Kuhusu Arusha: Slaa ni tatizo, najuta kumpa kura - 2

Hukumpa Kura Dr Slaa, hukuwa mwanachama wa CDM tangu uzaliwe, huenda wewe ni Makamba snr, hujafanya utafiti badala yake umeropoka bila kuchambua sheria zinasemaje kuhusu maandamano ya watu ikiwemo hiyo ya CDM. Mtu mzima hovyo, na bado sasa maandamano tunajimwaga tu hakuna wa kuturudisha nyuma; p olisi wa Tanzania wamekuwa wauaji wa rai wasio na hatia
 
Achaneni na huyu Mpumbavu anayetumwa na Tambwe Hiza( mzee wa propaganda) na MAkamba mropokaji. Tujadili mambo ya maana kama Dowans na katiba mpya, huduma za jamii n.k
 
Maada zingine kwa kweli, du! Hata hii nayo itupotezee muda wa kujadili...nway hii ndiyo faida ya mjadala au kujadili, kujiandaa kusikiliza au kusoma hata vitu usivyovipenda ambavyo hata hivyo akili ya kawaida kabisa inakwambia hakuna usumbufu wowote wa akili uliofanyika kabla ya mhusika hajaandika au kuzungumza.

Tunayo matatizo makubwa ya watu wanaopata nafasi 'nyeti' za kuandika katika magazeti yetu haya, wengi wao ni watu wa hovyo kabisa, katika uwezo wa kutumia faculties za ubongo, kuchambua mambo kwa faida ya audience yao ambayo, kwa mwandishi yeyote anapaswa kujua kuwa hadhira yake ni heterogeneous....

Eti mtu anajenga hoja kuwazuga wajinga wenzake kuwa alimpatia kura Dkt. Slaa kisha hapo hapo anasema "Najiuliza ujasiri wa kuichimba mkwara serikali kaupata wapi! Nastaajabu kuona kwamba mtu huyo, eti aliwahi kusimama kwenye mimbari na kuhubiri Neno la Mungu. Ni padri gani anayeweza kuwa mchochezi."

Hivi Dkt. Slaa kaanza kuichimba mkwara serikali leo!!!!!!!!!!!!!!, kwa ishu ya Arusha, amekuwa akiichimba mkwara, kwa hoja jadidi, kwa miaka 10 sasa, tena nayo inagwaya mbele yake kuonesha kuwa yuko sahihi all the time....kama ni uchochezi (kama kwa definition ya serikali, CCM na vibaraka wao hata kusema kuwa shule za kata ni hovyo ni uchochezi) nao pia aliuanza muongo mmoja uliopita, tena kwa kupitia hata bungeni na mikutano ya hadhara...huo ndiyo umesaidia kuondoa blanketi kubwa ambalo wananchi walifunikwa karibu nusu karne.
 
jamani mie naona viongozi wa chadema sio waliosababisha mauaji nina wasiwasi naile inteljinsia ya polisi ilikuwa nini? mbona siku ya mazishi polisi walitulia na watu wakamaliza shughuli yao? siasa za mabavu siku zote lazima zimwage damu
Sidhani kama nchi inastahili kuendelea kuwavumilia wanasiasa wa aina hii.
 
MMMMH Wana-JF....you are great thinkers....n great thinkers are not biased.......msimtukane...katoa mtazamo wake tu........................nahisi tuna CDM Tawi la JF
 
Any racial reconciliation we've had in this country has come not out of confrontation but out of a spirit of reconciliation. If we continue to practice an eye for an eye and a tooth for a tooth, we'll eventually end up with a land of people who are blind and toothless..
 
Back
Top Bottom