Kuhatarisha usalama wa Taifa? Give me a Break!

Madudu yanayofanyika ambayo mtoa hoja anasema yangeshughulikiwa na Idara hiyo, yanaweza kuwa hayashughulikiwi kwa sababu ushirikishwaji wa wananchi yawezekana ni mdogo sana au haupo kabisa. Wananchi ambao ni pamoja na mtoa hoja wanakaa kimya pengine wakifikiri kwamba Idara na vyombo vingine vya usalama vitafanya kazi kwa kupiga ramli. Haiwezekani.

Nimekuwa nikiwasikia baadhi ya watu wakiisifia Idara hiyo kwa kugundua mipango mingi ambayo kama ingefanikiwa nchi ingekuwa pabaya na pengine ndio maana kwa takribani miongo mitano sasa tangu nchi yetu ipate Uhuru hali imekuwa shwari kiusalama kwa wastani
 
Kama ingekuwa ni ‘madudu' kuyaainishe na ubovu wa Idara hiyo ya Usalama pengine itakuwa haitendewi haki kwa sababu zipo Idara kama hizo duniani ambazo pamoja na mambo makubwa yaliyofanyika katika nchi zao Idara zao hazikufutwa kama CIA ya Marekani, NDC ya Afghanistan, na CAN ya Spain.

Hata hivyo kama kipo kitu kinachoonekana kwamba Idara hiyo imekosea, sio vibaya kuisaidia kwa kutoa maoni hasa kupitia mtandao huu wa jamii forums. Mtandao huu uko wazi ni rahisi kwa Idara hiyo kuchota busara za JamiiForums na kuboresha mapungufu yanayojitokeza katika shughuli zake.

Hata hivyo, mimi bado naamini chombo hicho kina umuhimu wake kwa usalama wa taifa letu.
 
Wana JF naomba kueleweshwa hivi suala la uraia ni la Idara ya uhamiaji au Idara ya Usalama wa Taifa kwani mimi naliona kama sio jukumu la moja kwa moja kwa Idara ya Usalama wa Taifa. Mtoa hoja anailaumu Idara ya Usalama kwa suala la Bashe
 
Madudu mengi na ya hatari yanayotokea katika siasa za nchi yetu yanaashiria kuwa idara yetu ya Usalama wa Taifa imefika mwisho kiutendaji. Ebu ona:-

-Rais akamteua Chenge baada ya kuvunjwa kwa Baraza la mawaziri. Watu wakapiga kelele, yeye akakaidi. Baada ya muda mfupi akalazimika kumwondoa kwa aibu!

-Nape na Malisa wakavutana kuhusu uongozi wa UVCCM; Rais akawatosa wote na kumchukua Masauni. Amegundulika alifoji umri, akaondoka, lakini aibu ikabaki kwa Rais. Hakuna aliyewajibishwa katika idara ya Usalama.

-Sasa tunaambiwa Bashe si raia. Amekuwa katika nafasi nyingi ikiwamo NEC. Chiligati anasema walipitiwa tu. Wamepitiwa mangapi?

La kujiuliza, hivi tuna ile Idara ya Usalama wa Taifa au sasa ni Idara ya Uhasama wa Taifa? Kinachoonekana kujengeka sasa ni kuwa uhasama katika mahusiano ya watawala ni mkubwa sana. Leteni maoni ya nini mwisho wa uhasama huu.

Hii ni idara ya usalama wa taifa si ya NEC...may be kwa Chenge sawa. Idara hii itachemka kama tutampata kiongozi wa serikali ambaye amefoji si vinginevyo. Ni mtazamo wangu tu!
 
Wana JF naomba kueleweshwa hivi suala la uraia ni la Idara ya uhamiaji au Idara ya Usalama wa Taifa kwani mimi naliona kama sio jukumu la moja kwa moja kwa Idara ya Usalama wa Taifa. Mtoa hoja anailaumu Idara ya Usalama kwa suala la Bashe

Majukumu ya Idara ya Usalama wa Taifa yamewekwa wazi kabisa kwenye sehemu ya nne ya Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwa 1996. Katika kifungu cha 14(1) cha sheria hiyo kinasema kuwa:

"It shall be the duty of the Service [idara] to collect, by investigation or otherwise, to the extent that it is strictly necessary, and analyse and retain information and intelligence respecting activities that may on reasonable grounds be suspected of constituting a threat to the security of the United Republic or any part of it.

Maneno muhimu sasa kwenye kifungu hicho "threat to national security". Kama issue haiwezi kutishia usalama wa taifa then idara hiyo haitahusika. Tukija kwenye maswala ya uhamihaji yapo yanayoweza kutishia usalama wa taifa, lakini sio yote. Rejea kifungu hicho hapo juu "to the extent that it is strictly necessary" and "on reasonable grounds".

Mtoa mada amesema kuwa "Madudu mengi na ya hatari yanayotokea katika siasa za nchi yetu yanaashiria kuwa idara yetu ya Usalama wa Taifa imefika mwisho kiutendaji" Swali ni kwamba, je hayo madudu yaliyotokea katika siasa yanahatarisha usalama wa taifa?

Mfano mtoa mada amesema "Nape na Malisa wakavutana kuhusu uongozi wa UVCCM; Rais akawatosa wote na kumchukua Masauni. Amegundulika alifoji umri, akaondoka, lakini aibu ikabaki kwa Rais. Hakuna aliyewajibishwa katika idara ya Usalama." Je, kufoji umri kunahatarisha usalama wa taifa?

Pia mtoa mada anatetea hoja yake kuwa "kabla Rais hajateua mtu kwa nafasi kubwa kama ya Waziri Chenge au kabla hajapendekeza mtu kama Masauni kuingia kwenye Cental Committee, ilibidi Idara ya Usalama impe clearance kuwa watu hawa ni safi." Sasa mwenye mamlaka kuteua mawaziri ni nani hapo? Vipi idara ya usalama ikikataa kutoa clearance, rais atafanyaje? Na anamaanisha nini unaposema clearance?

Pia sikufurahihswa na usemi wa mtoa mada alivyosema "Tumegusa kitumbua! Basi tupe Job Description ya Idara ya usalama wa Taifa." What do you mean by "tumegusa kitumbua?" Kwa sababu sikubaliani na hoja yake ndio ameona aniite kitumbua? The mtoa hoja anasema Kwa kuwa mimi naonekana nipo idara hiyo, niwaelimishe Wana Jamii Forum wajinga wajue ni nini kazi ya idara hiyo ya usalama. kwa kweli sielewi kwa nini mtoa mada anaandika maneno kama hayo. Yaani kuchallenge argument yake, if any, ndio kumaanisha nipo usalama wa taifa?

Mimi nafikiri hata kabla ya kupublish hii mada, mtoa mada angejaribu angalao ku-research kidogo majukumu ya idara ya usalama wa taifa. If s/he really wants to be a GREAT THINKER s/he needs to think and analyse things before s/he writes.
 
Kazi ya mashushushu ni usalama si kuhujumu uchaguzi

RAIA Mwema namba 155 la Oktoba 13-19, 2010 liliandika makala iliyokuwa ikiuliza kama mashushu hutumiwa kuhujumu uchaguzi.
Makala hiyo iliyochapishwa katika safu hii ya Raia Mwema Ughaibuni ya Evarist Chahali anayeishi Uskochi, ilikuwa na kichwa kidogo cha habari "Dk. Slaa aibua madai fikirishi".

Mashushu ambao mwandishi anaulizia kama wanaweza kutumiwa kuhujumu uchaguzi ni maafisa Usalama wa Taifa wa Tanzania na uchaguzi anaozungumzia ni Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, 2010.

Katika makala yake, mwandishi ameanza kwa kujisifu kwamba ana ufahamu wa kutosha juu ya Usalama wa Taifa au intelijensia, ameisomea fani ya Usalama wa Kimataifa na kwamba anaijua vizuri Idara ya Usalama wa Taifa ya Tanzania.

Pamoja na sifa, tambo na majigambo yote haya, mwandishi anasema anachojaribu kuandika hakisemeki au hakizungumziki na anasema kwa kutekeleza kile anachotaka kukifanya lazima tujiulize maswali magumu na pengine ya kuogofya.

Napenda niseme kwamba kuanzia mwanzo kabisa katika kupitia makala yote ya mwandishi huyu hakuna chochote alichoandika ambacho hakizungumziki na hakuna swali lolote gumu wala la kuogofya ambalo amelidhihirisha katika makala yake.

Nilichogundua katika makala yake ni kuwa kama huo si mtindo wake wa kuwavutia wasomaji napenda kuamini kwamba yeye ni mshika bango wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na ameendeleza tu yale yanayofanywa na chama hicho yasiyofurahisha kila mtu, ni mambo yanayorandana na afanyayo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mgombea urais kupitia chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.

Hata hivyo, ameeleza mambo ya msingi sana katika kuthibitisha kwamba amejifunza fani ya usalama wa kimataifa kwa kusema kwamba uimara wa taifa lolote duniani unategemea uimara wa idara yake ya usalama wa taifa na kulegalega kwa mambo katika nchi yoyote duniani kunaashiria upungufu wa idara hiyo.

Lakini katika hali ambayo sikutarajia, mwandishi anakiri kwamba kwa miaka mingi sasa, Idara ya Usalama wa Taifa ya Tanzania ni miongoni mwa idara bora duniani. Hilo pengine lilitokana na maelezo yake kwamba anaifahamu vya kutosha Idara hiyo.

Wapo waandishi wengine ambao wamekuwa wakiandika habari kama hizo, lakini wakiwa na mitazamo inayotofautiana. Jambo ambalo linanishangaza au pengine linanitia shaka katika makala yake ni kama Idara anayoisifu hivyo imekwishakupoteza sifa hizo na kama ni hivyo je, hiyo ndiyo sababu ya yeye kuanza kuwa na shaka kama Idara hiyo sasa inaweza kutumika kuhujumu matokeo ya uchaguzi?

Amesema idara ya usalama wa taifa duniani kote hufanya kazi kwa siri kubwa kabisa na usiri huo ni sehemu ya utekelezaji wa kazi zake. Anasema usiri ni muhimu kabisa na wa lazima katika ukusanyaji wa taarifa nyeti.

Jambo ambalo wasomaji walitakiwa walijue kutoka kwa mwandishi ni ikiwa usiri wa Idara ya Usalama wa Taifa ndio utakaotumika kuhujumu matokeo ya uchaguzi na kama hilo ndio lengo ni kwa nini Idara hiyo ifanye hivyo, kwa kutumiwa na CCM au kwa utashi wake yenyewe?

Mwandishi amezitaja nchi za Uingereza na Marekani kama mifano kwamba mara chache wakuu wa vyombo vya intelijensia huitwa kutoa ufafanuzi kwa mambo yanayohusu usalama wa Taifa wa nchi hizo.

Kwamba aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Central Intelligence Agency (CIA) ya Marekani, George Tennet aliitwa kueleza juu ya ushahidi kwamba Iraki ilikuwa na mipango ya kutengeneza silaha za maangamizi.

Anasema katika nchi hizo mbali na kuondoa katika orodha baadhi ya mambo ambayo ni siri, mabunge yao yana kamati zinazoshughulikia masuala ya usalama na zinawaita viongozi wa idara hizo kutoa ufafanuzi katika masuala yanayohusu intelijensia pale inapokuwa lazima kufanya hivyo.

Suala hili halifanyiki kwa siri anayoizungumzia mwandishi na kama nia yake ingekuwa ni kulifahamu hilo angemuuliza Dk. Slaa ambaye amekuwa mbunge kwa miaka 15 na anafahamu kwamba ipo Kamati ya Bunge ambayo inafanya kazi kama zile zinazofanywa na mabunge ya Uingereza na Marekani.

Amerejea swali lake kama Idara ya Usalama wa Taifa inaweza kutumiwa na CCM kuhujumu uchaguzi na akaunganisha masuala mengine mawili kwamba; hakuna ofisa usalama atakayefurahi na tuhuma za Slaa zikibainika kama ni uongo na Watanzania watakuwa na hofu kama itabainika kwamba tuhuma hizo ni za kweli.

Swali kwamba Idara ya Usalama wa Taifa ilikuwa wapi wakati ukitokea ujambazi wa EPA na je, Idara hiyo ilikuwa ikifanya nini wakati mikataba ya kifisadi ikitokea. Mwandishi anajihami mapema kwa kusema kwamba maswali haya yatazua uhasama kati yake na idara hiyo.

Labda niseme tu kwamba si maofisa wa Idara ya Usalama tu watakaochukia bali Watanzania hawatafurahi kuona tuhuma hizi za Dk. Slaa ambazo ni za uongo zinazidi kuendelezwa na watu wenye hadhi za kisomi kama mwandishi mwenyewe kwa ahadi ambazo nina hakika hazitatimia.

Wananchi wa kawaida ambao wamekwishakuelewa kwamba Chadema ina tabia ya kuzua mambo na ambao wanaamini kwamba nchi hii ina ulinzi wa kutosha, hawawezi kuingiwa na hofu kwa kutegemea tu propaganda za askari wetu kutoka Uskochi.

Ninachotarajia mimi ni kwamba Idara ya Usalama wa Taifa haitamjibu mwandishi. Nililo na uhakika nalo ni kwamba itanyamaza bila kusema chochote kwa kuwa mwandishi mwenyewe amesema kuwa Idara hiyo inafanya kazi zake kwa siri kubwa kabisa.

Ninahisi kwamba mara zote Idara hii inaacha wajinga wajielimishe wenyewe. Swali kwamba Idara ya Usalama wa Taifa ilikuwa wapi wakati ufisadi wa EPA ukitokea sio la msingi bali jambo la muhimu ambalo Mtanzania wa kawaida anaweza kusema ni kwamba suala la EPA limeshughulikiwa sana na Serikali na baadhi ya wahusika wamefikishwa mahakamani.

Naamini kwamba ufisadi si sera ya Serikali wala ya Chama tawala-CCM- na ni vyema ikubalike kwamba, kwa sasa pengine tofauti na ilivyokuwa huko nyuma, ufisadi ni suala la mtizamo na hulka ya mtu kuliko kuonekana kama mtindo wa maisha wa baadhi ya Watanzania.

Serikali ya Tanzania inazingatia utawala wa sheria na tungejali sana suala la mtu kumiliki vitu kama gari, nyumba nzuri, vitu ambavyo wengine hawana, mtu huyu akaonekana kuwa fisadi, Watanzania wengi wangeishia jela.

Amezungumza mengi ikiwa ni pamoja na ikiwa Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye shughuli zake si za siri anaonyesha wazi kuipendelea CCM kwa kuingilia majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, hali ikoje katika Idara ya Usalama wa Taifa.

Nilijaribu kuhoji pale mwanzo kama mwandishi alikuwa anahisi nini juu ya usiri aliousifia sana, usiri wa Idara ya Usalama wa Taifa, kama usiri huo ndio utatumika kuhujumu matokeo ya uchaguzi.

Kinachojidhihirisha hapa ni kwamba mwandishi anataka Watanzania waamini kwamba Idara ya Usalama wa Taifa kwa kutumia kigezo cha usiri, inaingilia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kama alivyofanya Msajili wa Vyama vya siasa kwa nia ya kuhujumu matokeo ya uchaguzi (kama kweli alifanya hivyo).

Inaonekana anaamini kwamba usiri huu ndiyo utakaotumika kukipatia ushindi CCM kwa kuihujumu Chadema.

Lakini kila mtu anajua kwamba kazi ya Idara hiyo kama chombo cha usalama ni kuhakikisha Usalama wa Taifa ambao ni pamoja na uchaguzi kuendeshwa kwa amani, si kuuhujumu.

Inavyoonekana, mwandishi mara zote anaiangalia Idara ya Usalama wa Taifa kama chombo chenye uamuzi wa mwisho kwa kila kitu na anasema kwamba Idara hiyo inamfahamu mmiliki wa Kagoda, ama kwa njia zisizo rasmi au njia rasmi.

Hivi kama kweli kazi za Idara hiyo ni za siri ni vipi itathubutu kutekeleza au hata kama imetekeleza, ieleze wazi kwamba imefanya hivi na hivi kwa watuhumiwa wa aina yoyote, achilia mbali wa Kagoda.

Binafsi nina shaka juu ya uelewa wake wa usalama wa kimataifa na ufahamu wake juu ya Idara hii ambayo anadai ni moja ya idara bora duniani na inayotenda kazi zake kwa usiri.

Ni utaalamu gani anaozungumzia mwandishi unaoweza kutumika kushinikiza Serikali kwa njia zilizo rasmi na zisizo rasmi. Nimejaribu kudadisi kwa wajuzi wa masuala ya Usalama wa Taifa, nikaambiwa kwamba kazi ya idara hiyo duniani kote ni kutoa ushauri na si kushinikiza kama mwandishi anavyotaka tuamini.

Nilitaka kujua kama ameifahamu Idara hiyo vipi kwa kuhadithiwa au pengine alishawahi kuwa mtumishi kwenye chombo hicho nyeti? Kwa yote mawili nilipata jibu moja kwamba hata kama alihadithiwa au alifanya kwenye Idara hiyo, kulingana na kanuni za usiri ambao ameukiri yeye mwenyewe, hawezi kusimama hadharani na kusema kwamba amekuwa mtumishi wa chombo hicho.

Anasema pia kwamba idara ya usalama wa taifa kote duniani ni kama nusu jeshi (paramilitary) na viongozi wake wanaogopwa kupindukia na uamuzi wao hauhojiwi.

Katika udadisi wangu, niliambiwa mambo mawili kwamba kuogopwa kupindukia kunatokana na usiri wa idara zenyewe na nikaamini kwamba usichokijua ni sawa na usiku wa giza.

Kwamba wanaoiogopa idara ni wasioifahamu na anachotaka kusema mwandishi ni kwamba wasomaji waendelee kuiogopa Idara yao ya Usalama wa Taifa.

Nafikiri hilo si la lazima kwa sababu wananchi wana haki ya kukifahamu chombo ambacho kwanza kinahakikisha kuwa Taifa ni salama na kinatumia kodi za wananchi katika utendaji wake wa kazi wa kila siku. Hakuna sababu ya kukiogopa, ni chombo chao na ambacho kimewekwa kisheria.

Mwandishi ametaka pia wasomaji wake wapime madai fikirishi ya Dk. Slaa ambayo yametolewa kama tuhuma ikiwa hadithi au ni kitu kinachowezekana. Ukiyavulia nguo maji sharti uyakoge na kwa hilo mwandishi haamini kwamba anachosema Dk. Slaa ni hadithi tu, anaamini kwamba ni ukweli ingawa hoja yake imejengwa katika nadharia tu.

Wana JF,

Katika msukosuko tuliotoka nao huko nyuma hata kabla ya Uchaguzi ambako kulikuwa na shutuma nyingi sana za viongozi wa ngazi ya juu kukutwa na kashfa ya UFISADI, (EPA, KAGODA, MEREMETA, RICHMOND etc). Sijaona Usalama wa Taifa na TAKUKURU wakionyesha Positive reaction toward hawa mafisadi walio tajwa kwenye hizo scandal sasa sielewi TAKUKURU na USALAMA wa TAIFA wao kazi zao ni zipi kwa TAIFA hili, au maslahi ya watu baadhi? SIWAELEWI KABISA HAWA WATU katika hizo Sector muhimu sana nchini kwetu.

Walichoni shangaza kabisa hawa (USALAMA WA TAIFA NA TAKUKURU) ni kuwa muda mwingi wakati wa Uchaguzi wao walijikita humo ndani as if Uchaguzi ni kazi yaooo wao wanaacha mambo ya maana ya kuhakikisha hakuna kiongozi anae hujumu uchumi wa watanzania wao ndio wakwanza kuwa kimya mpaka raia aanze kusema sana na kupiga kelele ndio ati twashughurikia jambo hilo mbona hamkujitokeza kuwa wa kwanza na kusema hayo in Public???

Juzi hapa Dr. Slaa kawashutumu kuwa wao walichangia kwa asilimia kubwa kuchakachua matokeo ya uchaguzi uliopita (Usalama wa Taifa kwanini hawakumpeleka Slaa Mahakamani), na wao kwa akili zao mbovu ati wakajibu tuhuma hizo.

Mbona wakati wa RICHMOND, EPA hawakusema matokeo ya uchunguzi wao kuhusu mafisadi walio husika iweje majuzi walijitokeza hadharani na kuongea na tena kwenye siasa yaani wanaacha mambo mengine pia ya msingi wana jikita siasa.

Ivi Usalama wa Taifa hawa wanawafanyaia kazi watanzania kweli au yawafanyia kazi kundi la watu fulani tuu kwa manufaa yao?, Hao hao ndio ati hutumiwa kutupa ma profile ya wagombea ni yupi ni safi na yupi si safi. hawaoni aibu kabisaa?? Chenge ana tuhuma za RADA walikuwa wapi kumyamazisha Chenge hata kugombea Ubunge hata kama haki yake ndio lakini ki maadili ya uongozi ni kuwa unakaa kando mpaka matuhuma hayo yatokomee ndio urudi kwenye ulingo wa siasa.

Kweli nina mashaka MAKUBWA SANA USALAMA WA TAIFA na TAKUKURU KIUTENDAJI NCHINI TANZANIA
 
Nafikiri bado hatujaelewa hivi vyombo viwili vinaripoti kwa nani, hivyi vyombo kwa uelewa wangu vinaripoti moja kwa moja kwa kiranja mkuu. kwa hiyo lazima watekeleze yale wanayoagizwa kufanya. kumbuka watu hawa wanafanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu, kuliko hata wewe na mkeo au mwanao. hivyo kama kiranja mkuu anataka upepo upeperushe kura, hawa jamaa watafanya ingawa inakuwa inawauma.

Kumbuka pia kuwa, katika kazi moja hutumwa zaidi ya mmoja. Kwa hiyo lazima utekeleze ulilotumwa kwani adhabu za hao jamaa kwa kutokutii ni kubwa mno. Hata kama ungekuwa wewe nafikiri ungefanya kama ulivyotumwa kufanya ila ungetoa tu taarifa kama wanavyofanya kwa sasa.

Nasisitiza kuwa haya ni mawazo yangu.
 
Tatizo linaloisumbua Tanzania ni uteuzi wa viongozi katika idara zake! Hawachagui mtu kutokana na utashi wake wa kiutendaji, ila mtu huteuliwa ili alindea maslahi ya yule aliyemteua!!

Kwa taasisi nyeti kama TAKUKURU kujiingiza kwenye siasa na kuanza kumpigia debe mtu mwenye kashfa tena kubwa ni aibu kubwa sana, kwa serikali na aliyemteua!!
 
Wadau naomba msaada, mi kila siku ninavyosoma vijihabari nazidi kuchanganyikiwa...eti kazi ya UWT ni nini haswa?

Mi nilikuwa nadhani kuwa kazi yao sio Kulinda.....ulinzi wa ndani ya nchi ni kazi ya Polisi, na ulinzi wa nje (mipaka) ni kazi ya Jeshi (TPDF).

Mi nilikuwa nadhani kazi yao ni kufanya utafiti na kushauri tu!....sio kulinda, kukamata, au kumuhukumu yeyote.

Na je? kuna kamati ya usalama ya bunge ambayo inawahoji hawa ndugu zetu wa Usalama wa Taifa?

Pia, kuna rafiki yangu mmoja anataka kufanya kazi Usalama wa Taifa, kuna jinsi ya ku apply? (wapi, lini, kivipi, etc etc)......au ndio "you don't find us, we'll find you?"

Naomba kuwasilisha Hoja
 
Kwa sasa naona kazi zao zimeongezeka tofauiti na enzi za mwalimu.

Watu mtaani wanajisifu eti mimi usalama wa taifa ndo tabu ya kuajili makanjanja zamani ilikuwa issue kujua
 
Soma sana magazeti kama Tanzania Daima, Raia Mwema, Mwanahalisi na Sani utakuta matangazo ya nafasi zao za kazi.
 
Nikwambie Best. Usipoteze muda wako fanya mambo ya maendeleo. Ila kama una hamu zaid ya kujua ni kazi nzuri sana ya kizalendo na inayoheshimika kila nchi kama idara ya ujasusi na ya siri sehemu nyingi na hufanya kazi kwa maslahi ya wananchi na kulinda viongozi wake na kwa hapa Tanzania inawajibika kuwalinda Top Five, yaani Rais wa JMT. Rais wa Zanzibar, Makamu wa Rais , Waziri Kiongozi wa Zanzibar na Waziri Mkuu. Na pia wanahusika na kufanya mauji ya mtu au kiongozi yoyote anayeonekana kuwa tishio la serikali hasa iliyoko madarakani kwa mfano kama alivyofanyiwa aliyekua mkurugenzi wa idara hiyo Kombe na pia Kolimba Prof. Mwaikusa na wengine kibao.

Kwa kifupi wamegawanyika katika maeneo na idara mbalimbali kama vile kwenye taasisi za dini, mashuleni, vyuoni,sekta binafsi, makazini nk. na wengine kuchunguza uozo wa viongozi kuanzia kijiji, kata mpaka Taifa.

Tukija kwa sasa hapa kwetu kwa nyakati hizi hiyo siyo idara ya kujivunia tena imejaa dhuluma na vitisho, majungu, kujuana na wengi walioko huko ni watoto wa wakubwa fulani aidha jeshini, polisi, au kwenye idara yenyewe hiyo na hapo ndipo panapopoteza utamu na ladha halisi ya TISS.

Sikumbuki au kuwahi kuona kazi hii inaombwa mahali popote zaidi ya wao kuangalia uwezo wako binafsi na uzalendo wa nchi yako watakufuata wenyewe na kukupa baadhi ya kazi za majaribio na kukupa maelekezo machache na namna ya kutunza siri

NB: Nimetumika na idara hii kwa takribani miaka saba kama UC. Kwenye maeneo mbalimbali kama makazini mitaani, sehemu za ibada tena bila malipo ya maana zaid ya kupewa eti posho ambayo unaweza kupewa mkononi tu bila kusaini popote na na usihoji maana utawadhi wakubwa wako na jina lako likawa la chaki miaka yote bila kupata usajili unaoeleweka na utaishia kuonewa huruma na wenzako watasema mbona fulani amepata usajili na hana lolote na huyu mchapa kazi ameachwa kifupi nina maumivu yasiyo na idadi ya vitu nisivyopenda.

Kwa mfano Tanzania hakuna kazi nyingi lakini ili uonekane unafanya kazi inabidi upeleke taarifa (repot) hata kama ni ya uongo ambayo inaandikwa kufuata mtiririko wa (W5) Yaani.
When
Where
What
Who
Why
Kitu ambapo kama ukizingatia na kufuatilia vizuri mfumo huu hauwezi kuandika report ya majungu kitu ambacho hawakipendi wanataka uandike taarifa ya majungu na kumchafua mtu hasa yule ambaye kamati ya ulinzi na usalama inataka kumtoa kafara kama vile kumhamisha mtu fulani kutoka sehemu moja kwenda nyingine mfano ma RPC,RCO,RC.DC,DED,OCD na wengine kibao kama taarifa yako itakua safi sana imefuata taratibu zote utasifiwa na kupongezwa na wenye uzalendo wachache na lakini yatakupata ya yaliyompata Sitta.

Kwa kifupi niko kwenye hii idara nateseka na majungu, urasimu,dharau,bifu zisizo na maana yaani natamani kama utawala ubadilike labda itatuona wanyonge wa chini tutakalitumikia Taifa hili kwa uadilifu na haki sawa kwa kila.

Thnx. JF. Hatutambuani kwa majina halisi ingekuwa kazi kweli yangenikuta yaliyomkuta Kombe.
 
Kwa sasa naona kazi zao zimeongezeka tofauiti na enzi za mwalimu.
Watu mtaani wanajisifu eti mimi usalama wa taifa ndo tabu ya kuajili makanjanja zamani ilikuwa issue kujua

Njowepo, asante kwa mchango wako.....ila Usalama wa Taifa kusitambulisha mi sioni kama ni issue. Zamani nilikuwa nadhani hawa jamaa hawatakiwi kujulikana....lakini kuna mambo yanasikia mtaani ambayo haya "make" sense....kwa mfano:

1. Wanatembelea magari yasiyo na road licence wala insurance (kioo cha mbele hakina sticker): sasa kama hii ni kweli, basi kuona mtu/watu wapo kwenye magari ya aina hiyo, then ni obviously usalama wa taifa na kila mwenye macho atayaona hayo magari....na siku hizi yamekuwa mengi kweli sijui kwa nini

2. Nasikia wanakaa pale makumbusho. Sasa kama hii ni kweli, basi kuwajua pia ni rahisi kwani kila baada ya dakika kadhaa kuna gari/watu wanao ingia na kutoka pale...kwa hiyo ukikaa maeneo yale nusu saa tu, utapata list kubwa ya hao watu......obviously wanajulikana

3. nasikia wana vitambulisho vyekundu.....kwa hiyo ukikutana na jamaa ukamuhisi ni usalama wa taifa we msearch tu, ukikuta kitambulisho chekundu ujue ndiye

Hizi na story nyingine nyingi tu nimezisikia mtaani kuhusu hawa jamaa.......sasa kama kuwatambua ni rahisi hivyo, Usiri uko wapi?

Bado naomba wadau na Usalama wa Taifa waliopo humu ndani mnisaidie mimi na watanzania wengine kuelewe......PIA NIPO SERIOUS RAFIKI YANGU ANATAKA KUFANYA KAZI HUKO, kwa hiyo naomba Msaada wadau?.....kuna jamaa mmoja ameniambie kuwa kuapply aende pale St. Peters kwenye ule mjengo mpya.....na mwingine kaniambia ni Posta J-Mall. Sasa sijui ni kweli au vipi?......au aende makumbusho?.....

Pia Hivi mtu yeyote anaruhusiwa kuingia pale makumbusho kwa kisingizio "kakosea njia?" maana hakuna kibao kinachoonyesha usiiingie hapa.....kuna kibao kinachosema usishushe au kupandisha abiria....lakini sio usiingie huku.

Naomba kuendeleza Hoja
 
Asante Derimto...umepost na "mobile" hakuna button ya kukushukuru "thanks".....so nitasema tu asante.....

Pole sana kwa matatizo unayoyapa huko.....kwani huwezi kuacha kazi?.....hapo kwenye UC umenipoteza kidogo...unamaanisha Under Cover au?.......maana kuna kitu kingine kinaitwa NOC (Non-Official Cover).....sijui lakini.

Naendelea kuwasikiliza wadau....
 
......PIA NIPO SERIOUS RAFIKI YANGU ANATAKA KUFANYA KAZI HUKO, kwa hiyo naomba Msaada wadau?.....

mwambie huyo rafikiyo kazi za kufanya ni nyingi sana. I have many friends in that department wanalia njaa mno na wengine mnawaona kila siku wanatembea na wakubwa na wanasimama nyuma ya waungwana wanapohutubu. secrecy doesn't mean good life unless unataka waranty to ya kutongozea, maana machangudoa ukiwaambia mimi ni usalama wa taifa wanakuvulia nguo haraka.

advise your friend to seek a real career, si hiyo. Akiingia huko katika bajeti yako itakulazimu umwingize naye, maana maisha yatampiga kinoma.
 
Njowepo, asante kwa mchango wako.....ila Usalama wa Taifa kusitambulisha mi sioni kama ni issue. Zamani nilikuwa nadhani hawa jamaa hawatakiwi kujulikana....lakini kuna mambo yanasikia mtaani ambayo haya "make" sense....kwa mfano:

1. Wanatembelea magari yasiyo na road licence wala insurance (kioo cha mbele hakina sticker): sasa kama hii ni kweli, basi kuona mtu/watu wapo kwenye magari ya aina hiyo, then ni obviously usalama wa taifa na kila mwenye macho atayaona hayo magari....na siku hizi yamekuwa mengi kweli sijui kwa nini

2. Nasikia wanakaa pale makumbusho. Sasa kama hii ni kweli, basi kuwajua pia ni rahisi kwani kila baada ya dakika kadhaa kuna gari/watu wanao ingia na kutoka pale...kwa hiyo ukikaa maeneo yale nusu saa tu, utapata list kubwa ya hao watu......obviously wanajulikana

3. nasikia wana vitambulisho vyekundu.....kwa hiyo ukikutana na jamaa ukamuhisi ni usalama wa taifa we msearch tu, ukikuta kitambulisho chekundu ujue ndiye

Hizi na story nyingine nyingi tu nimezisikia mtaani kuhusu hawa jamaa.......sasa kama kuwatambua ni rahisi hivyo, Usiri uko wapi?

Bado naomba wadau na Usalama wa Taifa waliopo humu ndani mnisaidie mimi na watanzania wengine kuelewe......PIA NIPO SERIOUS RAFIKI YANGU ANATAKA KUFANYA KAZI HUKO, kwa hiyo naomba Msaada wadau?.....kuna jamaa mmoja ameniambie kuwa kuapply aende pale St. Peters kwenye ule mjengo mpya.....na mwingine kaniambia ni Posta J-Mall. Sasa sijui ni kweli au vipi?......au aende makumbusho?.....

Pia Hivi mtu yeyote anaruhusiwa kuingia pale makumbusho kwa kisingizio "kakosea njia?" maana hakuna kibao kinachoonyesha usiiingie hapa.....kuna kibao kinachosema usishushe au kupandisha abiria....lakini sio usiingie huku.

Naomba kuendeleza Hoja

Kuhusu magari ni kweli ila siyo yote yote mengine machache yanakuwa nayo ingawa siku hizi na wahuni wachache wameanza kuiga style hiyo ila kwa sehemu baadhi ya traffic wamestukia maana zile gari mara nyingi hutoka kwa series na kwa aina kwa mfano zilikuwepo toyota land cruiser na baadaye pajero ambazo ni nyingi sana kwenye idara hiyo kwa sasa hasa ngazi za wilaya kuliko magari yoyote halafu mashangingi Gx. Na sasa kuna mengine mapya
Pale Makumbusho ni sawa. Ila siyo kwamba wako kisiri kihivyo unavyodhani kuna wengine hawajulikani kulingana na location yake ya kazi na hana sababu ya kwenda kwenye ofisi zao kila mara asije akajulikana na kuharibu mambo

Siyo wote wenye vitambulisho ila fahamu wako wengi kila mahali na wanafamika official katika ofisi zao kama Agents kwa namba na password zao

Vitambulisho ni kweli vyekundu kama vina nembo yao vimeandikwa kwa chuma na siyo kama vile vya PCCB vyekundu na nembo ya Taifa ilogongwa kama kwenye passport zetu.

Ofisi huwa hazina kibao ila za makao makuu na za Mikoa huwa siku hizi zinakuwa na bendera na aina ya minara fulani tofauti na minara ya mawasiliano ya kawaida tuliyoizoea za wilaya huwezi kuzijua maana ziko kama nyumba za watu zaidi sana utaona hayo mgari yao na mara chache magari ya polisi huwatembelea kama vile Maofisa waandamizi na wakurugenzi

Umetosheka?
 
Asante Derimto...umepost na "mobile" hakuna button ya kukushukuru "thanks".....so nitasema tu asante.....

Pole sana kwa matatizo unayoyapa huko.....kwani huwezi kuacha kazi?.....hapo kwenye UC umenipoteza kidogo...unamaanisha Under Cover au?.......maana kuna kitu kingine kinaitwa NOC (Non-Official Cover).....sijui lakini.

Naendelea kuwasikiliza wadau....

Thnx. And You are Welcome all the time. Hapo juu umepatia vyote wala hujaenda mbali sana.

Kumbuka kuwa suala la kuilitumikia Taifa lako kuna changamto mbalimbali na mbaya na nzuri na siyo kwamba wote walioko huko ni watu wazembe kama inavyofikirika na wengi kwamba idara hiyo imeachia meremeta ,EPA,IPTL, na mengine kibao bila kuyafanyia kazi HAPANA KUNA WATU MAJEMBE YA KAZI WAMEKUNYWA TANZANIA NA WAZALENDO NA WAMESHIKA SEHEMU NYETI HAWAWEZI KUUMIZWA NA KUKANDAMIZWA KAMA SISI WADOGO na hao hawaogopi kumkera fulani taarifa itapelekwa na itamfikia mhusika na asipoifanyia kazi kuna njia nyinge wanayotumia wasomi na wazalendo kama vile kuwapa habari pamoja na ushahidi watu kama kina Kubenea na wakina Dk. Slaa

Kumalizia nikupe mfano mmoja wakati fulani nilipata taarifa iliyonisumbua sana na muhusika alikuwa ni Lowassa ambaye kwa wakati huo alikua anang'ara sana na kuonekana ni mchapa kazi na mwadilifu sana nikashindwa kuandika report yake kwa kuogopa kuwakwaza wakuu maana huyu jamaa anajua kupenya kila mahali mpaka kwenye hizi idara kama alivyofanya kule Arusha alihakikisha kuwa amewaweka mpaka PCCB mikononi mwake na atakayeleta mdomo yatamkuta kama DED. Raphael Mbunda na RC. D.Njolay wa Rukwa hivyo nikaenda kuumuliza mmoja wa Senior ninao wafahamu yeye alijibu kuwa kila jambo lina mwisho kaandike report nami nikajipanga nikafanya alivyonishauri tena kwa woga sana lakini huwezi kuamini haikupita miezi sita kila kitu kilitoka tena mengine kuanzia ofisini kwa mzee mwenyewe Ikulu na akaachia ngazi

NB: Kila raia mwema hutunza hadhi na uhuru wa nchi yake bila kujali anakutana na vipingamizi vingapi au analipwa nini uzalendo ni kitu muhimu sana kwa mtu yeyote anayejua thamani ya nchi yake na watu wake
 
Back
Top Bottom