Kuhama kwa hiyari Ngorongoro ni pigo kwa wasioitakia heri Serikali, wenye uchu wa madaraka

fimbo ya mpera

Senior Member
Oct 1, 2014
101
79
KUHAMA KWA HIYARI NGORONGORO NI PIGO KWA WASIOITAKIA HERI SERIKALI, WENYE UCHU WA MADARAKA
  • Tuhuma za kuunga unga zasambazwa kila kona kuichafua serikali, watendaji wake
  • Mitandao ya kijamii yatumika kusambaza uwongo
  • Watumishi wa NCAA wasio waaminifu watumia UDINI, UKABILA Kuhamasisha chuki dhidi ya serikali ya Rais Dkt. Samia
  • Uchu wa Madaraka makubwa baina ya baadhi ya vigogo katika taasisi hiyo wasababisha watupiane tuhuma za uongo
  • Waliokuwa mstari wa mbele kuratibu zoezi la uhamaji wa hiyari kutoka Ngorongoro Kwenda Msomera wazidi kuundiwa zengwe, lengo kuwavunja moyo wasiendelee kumsaidia Rais
Na. HAKI ONLINE MEDIA, Ngorongoro

Uchu wa madaraka makubwa baina ya watendaji waandamizi wa Mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro umesababisha kuibuka mbinu chafu za kuchafuana baina yao huku watendaji wanaoonekana kuwa mstari wa mbele kusimamia maelekezo ya serikali wakiitwa vimbelembele na kushughulikiwa kwa kuchafuliwa na kutukanwa mitandaoni wakiamini kufanya hivyo kutasababisha wapate nafasi kadhaa za juu za shirika hilo.

Taarifa za uhakika ambazo HAKI ONLINE MEDIA inazo zinaeleza kuwa miongoni mwa mambo yanayowakera baadhi ya wagombea madaraka NCAA ni kufanikiwa kwa Kitendo cha wananchi waliokuwa wanaishi hifadhini Ngorongoro kuamua kuhama kwa hiyari kuhamia msomera pasipo na mapambano yoyote baina yao na Serikali au mamlaka ya usimamizi wa eneo hilo NCAA kimesababisha baadhi ya vigogo wa taasisi hiyo ambao hapo awali walikuwa wakihamasisha wananchi wakatae kuhama kwa visingizio mbalimbali ikiwemo kusema ni eneo lao la asili, wabadili mbinu na sasa wameungana na watumiaji mitandao wa chama kimoja cha siasa kuwachafua, kuwapakazia na kuwatungia kila aina ya uwongo na shutuma wenzao wote wanaoendelea na zoezi la uratibu.

HAKI ONLINE MEDIA, inaweza kuthibitisha pasi na shaka namna michezo michafu inayofanywa na baadhi ya vigogo wa NCAA ambao hawakuwa wanataka zoezi la kuratibu uhamaji wa hiyari kutoka hifadhini humo ili kupunguza idadi kubwa ya watu inayopelekea msongamano wa majengo, uharibifu wa mazingira na kusababisha vifo, maradhi na kuzalisha vijana wasiojua kusoma na kuandika kutokana na kutokupeleka Watoto wao shule ambapo taarifa zinaonyesha kuwa 64% ya wakazi wa Ngorongoro hawajui kusoma wala kuandika.

Miongoni mwa michezo hiyo ni pamoja na kuzitumia akaunti hewa za mitandao ya kijamii zinazoendeshwa na baadhi ya watumishi wa taasisi hiyo zenye majina mbalimbali ikiwemo KIGOGO KIGOGO, MTIPESA, VERONYIKA na nyinginezo ambazo kimsingi zinasambaza Habari za kutunga na uwongo lengo likiwa ni kumchafua Rais wa Nchi Dkt. Samia Suluhu Hassan ionekane zoezi la watu kuhama ameliratibu vibaya.

Miongoni mwa mbinu wanazozitumia ni pamoja na kusambaza uchonganishi kutumia UKABILA wakitengeneza tuhuma za uchonganishi kuwa WAMASAI wanaoishi eneo hilo wanaonewa jambo ambalo wanajua wazi kuwa ni kinyume na mila na desturi za nchi yetu kuwa hakuna taasisi wala mwnanchi anayeweza kuhudumiwa ama kwa kupendelewa au kwa kupunjwa kwa misingi ya dini yake wala kabila lake kama ambapo wanataka kufanya.
 
Hatujasahau

Uangamizaji wa Jamii ya Wamasai ni doa kubwa sana, na sio kwa Viongozi wa Tanzania tu, bali kwa Watanzania wote na Waafrika kwa Ujumla.

It was Genocide.
 
Back
Top Bottom