Jamani mimi nashangaa kitu kimoja.Kama bodi ya mikopo mwaka huu haitoi mikopo kwa wanafunzi wenye EQUIV QUALIFICATION kulikuwa na haja gani ya kuweka vigezo vya EQUIV QUALIFICATION kwenye form zao walizotoa za kujaza online?.Pia kwa nini wasingetangaza kuwa wenye EQUIV QUALIFICATION hatapewa mikopo ili watu wa-apply wakijua kuwa chuo watasoma kwa kujilipia?....Vinginevyo wamekaa kimya na mbaya zaidi wametupotezea muda wa ku-apply kumbe tungefanya utaratibu mwingine wa kujipanga.