Kuharibika barabara: Wakazi wa Ubungo wajuta kuichagua CHADEMA wadai imekuwa " kama" walitenda dhambi!

Hivi vyama siku hizi wana fungi la kutengeneza barabara au mtoa post unajifanya hamnazo. Hukuwahi kusikia ccm wakijinasibu kuwa pale ambapo wamechagua upinzani hawapeleki maendeleo kuwakomoa wananchi? Post zingine hazina mashiko tekelezeni tu Sera ya ubaguzi watakuja wazalendo watatoa fursa za maendeleo kwa wote ili mpate kujifinza
 
Wakazi wa maeneo ya Goba na Tegeta A wilayani ubungo wamelazimika kuchanga sh 5000 kila mmoja ili kukarabati barabara iliyoharibiwa na mvua na madaraja yaliyovunjika.

Wakazi hao wamedai wabunge wao na madiwani wao hawapatikani hali iliyopelekea kuwaomba viongozi wa CCM wawasaidie kufikisha kero yao serikalini.
Hata hivyo baada ya watendaji wa Tarura kuletwa eneo la tukio walidai ukarabati utafanywa mwaka ujao wa fedha.

Wakazi hao wa ubungo wamedai kuwa kuichagua Chadema kuongoza wilaya yao imekuwa kama dhambi kwani maeneo mengine yote ya jiji la Dsm barabara zinakarabatiwa isipokuwa ubungo pekee.

Wananchi hao wamemtaka meya wa ubungo ajipime kama badu anatosha kuwaongoza kwani hawako tayari kuendelea kuchanga hela za ujenzi wa barabara .

Source Channel ten

Maendeleo hayana vyama!
Kujenga barabara na madaraja siyo kazi ya chadema. Kujenga vyote hivyo ni kazi ya serikali inayopokea kodi kutoka kwa wananchi. Chadema hawakusanyi kodi. Na ktk kujenga miundo mbinu siyo kazi ya chadema, Act au mwanaccm ni kazi ya serikali. Atakayekuwa anailaumu chadema ni yule ambaye hajui kazi ya serikali yake ni nini. Hizo barabara hawapiti wananxgi au wanachama wa chadema au ACT peke yao ni barabara za watanzania. Tusipobadilika tutaendelea kuendekeza uvyama badala ya kuiwajibisha serikali. Na ktk kuiwajibisha serikali ni kwenye sanduku ya kura. Ni bora ulale njaa, uku ukijua haki yako kuliko kushiba kwa cku moja then utalala njaa kwa miaka mitano
 
Hivi vyama siku hizi wana fungi la kutengeneza barabara au mtoa post unajifanya hamnazo. Hukuwahi kusikia ccm wakijinasibu kuwa pale ambapo wamechagua upinzani hawapeleki maendeleo kuwakomoa wananchi? Post zingine hazina mashiko tekelezeni tu Sera ya ubaguzi watakuja wazalendo watatoa fursa za maendeleo kwa wote ili mpate kujifinza
Maendeleo hayana vyama!
 
Upuuzi mtupu ,, Hivi tarura wametumwa na CHADEMA kuwaahidi wananchi wateseke mpaka mwakani!??? ,,, sisi wananchi wa Ubungo tunajuwa tatizo ni ccm kwani ndiyo wanao control tarura na Serikali ya ccm imechukuwa vyanzo vyote vya halimashauri ili madiwani na wabunge washindwe kujenga barabara zao.
Acha kulialia ndugu.
 
Wakazi wa maeneo ya Goba na Tegeta A wilayani ubungo wamelazimika kuchanga sh 5000 kila mmoja ili kukarabati barabara iliyoharibiwa na mvua na madaraja yaliyovunjika.

Wakazi hao wamedai wabunge wao na madiwani wao hawapatikani hali iliyopelekea kuwaomba viongozi wa CCM wawasaidie kufikisha kero yao serikalini.
Hata hivyo baada ya watendaji wa Tarura kuletwa eneo la tukio walidai ukarabati utafanywa mwaka ujao wa fedha.

Wakazi hao wa ubungo wamedai kuwa kuichagua Chadema kuongoza wilaya yao imekuwa kama dhambi kwani maeneo mengine yote ya jiji la Dsm barabara zinakarabatiwa isipokuwa ubungo pekee.

Wananchi hao wamemtaka meya wa ubungo ajipime kama badu anatosha kuwaongoza kwani hawako tayari kuendelea kuchanga hela za ujenzi wa barabara .

Source Channel ten

Maendeleo hayana vyama!
Kwani ni kazi ya chadema kujenga/kutengeneza barabara? Au zinapaswa kujengwa kwa kodi ya wananchi kupitia halmashauri husika?
 
Back
Top Bottom