dalalitz
JF-Expert Member
- Sep 6, 2013
- 3,418
- 1,980
Binafsi sina ushirika, Ukaribu wala uhusiano wa namna yoyote na Mtanzania Tundu Lisu.
Mwana sheria mahiri makini na mwenye kofia kadhaa za Kitaaluma, Kisiasa, Kiharakati na nathubutu kusema raia Mzalendo ingawa baadhi ya watu hawamkubali kwa unafki tu.
Silazimiki kueleza wasifu wake hapa Ila tu itoshe kusema:
Akiongea inaonekana dhati katika kupigania Haki na maslahi ya Mtanzania wa kawaida kutoka katika rasilimali ya Madini, Mafuta na Geti.
Binafsi,
Nimeanza kumsikia na kumuona kupitia vyombo mbalimbali vya habari akiwa katika juhudi na harakati mbalimbali kabla hata hajawa Mbunge.
Mara nyingi pengine ni kutokana na umahiri wake kwenye nyanja ya sheria nimekuwa Nikisikia akilalamika juu ya uwepo wa sheria zisizofaa na zisizo na Maslahi stahili kwa Tanzania,
Hiki ndicho zaidi kimekuwa kilio chake siku zote tangia Enzi hizo zaidi ya miaka Kumi iliyopita.
Hata hivyo,
Siwezi na sitaki kuwa mtetezi wake kwenye kila jambo Ila waswahili Tunasema Mnyonge.........?
Wanaokinzana nae hata hivyo wamegawanyika,
Wapo wanaochagizwa na nguvu za Kisiasa lakini pia wapo 'Bandera fuata upepo'.
Ukweli wa mambo ni huu:
Mikataba mingi katika Nchi hii ina walakini na haifaidishi Nchi na wananchi.
Hili lipo wazi na Ushahidi unatokeza kila uchao sasa kumpuuza na kumkejeli Mtu ambae amekua akiyapigania haya kelele miaka na miaka ni kudhihirisha kiasi gani hatujitambui.
Au hadi afe ndio tuanze kumsifia?
Tuache unafki, Mungu hapendi.
Kwa mwenye Akili yenye afya nipe dokezo:
Unajua Kwanini wenye Makinikia tunaaminishwa ni Wezi-wetu lakini hatuwastaki?
Usinijibu, Teheee!
Nawasilisha.