Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,903
- 1,053
Jamani Hivi kuchana vipeperushi vya mgombea mwenzako si ni kitendo cha uchokozi na uvunjifu wa sheria?
Kama ilivyokutwa mjini Bukoba mgombea wa chama cha mapinduzi amekuwa akichana vipeperushi vya wagombea wenzake (CUF na Chadema) na kuweka juu ya vipeperushi hivyo picha zake.
Huyu ni waziri mdogo wa mambo ya ndani na anafanya hivi akijua kuwa ni kuvunja sheria. Je aweza kuwa anafanya hivi kwa kutumia madaraka aliyonayo sasa?
Je wengine nao wakifanya anachofanya yeye nini itakuwa matokeo?
Tume ya uchaguzi kwa jambo hili mwasemaje? Je ni haki? Jamani wanaojua sheria za uchaguzi tupeni shule kabla jamaa hajaanza kushughulikiwa.