Kuhamia Dodoma kulivyovuruga ndoa yangu hadi najuta sasa

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,531
22,006
Hapa naandika ni usiku Wa manane sina usingizi nawaza mke Wangu aliyehamia Dodoma kikazi!

Naomba suala la kuhamia Dodoma serikali ifikilie na ndoa zetu zipo hatarini;

Mimi kiufupi rasmi sasa nimethibitisha mke Wangu tangu ahamie Dodoma mahaba yamepungua kabisa, nimejaribu kujikakamua kusafiri kwenda Dodoma Mara Kwa Mara lakini sasa naona mambo yangu yanayumba taratibu taratibu!

Sielewi hatima ya hii ndoa inakoelekea;
Nimeshazoea kulala huku nimekumbatia sasahivi nalala peke yangu; inauma sana!

Sasa hivi naishi kisela na wanangu waliopo darasa la tatu na la tano. Nilitegemea kufurahia maisha na mke Wangu kwenye nyumba hii Mpya tuliyohamia hivi majuzi; sasa imegeuka ghetto kwangu na wanangu!

Ndoa ilitufanya tuwe kitu kimoja lakini binadam anataka kututenganisha

Sasa tumebaki Mimi na watoto, house girl na Binti mmoja ambaye ni mdogo wake na mke Wangu katika nyumba kubwa kama hii sielewi mwisho wake!!

KIUFUPI NDOA YANGU IMEYUMBA TANGU WAHAMIE DODOMA
*********************************
Malezi mazuri watayapata wapi hawa satoto Wangu wawili Wa kike? Maana wakiharibikiwa itokee watiwe mimba, basi miaka 60 itahusika Kwa kauli ya waziri mkuu!!

NIFANYEJE KUJINASUA?
 
Pole, lakini mmoja wenu akubali ku surrender kwa mwenzie e.g. ama wewe uhamie Dodoma na kuhamishia shughuli zako huko na kisha upangishe hiyo nyumba yenu mpya, ama Mama aache kazi atafute namna nyingine ya kupata riziki Dar

Vinginevyo hiyo ndoa itazaa makelele ama kwako ama kwake !! Tena soon
 
Wednesday, February 22, 2017
Mpango wa kuhamia Dodoma unavyotikisa ndoa


DOM.png



Kwa ufupi
Tayari baadhi ya wafanyakazi wa wizara mbalimbali wameshahamia mkoani Dodoma kutekeleza uamuzi huo uliotangazwa mwaka jana na Rais John Magufuli.

By Imani Makongoro, Mwananchi imakongoro@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano kuanza kutekeleza mpango wa kuhamishia makao makuu mkoani Dodoma, umeibua hofu ya kusambaratika kwa baadhi ya ndoa, hukuWizara ya Afya ikianza kutoa ushauri nasaha kwa wanandoa.

Tayari baadhi ya wafanyakazi wa wizara mbalimbali wameshahamia mkoani Dodoma kutekeleza uamuzi huo uliotangazwa mwaka jana na Rais John Magufuli.

Kuhamia Dodoma kutamaanisha baadhi ya wafanyakazi ambao wake au waume zao wameajiriwa sehemu nyingine, kulazimika kuishi mikoa miwili tofauti na wenzi wao.

Mmoja wa wanandoa waliowahi kukumbwa na hali kama hiyo ni Charles Boniface Mkwassa, ambaye alilazimika kuishi ya upweke baada ya mkewe kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya.

“Mke na mume kuishi mbalimbali inahitaji umakini wa hali ya juu, kinyume na hapo ndoa itatetereka,” anasema kocha huyo mkongwe ambaye kwa sasa ni katibu mkuu wa Yanga.

Huku akicheka Mkwassa, anasema “Mimi na mke wangu (Betty) mbona tuliishi mbalimbali kwa miaka mingi. Mimi nilikuwa Dar es Salaam na yeye alikuwa mkuu wa wilaya, lakini tuliweza kuishi, ingawa haya mambo yanahitaji umakini kweli kweli.

“Ni kweli kuna baadhi ya wanandoa, mmojawapo atalazimika kuhamia Dodoma kutokana na mchakato uliopo, lakini ni kitu cha kuwekana sawa kweli, japo Dodoma si mbali na bahati nzuri Rais amesema ataleta treni la umeme hivyo itawarahisishia baadhi yao kukutana na familia zao siku za mwisho wa wiki.”

Zuberi Makuru, anayeishi Gongo la Mboto ambaye mkewe ni mwajiriwa serikalini na yuko mbioni kuhamia Dodoma anasema haoni sababu ya kumfuata.

“Haiwezekani niache mji wangu nihamie Dodoma. Hii itakuwa ngumu kwangu siwezi na sitofanya hivyo,” alisema.

“Hapo sidhani kama kutakuwa na uaminifu tena. Kama akiamua kwenda, acha aende tu, lakini sina imani na huko aendako.”

Makuru alisema mtu akiwa mbali na mwenza wake ni rahisi kushawishika, hasa wanapoishi mikoa au nchi tofauti.

“Kama akienda tutaendelea kuishi kama mke na mume tu kwa kuwa tulishafunga ndoa lakini kimatendo na mapenzi kama ya awali, sitarajii kama yataendelea,” alisema Makuru

Alipoulizwa kuhusu kumtembelea mkewe siku za mwisho wa wiki au mkewe kumtembelea Dar es Salaam ili kuendelea kudumisha ndoa yao, alisema anadhani utaratibu huo utafanyika miezi ya awali kisha utatoweka.

“Asikwambie mtu, kitendo cha kusafiri kumfuata mkeo au mumeo nionavyo kitafanyika kwa miezi kadhaa, lakini baadaye kitakata. Acha aende kwa kuwa sina namna kwa kuwa tunatafuta fedha, lakini naona dalili za kulegalega kwenye ndoa,” alisema.

Paul Mwangosi, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya watoto, anasema kwa kiasi fulani mpango wa kuhama utasababisha usumbufu kwa watoto, lakini kwa wazazi si tatizo kubwa kama lengo ni kuongeza kipato cha familia.

“Si tatizo kubwa sana kama mmoja atabaki Dar es Salaam na mwingine kwenda Dodoma au hata mkoa mwingine kwa sababu ya kufanya kazi na kuongeza kipato cha familia. Hayo ni makubaliano ya pande zote mbili, yaani mke na mume na namna atakavyomheshimu mwenzi wake huko atakapokuwa,” anasema.

Mtu mwingine anayeona mpango huo ni mtihani lakini ni rahisi kwa wale ambao dini zao zinaruhus, ni Najaha Bakari, ambaye ni mwajiriwa wa Serikali.

“Naona kama ndoa nyingi zitavunjika lakini kwetu sisi ambao dini inaruhusu wake wanne hata kama hakukuwa na ulazima wa mume kufanya hivyo, hii itamlazimu aongeze mke mwingine,” alisema Bakari.

“Kitaalamu tunaambiwa mwanaume hawezi kukaa muda mrefu pasipo kufanya tendo la ndoa, hivyo aidha uache kazi ili ulinde ndoa au ukubali kuwa na mtu mwingine wa kukusaidia majukumu ya ndoa yako. Yaani huu ni mtihani kweli kweli.”

Lakini, Dorice John, ambaye anafanya kazi kampuni binafsi ambaye ameolewa na mfanyakazi serikalini anayetakiwa kuhamia Dodoma, ameshapata njia ya kunusuru ndoa yake.

“Siwezi kumuacha mume wangu aende Dodoma peke yake eti mimi nibaki Dar es Salaam,” alisema John.

“Nasisitiza tena siwezi, kama ataondoka nitafuatana naye na kuacha kibarua changu Dar es Salaam sababu kule Dodoma kampuni ninayofanyia kazi haina tawi, hivyo sina namna zaidi ya kuacha kazi.”

