Kuhamishwa kwa OCD wa Wilaya ya Hai: Je, matukio yatakuwa yameisha au bado kuna mtu mwingine wa kuhamishwa?

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
373
660
OCD wa Wilaya ya Hai alihamishiwa Kilosa mwezi wa 12, huyu alikuwa sehemu ya Wilaya ya Hai kutokuwa tulivu kisiasa wakishirikiana na DC sasa amehamishwa ila pamoja na kupewa barua ya uhamishwa alikuwa bado ana panchi ili asihame tukahisi kuna maslahi mapana sana ila hatimaye amehama.

Je, utulivu utaendelea na matukio yatakwisha? Au kuna mtu lazima ahamishwe pia ndio pawepo na utulivu katika wilaya hiyo.
 
Kazi gani special ambayo amefanya na wengine walishindwa?
anaondolewa raisi madarakani sembuse OCD!!!!
 
Huyo OCD ndio yule alimwambia Mbowe hatashinda ubunge na kwa kushirikiana na Sabaya wakahakikisha Mbowe hashindi kwa kumtangaza mgombea wa chama chao mshindi usiku wa manane.

Askari wanatumiwa sana na CCM nao wao bila aibu wanaona raha kutumika.
 
OCD wa Wilaya ya Hai alihamishiwa Kilosa mwezi wa 12, huyu alikuwa sehem ya Wilaya ya Hai kutokuwa tulivu kisiasa wakishirikiana na DC sasa amehamishwa ila pamoja na kupewa barua ya uhamishwa alikuwa bado ana panchi ili asihame tukahisi kuna maslahi mapana sana ila hatimaye amehama, je utulivu utaendelea na matukio yatakwisha? au kuna mtu lazima ahamishwe pia ndio pawepo na utulivu katika wilaya hiyo.
Kazi yake kubwa Ilikuwa dhidi ya Mbowe
 
Huyo OCD ndio yule alimwambia Mbowe hatashinda ubunge na kwa kushirikiana na Sabaya wakahakikisha Mbowe hashindi kwa kumtangaza mgombea wa chama chao mshindi usiku wa manane...
Bila kuhamishwa DC Sabaya, bado watakuwa kama wanatwanga maji kwenye kinu.
 
OCD wa Wilaya ya Hai alihamishiwa Kilosa mwezi wa 12, huyu alikuwa sehem ya Wilaya ya Hai kutokuwa tulivu kisiasa wakishirikiana na DC sasa amehamishwa ila pamoja na kupewa barua ya uhamishwa alikuwa bado ana panchi ili asihame tukahisi kuna maslahi mapana sana ila hatimaye amehama...
Anakwenda uswahilini na waswahili wa Kilosa hawana time na mtu.

Ajiandae kuingia katika kutatua kero ya Wafugaji (matajiri) na wakulima (maskini).
 
Utulivu kivipi kwani Kuna vurugu au Vita baridi au Vita vya chinini chini? Ila kuamishwa Kuna mambo mawili umefanya kazi vizuri sasa unapelekwa mahali ukafanye vizuri zaidi au umeboronga unaamishwa ukaanze upya usijeukaboronga zaidi Ila kauli sahivi si nasikia ukiaribu apo unaharibikiwa apo apo
 
Back
Top Bottom