Kuhusu Arusha: Slaa ni tatizo, najuta kumpa kura - 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuhusu Arusha: Slaa ni tatizo, najuta kumpa kura - 2

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Freestyler, Jan 25, 2011.

 1. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mara sehemu ya kwanza ya makala haya ilipotoka wiki iliyopita, nilipata taarifa ya mshtuko. Nilinasa sherehe za watu wanaochekelea. Wanadai vurugu za Arusha zimefanikiwa kuwaweka juu.

  Ni ile ile falsafa ya siasa za majitaka. Kwamba baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wanaona Arusha ni mtaji wa kuwaweka hai kisiasa. Kufa kufaana!

  Sidhani kama nchi inastahili kuendelea kuwavumilia wanasiasa wa aina hii.

  Wapo radhi kuona damu inamwagika, watu wanakufa ili kutimiza matakwa yao kisiasa. Serikali ikigoma kumuadhibu, wewe mwananchi chukua hatua kwa kumchukia moja kwa moja.

  Nasikitika kwamba kura yangu kwenye Uchaguzi Mkuu 2010 niliitumbukiza pasipostahili. Nilimpa aliyekuwa Mgombea Urais wa CHADEMA, Willibrod Slaa (pichani)ambaye nimebaini kuwa hafai hata kidogo.

  Slaa ni chanzo cha mauaji ya Arusha. Najiuliza ujasiri wa kuichimba mkwara serikali kaupata wapi! Nastaajabu kuona kwamba mtu huyo, eti aliwahi kusimama kwenye mimbari na kuhubiri Neno la Mungu.

  Ni padri gani anayeweza kuwa mchochezi. Anayewatuma watu wakauawe! Nasikitika kuona kwamba mpaka leo, bado kuna wananchi hawajataka kukubali ukweli.

  Slaa aliwatuma vijana wa Arusha wakauawe kwa sababu alijua polisi kuna nini. Anafahamu kwamba vituo vya polisi, hasa vikubwa vina zana za kila namna kukabiliana na wahalifu. Unauliza bunduki polisi?

  Akifahamu hilo, yeye aliwaamrisha vijana kwenda kuvamia kituo cha polisi na kuwatorosha, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema. Alitegemea nini?

  Je, polisi wangekubali kuvamiwa, wapigwe, wauawe? Ni dhahiri Slaa alijua kwamba vijana wangekabiliana na jibu la kijeshi ambalo lingegharimu maisha yao. Hicho ndicho kilichotokea. Alifanya makusudi.

  Alitamani watu wafe ili ajiongezee mtaji wa kisiasa. Alikosea kupita kiasi. Damu za wahanga wa Arusha itazunguka kwenye kichwa chake. Aliwatuma yeye, basi kama si duniani, mbinguni atahukumiwa.

  Kama nilivyouliza wiki iliyopita, kwa nini Slaa hakusimama mstari wa mbele kwenda kuwatorosha Mbowe na Lema? Aliagiza tu, yaani yake ndiyo roho, za wale vijana ni nini? Ni kama msemo risasi kwa tembo, binadamu aah!

  Alijifanya mshika rimoti na kubonyeza, akaagiza, “nendeni kituo cha polisi, mumlete Mbowe na Lema kabla sijaondoka hapa.” Inawezekana serikali inamlea kwa sababu ya kuhofia kelele za jumuiya ya kimataifa.

  Je, tunastahili kuwalea watu wa aina hii kwa sababu ya woga wa jumuiya za kimataifa? Watanzania tuepuke, tujifunze hulka za wanasiasa, tutambue kuwa wao ni ‘sosi’ ya migogoro ya nchi nyingi na mauaji ya wenyewe kwa wenyewe.

  Ni busara kila Mtanzania akawa macho, aepuke kutumiwa na wanasiasa. Tuchuje maneno ya jukwaani kisha tuyaweke mbele yale yenye masilahi kwa taifa, yenye rangi mbaya tuyapuuze kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

  Wanasiasa maskini wa hoja hawafai. Hao ni rahisi kutupeleka kwenye machafuko. Wakigundua hawana ajenda ya kuwafanya watengeneze vichwa vya habari, wanakosa amani, hivyo wanaamua kufanya uchochezi na kuyaweka rehani maisha ya wananchi.

  Ajenda ya katiba mpya ilipomezwa na Rais Jakaya Kikwete, wakaamua kugeukia Arusha. Ni vizuri wanasiasa wakawa wakweli kwa wananchi, si kusema uongo ili kujipa ushindi wa mezani. Propaganda zilizopitwa na wakati.

  CCM na Chadema wote wamecheza rafu Arusha. Ni kama aliyeuziwa cheni ya bandia naye akatoa fedha feki. Ajabu ni kwamba makosa yao, mauti yanawaangukia wananchi. Ni kama nyasi kusiginwa wakati wa mechi ya watani wa jadi.

  Kama Chadema walidanganya kwa Rebecca Mngodo (Mbunge Viti Maalum), CCM nao walicheza ‘faulo’ kwa Mary Chatanda ambaye inadaiwa uwakilishi wake ni Tanga lakini alipelekwa Arusha makusudi kuongeza kura.

  Chadema hawaelezi ukweli kwamba Arusha, CCM ina madiwani wengi kuliko wao. Wanataka uchaguzi wa Meya urudiwe ilhali hata wakifanya hivyo, bado chama tawala kina nafasi kubwa ya kutetea. Kina wapiga kura wengi ndani ya halmashauri ya jiji.

