu.




Rais Samia amesema haya

''Tutaunda Kamati ya Wataalamu kuhusu Covid 19 watuambie kitaalamu hayo yanayopendekezwa na Ulimwengu kuja kwetu yapoje, hatuwezi kujitenga tu kama Kisiwa na hatuwezi kupokea yanayoletwa bila kuweka cha kwetu, bila kufanya utafiti wa kwetu.

Rais Kikwete alituambia akili za kuambiwa changanya na zako, tuweke na zetu tuwe na msimamo maalum unaoeleweka, sio tunasoma tu mambo ya Covid 19 Ulimwenguni, Tanzania deshi deshi deshi haieleweki, tueleweke kama tunakubali au tunakataa

Suala la Covid 19 nafikikiria niunde Kamati ya Wataalamu waliangalie kwa upana wake kitaalamu halafu watushauri Serikali, halifai kulinyamazia aidha kulikataa au kulikubali bila kufanya Tafiti za kitaalamu''


Samia.jpg
 
Hivi Tanzania haikuwa na ushauri wa kitaalamu na JPM marehemu maamuzi ya corona na hatua alizochukua hakuzingatia ushauri wa wataalamu?

Fitina za aina hii kwa marehemu na utafutaji uungwaji mkono kwa njia hii hazitamsaidia mtu.

Je, anataka Watanzania wa amini suala la corona halikuchukuliwa kwa uzito? Ama ndio njia ya mzunguko kwenda kukubaliana na chanjo za WHO na wajasiriakorona.
 
Nyungu na mauchawichawi mengine TUPA KULEEE. Mataga mtatotowaaaaaa mwaka huuu.
Unajidanganya, nyungu kama kawa na inafanyiwa utafiti na matokeo watapewa WHO waamue lakini nyungu ni tiba dunia itaitambua, Uingereza corona imewashinda wameamua kuchukua approach ya Tanzania ya kuishi nayo, no lockdown ,no carfew.Magufuli alikuwa akili kubwa alijua dude corona si la kuendea pupa, mtahangaika sana.
 
Hivi Tanzania haikuwa na ushauri wa kitaalamu na JPM marehemu maamuzi ya corona na hatua alizochukua hakuzingatia ushauri wa wataalamu?

Fitina za aina hii kwa marehemu na utafutaji uungwaji mkono kwa njia hii hazitamsaidia mtu.
Kwa hiyo unaamini ni fitna si ndio ? Akili za kishenzi kabisa.

Acheni afanye anvyoona, si ndio uhalisia anaaona yeye?
 
Back
Top Bottom