Kuhamisha Wamachinga kwa kuvunja miundombinu yao na kupora mali zao ni uhalifu kwa DSM na Mwanza

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
3,036
3,479
Ni takribani wiki mbili sasa wafanyabiashara ndogo-ndogo (wajasiriamali au wamachinga) waliagizwa na serikali za mikoa mbalimbali kuhama kutoka katikati ya miji mikubwa na ama kuelekezwa wapi waende au bila kupewa eneo mbadala na rafiki kwa biashara.

Wamachinga walitoa mawazo yao ili kufanikisha utekelezaji na mipango hiyo ya serikali kuwa na mafanikio ni pamoja na haja ya wao kushirikishwa ipasavyo kwa mjibu wa sheria.

Hata hivyo mawazo na mapendekezo yao yalipuuzwa na kuhesabika sio ya msingi na hayana nafasi kukubaliwa kinyume na jinsi serikali ilivyopanga kufanya.

Ikumbukwe kuwa kupanga miji kuwa safi kuweka taratibu za kufanikisha hilo haziwezi kuwa na tija kama tabia za uchafuzi wa mazingira hazijadhibitiwa.

Mji wa Mzizima (Dar es Salaam) ulianzishwa mwaka 1866 na sultani wa Zanzibar

Viongozi wa mikoa ya Dar Es Salaam na Mwanza mmekosea njia ya isiyo ya kistaarabu kuwahamisha wamachinga kwa kuvunja sehemu zao za kazi kisha mali kuporwa na watu mliowatuma kutekeleza uharibifu huo.

Vijana wapoteza mali zao kwa hatua zinazovunja haki za binadamu na hazikubaliki popote. Machozi yao yatawatesa maisha yenu yote
 
Mji wa Mwanza ulianzishwa mwaka 1892 na wajerumani

Viongozi wa mikoa ya Dar Es Salaam na Mwanza mmekosea njia ya isiyo ya kistaarabu kuwahamisha wamachinga kwa kuvunja sehemu zao za kazi kisha mali kuporwa na watu mliowatuma kutekeleza uharibifu huo.

Vijana wapoteza mali zao kwa hatua zinazovunja haki za binadamu na hazikubaliki popote. Machozi yao yatawatesa maisha yenu yote
 
Mi naona wamachinga taratiibu wanarudi kwenye maeneo. Kimsingi njaa ikiuma kila mtu hutoka mafichoni. Bora jela kuliko njaa.
 
Sioni kosa la serikali kwenye kuondoa wamachinga. Iwe ni kwa nguvu au kwa upole.

Swali ambalo mmachinga anapaswa kujiuliza je sehemu ninayo fanya biashara ni halali? Umeambiwa ondoka unabisha serikali ikusaidie nin sasa?

Hivi kama watz wote wakiwa machinga nchi itasonga kweli? Umizeni kichwa cha kufanya na sio kudeka kama yatima.
 
Kuna mtu humu aliwahi kusema umachinga ni lawlessness, hakukosea kabisa.

Ni ishara mbaya sana kwa uchumi ukiona fremu zimefungwa/ hazijapangishwa halafu mbele kuna mmachinga kajenga kibanda.

Mmachinga hana faida kwa taifa, kama hawawezi kupangisha fremu na kulipa kodi watafutiwe mashamba huko vijijini wakalime.

Tusiwe na huruma kwenye haya maswala, sheria lazima zifuatwe na maslahi mapana ya taifa kiuchumi yazingatiwe.
 
Fuatilia mambo vizuri walipewa muda na bado ulivyoisha wakaongezewa waliokubali wengine walipelekwa mawasiliano wengine kuna mitaa bado wameachiwa kariakoo sio kila kitu ni kupinga na kuweka hisia zako binafsi.
 
Shida ya watanzania wengi sisi hatupendi kufata yale tunayoambiwa, tunasubr mpk mwisho wa siku ndio tunaanza kuchukua hatua.

Endapo wangehama tangu siku walizopewa taarifa sidhani kam ahaya yangetokea kabisa. Kwa yanayoendelea sasa asilimia kubwa ni wamejitakia wenyewe kwani wangeenda kweny maeneo husika tangu hapo awali haya yote yasingetokea.
 
Kuna mtu humu aliwahi kusema umachinga ni lawlessness, hakukosea kabisa.

Ni ishara mbaya sana kwa uchumi ukiona fremu zimefungwa/hazijapangishwa halafu mbele kuna mmachinga kajenga kibanda...
Mwanzo sikuwa nimejua huu usumbufu ugumu wa machinga kuhama unasababishwa na nini iwapo wanapewa maeneo yanayorusiwa kufanya biashara zao?

Sasa nilichokigundua kutoka kwa watu niliokuwa nawafahamu wanaenda mjini kufungua biashara zao kumbe ni hivyo vibanda vya chuma na mbao walikuwa wameondoka kwenye fremu wakajenga vibanda vya chuma na mbao mjini kufanyia biashara zao Sasa maeneo wanayopewa ni madogo kwaajili ya machinga wa ukweli na hao wengine wanaohitaji eneo kubwa Ili biashara zao zitoshe au biashara zao nizamjini tu hivyo nje ya mji hazifanyiki vizuri kama saluni za kike na urembo, saluni za kiume, ushonaji, miamala ya pesa vyote vinahitaji chumba na vyumba vilitumika hivyo vya mbao na chuma Sasa huu ugomvi sijui utaishia wapi.
 
Ni takribani wiki mbili sasa wafanyabiashara ndogo-ndogo (wajasiriamali au wamachinga) waliagizwa na serikali za mikoa mbalimbali kuhama kutoka katikati ya miji mikubwa na ama kuelekezwa wapi waende au bila kupewa eneo mbadala na rafiki kwa biashara...
Waondoke, kwanini wanafanya biashara kwenye reserve za barabara?
 
Ni takribani wiki mbili sasa wafanyabiashara ndogo-ndogo (wajasiriamali au wamachinga) waliagizwa na serikali za mikoa mbalimbali kuhama kutoka katikati ya miji mikubwa na ama kuelekezwa wapi waende au bila kupewa eneo mbadala na rafiki kwa biashara...
Tueleze uliko ili machinga wahamie kwenu.
 
Back
Top Bottom