Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,193
- 25,504
Mwanzo mwanzoni naomba nijiepushe kuingia kwenye mjadala juu ya uhalali au uharamu wa kufutwa kwa Ubunge wa Joshua Nassari wa Arumeru Mashariki. Sababu yangu kuu ni moja:jambo hilo ni la kisheria linalohitaji kujadiliwa,ushahidi na tafsiri ya kikatiba na kisheria. Mahali sahihi ni mahakamani,hususani Mahakama Kuu ya Tanzania.
Iliripotiwa humu JF kuwa mshahara wa Mbunge wa Singida Mashariki na Wakili Msomi mwenzangu Tundu Lissu umesitishwa kufuatia kile kinachosemwa kuwa Bunge (uongozi wa Bunge) halijui alipo Tundu Lissu. Hoja ya kutojulikana alipo Lissu ndiyo mzizi uliositisha mshahara wake.
Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi Septemba mwaka 2017. Ingawa sijui idadi halisi ya Mikutano ya Bunge iliyofanyika tangu hapo,naamini mikutano mitatu inafika. Najua na kuamini kuwa Lissu hakuhudhuria vikao na mikutano ya Bunge tangu hapo Septemba 2017. Amekuwa akipokea matibabu ya majeraha take yaliyotokana na shambulio dhidi yake.
Pamoja na kutohudhuria kwake Bunge kwa kipindi chote hicho,Ubunge wa Lissu umebaki na haujafutwa au kusitishwa. Maana yake ni nini? It means and implies kwamba Lissu ana sababu za kueleweka na za kihalisia za kutohudhuria. Also,it means and implies that uongozi wa Bunge unazijua sababu hizo na umezikubali.
Kubaki kwa Ubunge wa Lissu hadi sasa ni kukubalika kwa sababu zake na uongozi wa Bunge. It also means and implies that alipo kunajulikana na anachokifanya kinajulikana. Iweje mshahara wake usimamishwe ikisemwa hajulikani alipo?
Naamini kuwa alipo Lissu panajulikana na uongozi wa Bunge ndiyo maana Ubunge wake unaendelea. Wangapi na akina nani watakubalina au kupingana nami? Jumamosi njema waungwana na wazalendo wa Tanzania!