  Tatizo hapa ni kwamba wanawatumia wananchi kama mitaji yao, kwa hiyo wanaendelea kuwazuga kwa hoja za kizamani. Wamechagua kuwa wapinzani, kwa hiyo wanapinga kila kitu. Mtu kashindwa anadai kachakachuliwa, anaambiwa athibitishe madai yake, anashindwa.

  Nasikitika kwamba uchaguzi ulishapita na kura nilishaitumbukiza pasipostahili. La kujifunza ni kwamba siku nyingine kabla sijachagua, nitachanganua vilivyo aina ya mtu ninayemtaka.

  Nashukuru Mungu hakushinda, maana leo ningejuta zaidi.  [FONT=&quot]Source
  [/FONT]
   
 2. matuse

  matuse Member

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15

  Kwa uwezo wako wa kufikiria na kuchambua mambo lazima ulimchagua mkwere usitudanganye
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  :msela::msela::msela:Umepata chai asubuhi kabla ya kuandika?:bange::bange::bange:
   
 4. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tambwe Hiza,
  acha kutudanganya source ya mauwaji siyo Dr.Slaa bali ni ukiukwaji wa taratibu na demokrasia kwenye uchaguzi wa meya.:nono:
   
 5. WAKUNJOMBE

  WAKUNJOMBE JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  umetumwa namafisadi eeehhhhhhhh...............wamekupa how much?

  Yaani njama za ccm zote tunazijua.......hutudanganyiki

  hebu nikuulize.......maana inaonyesha hujui nn maana ya kuandamana?

  Hivi wale wanchi kule mbeya walio andamana na kuchoma gari la mafuta plus kituo cha mafuta kisa matumizi ya barabara walitumwa nanani?...... Slaa?

  Hivi haya maandamano ya vyuo vikuu yanayo endelea vyuoni wanatumwa na nani?.........ni slaa pia

  issue ni hivi........wananchi wamechoshwa na mafisadi toka ccm

  na nikutaarifu tunakokwenda kunamaandamano ya kufa mtu........yaani watu wataona risasi kama vile maji pindi wakidai haki zao ........kama huamini waambie hao mafisadi wajilipe hizo hela za dowans...

  Kila kwenye maandamano kunasababu za msingi..........aliyekwambia slaa aliuwa ni nani usidanganyike na mikaanda ya video iliyo chakachuliwa na mafisadi
   
 6. Didia

  Didia JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 721
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Freestyler amehamisha habari kutoka mtandao wa udaku (Global Publishers) wala hajaonesha maoni yake nini katika udaku huo. Sijui lengo la post hii ni lipi au nikuwa na idadi kubwa ya post?
   
 7. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  freestyle.... kwenye signature yako.... umekosa nukuu kabisa katika moja ya viongozi wowote hapa duniani mpaka ukaamua kumnukuu Yusuf Makamba...?
   
 8. F

  Fareed JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Source ya maandiko haya ni Global Publishers, kampuni inayochapisha magazeti ya UDAKU na kumilikiwa na kada wa CCM Eric Shigongo. Moderators futeni hii thread tafadhali, msiruhusu JF kutumiwa kueneza mambo ya UDAKU. After all, this is "The Home of Great Thinkers." Si jamvi la kuchambua habari za UDAKU. Ebo?
   
 9. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #9
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Mkuu huyo ni Mzee Yussuf mwimbaji wa taarab..siwezi kunukuu kauli ya Makamba hata siku moja! Unajua kwa nini>
   
 10. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Unataka tuamini ww ni CDM wakati ni Ccm ? Hicho ulichoaondika ni pripoganda za akina Tambwe hiza darasa la saba
   
 11. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #11
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Lengo langu lilikuwa ni tofauti,nashukuru umeona maudhui na umegonga nyundo! Sikutaka kuiweka mapema kuepuka 'bias' ya mawzo.
   
 12. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #12
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wala sijataja uanchama wangu kwenye hili na halikuwa lengo langu.Shambulia mada usishambulie mtoa mada!
   
 13. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #13
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Vilevile source haibadilishi malengo ya mtoa makala..alichoandika ndicho alichoandika!
   
 14. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Invisible kuna mtu anakuhitaji huku.
   
 15. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  mkuu... topic uliyoleta hapa JF ina kichwa cha habari...slaa ni tatizo Arusha, najuta kumpa kura....ikimaanisha haya ni mawazo, mtazamo na maoni yako..... iweje sasa unamtumpia mzigo mtoa makala......wakati wewe ndio mtoa mada hapa JF
   
 16. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #16
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Si mawazo yangu.Nimeedit 'heading'....
   
 17. m

  mcheshi JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 769
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Inawezekana hata kuona uoni wewe.Au unatumia miwani ya mbao!Au mgonjwa wa akili.Umasikini na maradhi viwe juu yako maana unavipenda sana.
   
 18. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  kwakuwa ume edit heading... itakubidi u edit thread replies zote ili kuwe na mtiririko sahihi
   
 19. n

  ngoko JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nani kasema uchaguzi ukirudiwa kwa kufuata utaratibu mshindi lazima awe Chadema ?
   
 20. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #20
  Jan 25, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  km unatafuta kazi ya uandishi wa habari mskala km ukiipeleka tbc radio uhuru daily news uhuru na mzalendo na habarileo wanakupa kazi fasta lkn hapa kwenye visima vya fikra tunakuona km unajifunza abcd pale saint halmashauri.
   
Loading...