Madhara ya wanandoa kuishi mbali

Suala hilo la wanandoa kuishi mikoa miwili tofauti lina madhara, kama anavyobainisha mhadhiri msaidizi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Dunstan Haule.

“Bora Mwananchi mlivyoliona hili mapema. Achilia mbali ndoa kulegalega au hata kuvunjika, lakini kuna vitu vingi vitaibuka hapa,” alisema Haule.

Anasema mbali na madhara ya kijamii, wanandoa wanaweza kuathirika hata kiafya, kuibuka kwa migogoro ya ndoa na hata uhusiano na watu wengine.

“Kuoana ni kitu kingine na ndoa ni lile tendo la ndoa, hivyo mke au mume anapokuwa mbali kwa muda mrefu, kwa kiasi fulani huwa inachangia kuharibu ndoa. Hata kazi nyingi kwa mmojawapo pia huchangia kuvuruga ndoa, lakini pia uhusiano wa wazazi na watoto vilevile unapungua,” anasema Haule.

“Hali huwa ngumu zaidi kwa wanandoa pale wanapokuwa maeneo yenye baridi, wengi wao, hasa wanaume, hushindwa kuvumilia na kujikuta wakishawishika kuchepuka. Huko anakochepukia hajui kama ni salama au la hivyo kuhatarisha hata afya yake pia.”

Pia anasema mpango huo unaweza kuathiri familia nyingine kutokana na ukweli kuwa tayari zimewekeza Dar es Salaam na ni vigumu kuanza maisha mengine mapya Dodoma.

“Utakuta mtu ana nyumba Dar es Salaam, hawawezi kuondoka wote lazima mmoja atabaki. Kama ni baba ndiye mtumishi wa umma, atakwenda kwanza kuangalia ustaarabu wa huko na kuiacha familia Dar es Salaam. Hapo sasa kama hakuna umakini lazima ndoa itatetereka,” alisema.

“Sijui Serikali imejipangaje katika hili?”

Sheria kwa wanandoa wanaoishi mikoa tofauti

Kama wanandoa wanadhani wanaweza kutumia sheria kulinda ndoa zao, hawataweza kwa kuwa Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 haijalizinmgatia, kwa mujibu wa Frank Chacha, ambaye ni mwanasheria.

“Ni utaratibu tu ambao umewekwa kwamba mmoja kati yao anaweza kuomba kuhamishiwa karibu na mwenzi wake,” alisema Chacha.

“Waliweka utaratibu huu kwa lengo la kuzuia maambukizo ya Ukimwi. Hata kwenye sekta binafsi pia utaratibu huu upo, lakini katika sekta hizi tatizo linakuja pale kampuni ambayo ama mke au mume anafanyia kazi haina tawi katika mkoa husika.

“Lakini kuna baadhi ya taasisi kama benki na nyinginezo ambazo ziko nchi nzima, huwa wanandoa wanaomba na kuhamishwa.”

Wizara ya Kazi yafunguka

Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama alisema mpango huo hautatekelezwa kwa mkupuo, bali kwa awamu ili watumishi ambao ni walengwa wapate fursa ya kuweka mambo sawa katika familia.

“Zoezi la kuhamisha watumishi wa Serikali litafikia tamati 2020, si la kuisha leo wala kesho,” alisema.

“Hivi sasa ni watumishi wa Serikali wanaohamia Dodoma na mawaziri na manaibu, makatibu wakuu na manaibu na baadhi ya watumishi wachache katika ofisi hizo ambao hadi kufikia Februari 28 wawe wamehamia Dodoma.

“Baada ya hao, itaingia awamu ya pili ambayo itahusisha baadhi ya watumishi kulingana na bajeti itakavyokuwa ikipangwa hadi 2020.”

Wapatiwa ushauri nasaha

Pamoja na kuhama kwa awamu kutoa fursa ya familia kujipanga, Serikali imeanza kutoa tiba ya ushauri nasaha kwa watumishi wake wanaotakiwa kuhamia Dodoma.

Mpango huo unafanyika kuwaandaa kisaikolojia wafanyakazi ambao watajikuta wakitakiwa kuhamia mji huo mkuu ulio katikati ya nchi.

Wiki tatu zilizopita ushauri huo nasaha ulitolewa kwa watumishi wa Wizara ya Ujenzi, Mwananchi imebaini.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu aliithibitishia Mwananchi kuwa wizara yake inatoa ushauri kwa watumishi wanaohamia Dodoma na kueleza kwamba ni kuwaandaa kukabiliana na mazingira tofauti.

“Tuliwaita baadhi yao na kuongeza nao, zoezi hili ni endelevu na wizara ilifanya hivyo ili kuwaandaa kwa kuwa wanakwenda katika mazingira tofauti na waliyoyazoea,” alisema.

“Hatukufanya hivyo kwa kumaanisha kwamba wana matatizo fulani, la hasha. Isipokuwa ni kuzungumza nao kirafiki kwa ajili ya kuwashauri na kuwaweka sawa katika kuanza maisha mapya ya mkoani Dodoma.”

Uamuzi wa kuhamia Dodoma ulifikiwa mwaka 1973 na kutangazwa rasmi mwaka 1974, lakini utekelezaji wake ukakumbwa na matatizo ya kifedha baada ya nchi kuingia katika vita dhidi ya Uganda na baadaye mtikisiko wa kiuchumni wa dunia.


Hapa naandika ni usiku Wa manane sina usingizi nawaza mke Wangu aliyehamia Dodoma kikazi!
Naomba suala la kuhamia Dodoma serikali ifikilie na ndoa zetu zipo hatarini;
Mimi kiufupi rasmi sasa nimethibitisha mke Wangu tangu ahamie Dodoma mahaba yamepungua kabisa, nimejaribu kujikakamua kusafili kwenda Dodoma Mara Kwa Mara lakini sasa naona mambo yangu yanayumba taratibu taratibu!
Sielewi hatima ya hii ndoa inakoelekea;
Nimeshazoea kulala huku nimekumbatia sasahivi nalala peke yangu; ina uma sana!
Sasa hivi naishi kisera na wanangu waliopo darasa la tatu na la tano,
Nilitegemea kufurahia maisha na mke Wangu kwenye nyumba hii Mpya tuliyohamia hivi majuzi; sasa imegeuka ghetto kwangu na wanangu!
**Ndoa ilitufanya tuwe kitu kimoja lakini binadam anataka kututenganisha**
Sasa tumebaki Mimi na watoto, house girl na Binti mmoja ambaye ni mdogo wake na mke Wangu katika nyumba kubwa kama hii sielewi mwisho wake!!
**KIUFUPI NDOA YANGU IMEYUMBA TANGU WAHAMIE DODOMA**
*********************************
Malezi mazuri watayapata wapi hawa satoto Wangu wawili Wa kike? Maana wakiharibikiwa itokee watiwe mimba, basi miaka 60 itahusika Kwa kauli ya waziri mkuu!!
NIFANYEJE KUJINASUA?
 
Hizo ndo changamoto za ndoa mkuu ukiweza mwachishe kazi mtafutie kazi ambayo atakuwa karibu au kubali na wewe hamia dodoma
 
Pole, lakini mmoja wenu akubali ku surrender kwa mwenzie e.g. ama wewe uhamie Dodoma na kuhamishia shughuli zako huko na kisha upangishe hiyo nyumba yenu mpya, ama Mama aache kazi atafute namna nyingine ya kupata riziki Dar

Vinginevyo hiyo ndoa itazaa makelele ama kwako ama kwake !! Tena soon
Kuacha kazi yeye ni ngumu! Halafu na Mimi kuhamia Dodoma ni ngumu sana; kazi zangu nilizowekeza dar na kutengeneza soko siwezi kuhama; kitendo cha kuhamisha shughuli zangu Dodoma itakua ndiyo kufilisika kwangu; SIWEZI KABISA KUHAMIA DODOMA, Sasa sijui hatima yangu; wakati mwingine najuta sijui kwanini nilioa msomi
 
Hii ndiyo faida ya kuoa mwanamke asiye na elimu, popote utakapopelekwa una hama nayeee. Ukiwa na biashara unaiuza una hama tu na mtaji unaenda kuianzisha huko.
Maana hawa wasomi ukimwambia aache kazi hataki, hata kama inamaslahi madogo kwetu kisa tu ni mwajiriwa was serikali. Tuoe tunaowaweza tu sasa.
 
