Kuhesabu pesa ulizopewa na mpenzi wako mbele yake.

shining

Member
Dec 6, 2013
20
8
Habari zenu wanajamvi,
Naombeni mnijuze kwa mitizamo yenu, kuna tatizo gani mpenzi wako akikupa pesa nawe ukaihesabu hapohapo kujua ni kiasi gani, nimekua nikiona wengi sana sana wadada yaani akipewa tu yeye anaihifadhi halafu anaenda kuhesabia mbele baada ya kuachana na aliyempa. Kwani kuna tafsiri gani hapo kama utaamua kuhesabu misimbazi yako ujue kama imekidhi maombi/makubaliano? Nipeni mitizamo yenu ili nifahamu kama huwa nakosea kufanya mahesabu yangu hapo mbele yake maana kuna ndugu mmoja akiwepo huwa ananikata jicho flan hiv huwa silielewi kabisaa.
 
Smile; Unadhani atakuwekea magazeti au? Huna haya? Sio fresh

Haya kivipi? Si bora uhesabu hapo kama kuna mapungufu uongee kuliko kunung'unika mbele ya safari?
 
Habari zenu wanajamvi,
Naombeni mnijuze kwa mitizamo yenu, kuna tatizo gani mpenzi wako akikupa pesa nawe ukaihesabu hapohapo kujua ni kiasi gani, nimekua nikiona wengi sana sana wadada yaani akipewa tu yeye anaihifadhi halafu anaenda kuhesabia mbele baada ya kuachana na aliyempa. Kwani kuna tafsiri gani hapo kama utaamua kuhesabu misimbazi yako ujue kama imekidhi maombi/makubaliano? Nipeni mitizamo yenu ili nifahamu kama huwa nakosea kufanya mahesabu yangu hapo mbele yake maana kuna ndugu mmoja akiwepo huwa ananikata jicho flan hiv huwa silielewi kabisaa.

ndio maana siku hizi nakugonga bila kukupa hela
 
Kuhesabu mbele yangu ina maana unahisi nimekudhulumu.kama unafanya biashara labda, lakini kama ni hela ya sabuni na pads we unapokea tu na kuweka mfukoni na kufurahi kumoyo.! Unataka kuhesabu kwani ulinikopesha? Unless umeniomba fixed amount of money ndo unahakikisha kama sijazidisha ili unirudishie.
 
Mimi nisingejisikia vizuri mtu wangu akihesabu mbele yangu, kwani ananidai!
 
kuhesabia pesa mbele ya mpenzy wako ni UTOVU WA NIDGAMU:

1. kama aliahidi kukupa kiasi fulani cha pesa sharti atekeleze au kama kimepelea si atakuambia? kuna haja gani ya kuhesabu? hii ni ishara ya kutokuwa na imani na mtu wako--something you don't have to show publicly.

2. kama hajakuahidi kiasi unahesabu mbele yake ili iweje? kwani kuna biashara mlifanya na kuahidiana kugawana faida hadi utake kuhesabu pesa zako (before leaving the counter)?

jiangalie sana wewe mtoto wa kike!
 
Utovu wa nidhamu unakuja vp! Mtu unamuheshimu sana nayeye anajua, yani kitendo cha kuhesabu pesa mbele yake ndo uwe mtovu wa nidhamu? Kwanini ujiskie vibaya? Kwan si nataka tu kujua ni kiasi gani, sababu hasa ya kujiskia vibaya ni ipi?
 
huyo dada nampiga chini baada ya apo!!! ni tabia mbaya sana!!!
 
Hayo mapenzi ya kupeana hela yapo dar es alam tu vijijini hakuna kitu kama hicho.ukimpa hela mtu wa kijijin anakataa.mjini tunapigwa sana.
 
utawajua tu wapenda hela na walio kwenye uhusiano wa kibiashara na hawaaminiani kabisa
watu wa hivi tuwashauri wanunue mashine ya kuhesabia hela wakipewa wanaweka na zinahesabiwa
 
Mara nyingi ukipewa hela kwenye mazingira ambayo inahitajika kuhakiki hapo hapo kama bank ama kwa mtu usiye na uhusiano naye then ni vizuri kuhakiki hapo hapo. Lakini kama ni mtu ambaye mnaaminiana inaleta picha mbaya coz hata kama imekuwa pungufu mbeleni si mnamalizana?
Kama wewe unapewa na mpenzio na unafanya hivyo basi humuamini na mapenzi ya kumvulia mtu usiyemwamini nguo na in return ukapewa hela basi unajua tafsiri yake.....
 
Habari zenu wanajamvi,
Naombeni mnijuze kwa mitizamo yenu, kuna tatizo gani mpenzi wako akikupa pesa nawe ukaihesabu hapohapo kujua ni kiasi gani, nimekua nikiona wengi sana sana wadada yaani akipewa tu yeye anaihifadhi halafu anaenda kuhesabia mbele baada ya kuachana na aliyempa. Kwani kuna tafsiri gani hapo kama utaamua kuhesabu misimbazi yako ujue kama imekidhi maombi/makubaliano? Nipeni mitizamo yenu ili nifahamu kama huwa nakosea kufanya mahesabu yangu hapo mbele yake maana kuna ndugu mmoja akiwepo huwa ananikata jicho flan hiv huwa silielewi kabisaa.

Unless mlikubaliana atakupa kiasi gani, au mnafanya biashara ss ushampa mziko wake anakupa malipo hapo ni vema kuhakikisha kama yuko sahihi! au kumuondoa doubt yy kuwa hajakosea kuhesabu,

lakini hela ya kupewa tu unaihesabu ya nn, kama ikiwa pungufu ya matarajio uombe uongezwe au? au ukunje sura? Kama hauna makubaliano we pokea mpe HUG sema ahsante chapa lapa, hata kama ni buku buku 5! powa tu, si ya bure?
 
Back
Top Bottom