Kuhama wabunge ni fursa kwa vyama kufanya siasa

Benson Mramba

Verified Member
Oct 29, 2013
586
1,000
Kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko ya vyama vya siasa kunyimwa fursa ya kufanya mikutano ya hadhara.

Aidha kwa miaka mingi chaguzi ndogo zimekuwa fursa ya vyama kujijenga au kuporomoka kisiasa kabla ya uchaguzi Mkuu. Kati ya mwaka 2010 hadi 2015 CHADEMA iliimarika sana kupitia chaguzi ndogo.

CHADEMA ilishinda uchaguzi wa jimbo la Arumeru Mashariki na Kata nyingi sana na kupata kura nyingi sana Igunga, Kalenga na kwenye Kata mbalimbali ukilinganisha na matokeo ya uchaguzi Mkuu wa 2010.

Matokeo hayo yaliongeza mvuto wa chama kiasi cha kuvuta mgombea urais, wagombea ubunge na Udiwani katika uchaguzi wa 2015.

Fomu za kugombea ndani ya chama cha CHADEMA zilipanda kutoka tsh 50,000 kwa ubunge hadi 250,000 wabunge wa majimbo na 500,000 kwa Wabunge wa viti Maalum. Hii ilisababisha na wingi wa watia nia.

Kwa anachokifanya Mbowe na Vijana wake ikifika 2020 CHADEMA itakosa wagombea na ikipata watakuwa vimeo. Wagombea wote makini watakimbilia CCM.

This is just the principle of political marketing.

Ni bahati mbaya tu CHADEMA na wapinzani hawana hela na watanzania hawako tayari kuwachangia tena kwasababu wanajua wanapokea ruzuku kubwa lakini pia hawawamini viongozi wa upinzani.
 

DuppyConqueror

JF-Expert Member
Mar 30, 2014
9,448
2,000
Waelewa na werevu wanazidi kuoambanua mbivu na mbichi.
Inashangaza viongozi wa juu wa CDM wanasingizia murder attemp ya Lissu ni serikali. Cha kusikitisha, hawatoi hata chembe ya ushahidi.
2. Wanasema CCM inanunua wabunge..hapo pia...hawatoi hata chembe ya ushahidi...inasikitisha sana hasa taarifa hizi zikitokea kwa viongozi..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom