Kuhifadhi pesa nje ya nchi kinyemela ni hatari

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,994
Kuna watanzania wanaodhani kuweka pesa nje ya nchi kisiri siri kuna usalama ni hatari sana.Wazungu ni wajanja mno.Ukienda kuweka wanaweza wakajifanya hawaoni.Unaweza kuziweka kwa kusafirisha kwa njia za panya nk.Zikifika kwao watajifanya hawajali watakufungulia akaunti utaweka na wao watatulia kimya.

Siku ya siku wakitaka kuzitaifisha wataibuka.Watatuma wakaguzi wao kuangalia akaunti zote.Watatuma watu wa mamlaka za kodi za nchini kwao kukuhoji vyanzo vya hizo pesa umezipata wapi? Na kwa kuwa wewe utakuwa uliziingiza kinyemela zitaonekana kama vile uliziingiza ukiwa umezipata ndani ya nchi yao.Kwamba kuna kitu kisichoeleweka ulichokifanya nchini mwao ukapata hiyo pesa.Kwa kuwa utakuwa hukuwa na shughuli za kueleweka ndani ya nchi zao hizo hela zitahesabika kama hela chafu za wizi ambazo umeibia raia wao au za rushwa nk.

Watakachofanya ni kuzitaifisha na wewe ndio unakuwa mwisho wako na tupesa twako ulitoenda kuficha kwa siri nje ya nchi.Wenzetu wakenya kwa kuelewa hilo wengi huziweka nchini kwao na kuwekeza kwenye vitega uchumi nchini kwao zaidi maana wameshabamizwa sana.
 
Ungewaambia wezi wenzako hapo Lumumba kuliko kujaza servers za JF bure. Jaribu kuanza na yule aliyeweka fedha kule kisiwani Jerseys namaanisha yule Wa rada.
 
Ungewaambia wezi wenzako hapo Lumumba kuliko kujaza servers za JF bure. Jaribu kuanza na yule aliyeweka fedha kule kisiwani Jerseys namaanisha yule Wa rada.

Za Mbowe alizotuhumiwa zilizoandikwa kwenye magazeti vipi umezisahau?
 
Za Mbowe alizotuhumiwa zilizoandikwa kwenye magazeti vipi umezisahau?
Kumbe tuhuma!? Mi nilidhani amekiri mwenyewe kama yule Wa rada ambaye ni mbunge wenu mliyemkabidhi jukumu la kuwatungia waTz katiba mpya yeye aliyesema ni vijisenti tu. Halafu ungesema tu kuwa jarida lenyewe ni utumwa hapana ni Uhuru jarida la chama.
 
Back
Top Bottom