Kuhudhuria Msiba wa Kibaka ' Maarufu ' Mtaani ni Kujitafutia Thawabu au Laana zaidi kutoka kwa Mwenyezi Mungu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,054
107,538
Kuna Kijana Mmoja ambaye nadhani kama kungekuwa na Shindano la Kutafuta Vibaka Bora Tanzania nzima nina uhakika kila mara angeibuka Mshindi ila baada ya Sisi Kaka zake na Wanajamii kila mara Kumuasa na Kumuonya aachane na hiyo tabia mbaya ( japo na Sisi pia alikuwa akituibia ) hakutaka Kutusikia na hatimaye Jioni hii alienda Kuiba mahala na wamemuua.

Cha Kunishangaza kabisa wakati Mimi nikikataa kabisa kwenda Msibani Kwao kwakuwa sijaona na sioni Tija yoyote ile ya Kuhudhuria Msiba wake huyo Kibaka mzoefu kuna Watu kadhaa ambao hata Wao walishaibiwa nae mno Vitu vyao vya Thamani tu nimewaona Machozi yakiwatoka na wakisikitika Kuuwawa Kwake na wengine hivi sasa wanaenda Msibani Nyumbani Kwao.

Kama kawaida hakuna mahala ambapo huwa napaamini kuwa huwa pananijenga na nikiri pamesababisha uwezo wangu wa Kufikiri kuwa mkubwa kama Kukutana na ' Intelligent Members ' wa JamiiForums kwa Michango yao mbalimbali yenye Mantiki na Tija wameweza Kuimarisha sana Ubongo wangu hivyo naamini na hapa pia nitapata Hekima na Busara zao.

Je kati ya Mimi GENTAMYCINE niliyegoma na kuapa kabisa kuwa sitohudhuria Msiba wa huyo Kibaka Mzoefu aliyeuwawa Jioni hii na wale Wenzangu ( wana Jamii ) ambao nao pia ni Wahanga wa Kuibiwa nae wameamua hivyo hivyo wanaenda Msibani Kwao Kiimani na Kihaki kabisa nani ambaye Maamuzi yake yatakuwa na Thawabu au Laana kwa Mwenyezi Mungu?

Nawasilisha.
 
Mpwaa kila binadamu chini ya jua anaumuhimu wake ,ungekwenda tu kwenye sherehe yake ya mwisho na ndio maana hata wanajeshi wakikutana na jeneza lake humpigia saluti ,huna mamlaka ya kumuhukumu hiyo nikazi yake Mungu.
Wanajesh wanampigia salut mwizi?
 
Aliyekufa amekufa tu mzee awe kibaka, mcha mungu, mzinifu wote tunakufa na wewe mkuu genta utakufa sidhani kam utapenda siku umetangulia mje mtu akuandikie uzi hapa kama hivi!

wewe nenda kazike kiroho safi akuna aliye mkamilifu hapa duniani kila mtu anaondoka na yake
 
Mpaka muda huu naona Mzani umeniangukia Mimi na Members wengi wenye Imani Kali wamenishauri niende tu. Sawa nimewasikieni ngoja Mvua hii iishe / isimame kidogo nitaenda japo nikiri tu wazi hapa hapa kuwa naenda kwakuwa tu nyie mmenitisha hapa na maneno ya Kiimani ila Kimoyomoyo sikutaka kabisa kwenda kwani hata Mimi Marehemu Kibaka alinikosakosa katika Uchochoro mmoja hivi Kitaani Mwezi sasa umepita.

Cc: torvic , ZEE LA HEKIMA , STRUGGLE MAN na dagii
 
Ndugu GENTAMYCINE hapo ndio utajua haijarishi mtu alikuwa na ubaya wa namna gani
ipo siku watu watatamani wangeendelea kumuona,
Huwa inashangaza sana kwakweli lakini tuseme tu huo ndio unaoitwa ubinaadamu, Ukiishakuwa na utu ni jambo la halina kizuzi mwili utakubaliana tu na mapokeo ya nje.
Ndio maana unaweza fika mahali mazishi ya mtu usiyemjua na bado ukatokwa na machozi
 
Nahisi 99% ya Members walionijibu hapa wanaweza wakawa ama Maaskofu au Masheikh kwani sijaona hata Mmoja mwenye Roho Ngumu akiniunga mkono Maamuzi yangu ya Kutohudhuria Msiba wa Marehemu Kibaka.
 
  • Kicheko
Reactions: Obe
hoja ya kitoto kweli

Na ukiwa ni ' Mpumbavu ' Mwandamizi kama ulivyo ni lazima tu utaiona ni ya Kitoto. Na kama kumbe ulishajua ni ya Kitoto ulichoifungua na Kuisoma hadi Kuielewa na Kuijibu ni nini? Hoja za Kikubwa kama Pua lako hilo Kubwa hukuziona hapa? Swine!
 
staki ban punguza jeuri na lugha za hovyo!!

much know
 
Nahisi 99% ya Members walionijibu hapa wanaweza wakawa ama Maaskofu au Masheikh kwani sijaona hata Mmoja mwenye Roho Ngumu akiniunga mkono Maamuzi yangu ya Kutohudhuria Msiba wa Marehemu Kibaka.
hovyo kabsa
 
Watu wengi sana wana mapungufu na bado wanazikwa na watu
Kuanzia viongozi waliotawala mpaka vibaka hao lakini wamezikwa na watu na wapo waliogoma kabisa na kutamani hata kuitemea mate maiti kwa madhila waliyoyafanya kwa binadamu wengine
Kama hujisikii kuzika usiende mkuu ni maamuzi yako tu wapo watakaomzika maana haiwezekani wakamtupa aliwe na mamba au chatu
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom