FIKRA MBADALA
Senior Member
- Jun 30, 2008
- 167
- 16
Madudu yanayofanyika ambayo mtoa hoja anasema yangeshughulikiwa na Idara hiyo, yanaweza kuwa hayashughulikiwi kwa sababu ushirikishwaji wa wananchi yawezekana ni mdogo sana au haupo kabisa. Wananchi ambao ni pamoja na mtoa hoja wanakaa kimya pengine wakifikiri kwamba Idara na vyombo vingine vya usalama vitafanya kazi kwa kupiga ramli. Haiwezekani.
Nimekuwa nikiwasikia baadhi ya watu wakiisifia Idara hiyo kwa kugundua mipango mingi ambayo kama ingefanikiwa nchi ingekuwa pabaya na pengine ndio maana kwa takribani miongo mitano sasa tangu nchi yetu ipate Uhuru hali imekuwa shwari kiusalama kwa wastani