Kuhama kituo cha kupigia kura.

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,510
7,541
wadau wa JF,ninatatizwa na hili. kituo nilichoandikishia kupiga kura 2005 ni chuo kikuu cha DSM jimbo la Ubungo wakati huo naishi maeneo ya jirani.sasa ninaishi Kimara jimbo hilo hilo la Ubungo. sasa naomba nifahamu siku ya uchaguzi nitapigia kura wapi? ni chuo au kituo cha karibu huko Kimara ninapoishi sasa?
 
Kwani mbona walisha towa matangazo mengi tu ya jinsi mtu anavyoweza kuhamisha kumbukumbu zake toka kata moja kwenda nyingine ama kutoka jimbo moja kwenda jingine nadhani ilikuwa mwezi wa saba kama sijakosea. Na walishafunga hilo zoezi lilidumu kwa muda wa wiki 2 tu kwahiyo hapo huna jinsi inabidi uende huko ulikojiandikisha ili haki yako isipotee
 
Ni pale ulipojiandikisha awali endapo hujahamisha taarifa zako kwenda pahala pengine. KAma hujafanya hivyo, UDSM siyo mbali kapigie kura CHADEMA. GOOD day mtu wangu
 
je kujiandikisha ni kwamba unajiandikisha pale unapoishi au unaweza kwenda kujiandikisha popote tu???
 
Back
Top Bottom