Kuhusu Bandari ya Bagamoyo na Umeme wa Gas, Ndugu Job Ndugai na Prof. Muhongo wamechemka big time!

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,651
5,125
Ndugu Watanzania wenzangu, pamoja na siku 21 za kuomboleza kifo cha Hayati Dr. Magufuli kuisha. Mimi bado naomboleza mpaka 40 yake ipite!

Kuna makala yangu moja humu JF niliwahi kumtahadharisha Hayati Rais Magufuli kuhusu wanafiki walio mzunguka!

Nilimwambia akiondoka madarakani hakuna hata muda wa hawa wanafiki kujisumbua kutaja hata majina yake yote manne eti DR. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI!

Wanafiki wanaofurahia kifo cha Hayati Rais Magufuli ni wengi mno!

Lakini ninalotaka kuwambia Watanzania wenzangu leo ni kwamba yote kwa yote lakini hawa watu wawili(2) Job Ndugai na Sospeter Muhongo ni watu wa kuwachunga na kuwaogopa kama ukoma! HAWAFAI! ni ma- puppet leaders!

Suala la Bandari ya Bagamoyo, Mwendazake Hayati Rais Magufuli aliwahi kulifafanua kwa kina sana na zile facts za Rais Magufuli kama ndo ziko kwenye hilo li mkataba lao basi mtu MPUMBAVU TU ndiye anaweza kufuata mawazo ya JOB NDUGAI.

Kwa watu tunaofuatilia "Conspiracy theories" kama mimi FK , bado napata mashaka sana kama "the demise of JPM is a natural death'

Niki- link hizi "dots " akili yangu inakataa kukubali kwamba Hayati Rais Magufuli amekufa a natural death!

The first dot: Rais Magufuli akataa Wachina kujenga SGR.

The second dot: Rais Magufuli awanyima Wachina kandarasi ya kujenga Nyerere Hydroelectric Dam.

The third dot: Rais Magufuli apiga chini Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo!

The fourth and the most recent dot ni pale Rais Magufuli alipogundua ufisadi wa kutisha wa Wachina kupitia Benki yao hapa Nchini (kama sikosei ni CHINA BANK) na kuwaweka lupango Wakuu wa Bank hiyo!

Na katika ku- reconcile hilo katika " high profile" level ndo kukapelekea ujio wa Waziri wa Mambo ya Nje wa China moja kwa moja hadi CHATO.

Yawezekana kabisa Hayati Rais Magufuli aliweza kujizungushia mitutu mingi lakini hakuzungukwa na watu "SMART"

Hawa Wachina tunao- deal nao leo si wale Wachina wa Mwl. Nyerere.

Sasa hizo dots hapo juu unganisha na kelele za JOB NDUGAI kuhusu BANDARI YA BAGAMOYO. You can smell something "gargantuan"

Wachina hawa wanataka kui- colonial ize Afrika kupitia MADENI na MIKOPO! They are so worse everywhere kuanzia KENYA, ZAMBIA, SRI- LANKA n.k. Hayati Rais Magufuli alitutoa kwenye KITANZI cha MADENI ya CHINA yasiyolipika sisi na VITUKUU vyetu (Mkataba wa Miaka 99!) CHINA IS A SCAM!

Ukija kwa huyu Professor wa "Mawe" Sospeter Muhongo ambaye mimi namuona newbie "mweupe" kwenye business world, kumbuka wakati wa Escrow saga huyu "Msomi" ndo alisema baada ya kuona "payslip" ya Bank ya PAP akajua tayari PAP iliinunua IPTL bila kuona " Certificate of transfer of shares "zilizolipiwa na kuwa taxed!

Leo huyu Professor wa "Mawe" anatuambia tuache mradi wa umeme wa maji ambao umekamilika kwa 50% turudi kwenye Gas ambayo alishaiiuza kwa Mabwana zake na yeye kubaki kuwa dalali wao!

Yaani tuache umeme wetu wenyewe ambao utatushushia gharama ya unit moja kutoka Tzs.660 ya sasa tunayolipa TANESCO hadi Tzs.36 (shilingi thelathini na sita tu) twende kwenye umeme wa Gas wa Professor wa "Mawe" na Mabwana zake ambao watatuuzia pengine kwa Tzs.1000 (elfu moja) kwa unit!

Hii itakuwa ni akili au MATOPE?!

Mtuache kwanza tuomboleza kifo cha MWAMBA HAYATI DR. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI.

Na pia MAMA nakushauri sana kuwa macho na hawa watu JOB NDUGAI, PROF. MUHOGO, DR. KIGWANGALA na wengineo, hawa ni wanasiasa MASLAHI wana macho ya UGALI TU hawana lolote wasikudanganye eti wanakupenda!

Kama Rais Magufuli aliwaamini na kuwapa vyeo leo hata mwezi haujaisha wamemgeuka itakuja kuwa wewe.
MAMA KUWA MACHO! "MAZA BE EYEZ"!
 
Huu mradi sijui kwanini unamvutano hivi.

Yote sababu ya kale kajamaa fulani pande zile kulee.
 
Acha porojo wewe, watu wanasubiri mkutano mkuu wa kusikiliza rufaa. Mfalme amehutubia ufalme wake jana wala hakusema mkutano mkuu utakaa lini!
 
Kuhusu mradi wa bandari ya Bagamoyo The late President mbona yeye alivioanisha!

Na huo mkataba ulionekana kuna vipengele vya hovyo. Sasa hao wanaotuambia mradi wa bagamoyo uendele rais alidanganywa
Watuweke huo mkataba.

Ova
 
Back
Top Bottom