NGWANA ANGELINA
Member
- Mar 25, 2017
- 70
- 44
Ndugu wanajamvi,
Kwanza naomba niwatakie mapumziko mema ya sikukuu ya wafanyakazi, najaribu kutafakari kauli ya serikali ambayo mkuu wa kaya anaiongelea kila anapohutubia kuwa mwaka huu serikali itaajiri zaidi ya watumishi elfu hamsini.
Je ni watumishi wapi au kada zipi ambazo serikali ina mpango wa kuajiri? Maana vijana walioko/tulioko mtaani ni wengi na kila mtu kasomea kada fulani, mfano kuna waliosoma Engineer, Clinical officer, Pharmacy, Account, Social programs, Banking, IT, ADM, nk. Kwa kweli watu ni wengi sana, kwa mtazamo wako unadhani serikali imelenga wapi zaidi?
Je na hawa watakaoajiriwa (ikitokea kama ni kweli) watapelekwa kufanya kazi wapi? maana naona taasisi kama TRA, TPA, Bank kama Posta na NMB hata TANESCO wanatangaza nafasi na kuajiri ama wao hawahusiani na utaratibu wa ajira za serikali?
Hebu tusaidiane kueleweshana tafadhali ili wengine tuendelee kujipanga zaidi kuliko kuendekeza matumaini.