Hute
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,537
- 6,463
1. Tuseme ukweli, hivi mimi nizae mtoto halafu watu wachache tu wanaokipenda kiswahili waniamulie kuwa mtoto wangu lazima asome kwa lugha ya kiswahili wakati mimi kiswahili sikipendi?
2. mimi kiswahili nimeanza kuongea kwa ufasaha nilipofika miaka 12, na hadi nafikia form two nilikuwa na kiswahili kibovu tu, my mother tongue ni kilugha (mojawapo ya makabila ya tz).
3. kati ya maprofesa wale wenye manywele pale udsm wanaoshabikia kuturudisha nyuma watoto wetu waanza kusoma kila kitu kwa kiswahili, ni wangapi watoto wao hawajapelekwa English medium, wangapi watoto wao wamepelekwa kwa kayumba wanakofundisha kwa kiswahili?
4. kati ya wale maprofesa wa kiswahili pale udsm, ni wangapi wanajua kuongea kiingereza fasaha? wasije kuwa hawajui kiingereza sasa wamekichukia wanafikiri kila mtu ni kama wao!
5. maprofessa wa tz pale udsm wangapi wametunga vitabu vya sayansi, na masomo mengine yoote?
6. ni vitabu vingapi ambavyo maprofesa wenzao wa nchi zingine ambao ndio wenye akili, wamepata leseni ya kuvitafisiri kwa kiswahili ili tuvisome kwa kiswahili? tuanze leo kusoma physics kwa kiswahili, tusome biology, na masomo mengine yoote ya vyuo vikuu kwa kiswahili (wakati wao hawajatunga hata kitabu kimoja cha kitaaluma, zaidi ya kutunga vitabu vya lugha ya kiswahili tu).
7. wakati wengine kama Rwanda na nchi zingine, wanapambana nchi zao zitumie English, maprofesa wa kitanzania wanapambana kuishawishi tz itumie lugha ya kiswahili wakati tupo kwenye east africa community.
8. kati ya wasomi woote wa tz, viongozi woote kuanzia rais hadi wakurugenzi na walimu wa vyuo vikuu woote nchini, madaktari nchi nzima, wanasheria nchi nzima, mainjinia, na wasomi woote, kati yao ni nani watoto wake wanasoma kayumba? kati yao ni nani atakubali watoto wake wakasome kwa lugha ya kiswahili?
9. hivi hawa maprofesa huwa wana akili au wanatafuta dili ya kutafisiri vitabu walivyotunga wenzao ili watoto wetu ndio wavitumie?
10. wanasema (hasa yule aliyeongea itv mwenye manywele kama nini sijui) anasema nchi zote zilizoendelea zimeendelea kwa lugha zao. tuambie vitu unavyonunua toka china, japan etc, vingapi vinatumia kijapan? hata katika biashara zao zote wanatumia lugha za wengine. nenda india kutibiwa baada ya kuvimbiwa ugali huko udsm, pale utakuta kingereza tu na wakati huohuo na kihindi kinatumia.
11. ushauri wangu kwenu maprofesa wa udsm, acheni ushamba, hatutaki watoto wetu wasome kwa kiswahili, tunapambana watoto wetu wasome kwa kiingereza ili waweza kujua lugha ya dunia wasipate shida kama ninyi maprofesa mkitoka nje mnavyopata shida kwa kushindwa kuongea kiingereza kwa kujifanya mnatukuza kiswahili wakati kiswahili wala sio lugha yenu, wengine hapo wahaya (kama wewe uliyeongea itv) wengine wachaga, wengine wahehe, wengine wanyakyusa etc. msiturudishe nyuma, bora tupeleke watoto wetu wakasome kenya na uganda kukwepa kiswahili chenu. hivi usomi wenu uko wapi? upo tu kwenye makaratasi au hata kwenye kufikiri?