Kuacha kazi yeye ni ngumu! Halafu na Mimi kuhamia Dodoma ni ngumu sana; kazi zangu nilizowekeza dar na kutengeneza soko siwezi kuhama; kitendo cha kuhamisha shughuli zangu Dodoma itakua ndiyo kufilisika kwangu; SIWEZI KABISA KUHAMIA DODOMA, Sasa sijui hatima yangu; wakati mwingine najuta sijui kwanini nilioa msomi
Kama mpo makini mapenzi ya mbali ni matamu sana, pale unapojua weekend hii ninamuona, maandalizi yake na ile excitement, lakini wote muwe na mwelekeo mmoja.
 
Kamata mdogo mtu sasa,wewe vipi yaani fulsa inakuja alafu unakuja kulialia hapa??kweli wewe ni mwanamme wa dsm tafuna huyo upoze machungu
 
Kuacha kazi yeye ni ngumu! Halafu na Mimi kuhamia Dodoma ni ngumu sana; kazi zangu nilizowekeza dar na kutengeneza soko siwezi kuhama; kitendo cha kuhamisha shughuli zangu Dodoma itakua ndiyo kufilisika kwangu; SIWEZI KABISA KUHAMIA DODOMA, Sasa sijui hatima yangu; wakati mwingine najuta sijui kwanini nilioa msomi
Changamoto
 
Kama mpo makini mapenzi ya mbali ni matamu sana, pale unapojua weekend hii ninamuona, maandalizi yake na ile excitement, lakini wote muwe na mwelekeo mmoja.
Mama mapenzi ya mbali vishawishi katikati hapa ni vingi tena kwa wote tu. Ingawa hata mkiwa pamoja bado ni vingi lakini uwepo wa mwenza kidogo ni kinga
 
Ninyi mnaojadili ndoa mtakuwa maskini.kama hutaki kwenda dodoma acha kazi.Kuna batalions la vijana wenye mori wa kazi.Mtume paulo hakioa ndio maana aliweza kuhubiria mataifa mengi.Wengi nchi hii wanatakiwa bakora.
 
Kuacha kazi yeye ni ngumu! Halafu na Mimi kuhamia Dodoma ni ngumu sana; kazi zangu nilizowekeza dar na kutengeneza soko siwezi kuhama; kitendo cha kuhamisha shughuli zangu Dodoma itakua ndiyo kufilisika kwangu; SIWEZI KABISA KUHAMIA DODOMA, Sasa sijui hatima yangu; wakati mwingine najuta sijui kwanini nilioa msomi
Brother binafsi nimekuelewa. If you real mean it. Mkeo aache kazi na arudi atulie Nyumbani, then mfungulie biashara atakayokuwa anaisimamia at the same time akiwa anatafuta kazi nyingine hapa hapa town. Mjulishe malengo yake ya kutafuta hela ni watoto. Endapo atazipata huko Dodoma akakuta watoto wameshakuwa na Tabia mbaya kwa kukosa malezi ya mama basi hizo pesa zake zitakuwa hazina maana yoyote.

Brother kwanza mtege umsikie yeye anamawazo gani juu ya mstakabali wa ndoa yenu. Ukiona anajibu pasina kuumia kama wewe, jiulize je alipoambiwa kwenda Dom alifurahia au alilia? Kama alifurahia basi kuna tatizo upande wake la kiuaminifu, but kama alilia basi anaipenda sana ndoa yake ukimwambia unamfungulia ofisi Dar na aache kazi arudi atafurahia pia.
 
Back
Top Bottom