faru john junior
JF-Expert Member
- Dec 26, 2016
- 1,596
- 1,717
Habari za mchana wadau wa JamiiForums
Kama kichwa cha habri kinavyoeleza, ningependa kupatiwa ufafanuzi katika hili jambo. Leo asubuhi nimeenda hospital ya agakhan pale makao makuu karibu na bahari kwa wale wanaojua raman ya Dsm,na lengo ni kupata huduma ya matibabu nikitumia bima ya afya. Mimi ni mtumishi wa umma moja ya shirika kubwa hapa nchini .
Kilichonishangaza ni kwamba kadi yangu ya bima walikataa kunipatia huduma kwa madai kuwa kadi yangu haina nembo ya shirika ninalolitumikia kwani bima zote za serikali wanazopokea zina nembo au majina ya mashirika husika.
Kwanza nilshangaa kidgo kusikia hivyo kwani kadi yangu haikuwa na hyo nembo kama alivyodai mtoa huduma. Lakini hyo haikuwa shida sana ila nikaendelea kumuliza kuwa hawa wenye hizo kadi zenye nembo au majina ya taasisi husika kuna nini hasa tofauti na mm japo nilimweleza ni taasisi gani natoka.
Majibu niliyopewa ni kwamba hizo taasisi huwa zinatoa fedha ya nyongeza tofauti na ile ambayo wangekata kutoka kwenye mfuko wa bima ya afya. Alinitajia badhi ya taasisi ambazo hutoa fedha za ziada kwa watumishi wake kutibiwa pale ni kama bank kuu BoT, TRA.
Sasa swali langu ni kwamba je serikali haioni kuwa huu ni ubaguzi kwa watumishi wasio patiwa hyo nyongeza ya malipo? Watumishi wa umma na serikali ni sawa baba/mama na watoto wake je kuweka ubaguzi wa wazi kiasi hiki haoni kuwa ni kudidimiza huduma hasa upande usio pata hicho kipaumbele?
Je, hao TRA na BoT wataweza kufanya kazi vzri bila kumtegemea nesi, mwalim,polisi, nk?
Asante sana