Kuhakikisha ushindi mnono Dr. Slaa apaswa kufika Lindi, Mtwara na Ruvuma..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuhakikisha ushindi mnono Dr. Slaa apaswa kufika Lindi, Mtwara na Ruvuma.....

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 24, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  Kinyume na ngebe za CUF na CCM kuwa wao ndiyo watagawana kura za huko taarifa za uhakika nilizozipata kwa wapenda maendeleo wa huko wangependa Dr. Slaa angalau afike makao makuu ya mikoa hiyo kabla ya uchaguzi kufunga dili ya kiutu uzima.

  Taarifa hizo zinasema wakaazi wa mikoa hiyo wamechoshwa na ahadi za JK za kusisitiza matatizo yao anayafahamu sana bila ya kuwaelezea ufahamu huo umemsaidia nini na kwa nini sasa anataka waendelee kumwamini tena kwa miaka mitano ijayo wakati ameshindwa kuzitekeleza hata ahadi zake za miaka mitano iliyopita haswa kwenye eneo la uchimbaji wa visima vya maji ambapo ndicho kikwazi kikubwa cha maendeleo kwa mikoa hiyo............
   
 2. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  anakwenda mkuu wiki hii nimeona ratiba
   
 3. Da vincci

  Da vincci Member

  #3
  Oct 24, 2010
  Joined: Aug 9, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  sure mimi nipo huku for the time being na watu wapo curious kweli kumuona na kumsikiliza dr wa ukweli moja kwa moja yani at least angepita makao makuu ya wilaya tu kwa siku1 through his chopper he can make it..
   
 4. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwenda bila shaka atakwenda lakini mikoa hiyo sambamba na mkoa wa Pwani wana kasumba ya udini sana. Mikoa hiyo haina tofauti kubwa na ile ya Zanzibar. Si nia yangu kutaka tujadili suala la udini, lakini naona changamoto iliyopo katika mikoa hiyo. Naufahamu vizuri mkoa wa Ruvuma na changamoto zake za kidini, siifahamu sana Lindi na Mtwara. Lakini pia naufahamu vema mkoa wa Pwani na ninajua misimamo ya watu wa huko. Pamoja na umasikini wake, mikoa ya Lindi na Mtwara bado sana katika suala zima la mageuzi ya kweli.

  Mikoa hii ipo nyuma sana kielimu na kiuchumi, haina mwingiliano mkubwa na watu wa nje na hivyo kujikuta kwamba imekuwa ni mtaji mzuri wa CCM. Siku zote CCM inakomba kura nyingi kwa watu wenye elimu ndogo na walio katika dibwi la umaskini. Ndiyo maana hivi sasa wanajitahidi kwa kila njia kuziba nafasi ya wanafunzi wa vyuo vikuu kuweza kupiga kura. Umasikini na ukosefu wa elimu kwa wananchi ndivyo vinavyoendelea kuwapa kiburi CCM. Na hii ndiyo sababu nyingine wanajivunia kura za vijijini na katika mikoa kama hiyo ya kusini, ambako hali ya maisha ya watu bado ni duni na uelewa wao bado uko chini na hivyo kuishabikia zaidi CCM kutokana na zawadi ya khanga, tshirt na kofia tu.
   
 5. KasomaJr

  KasomaJr JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Lukolo nakubaliana na wewe kwa 100% your comments are right....i wish Dr. Slaa angekuwa na muda kufika huko, lakini siku 70 hazitoshi kuzungukia majimbo 401 waungwana.....i know ni haki yao pia kupata kumsikiliza shujaa huyu. Pamoja na hayo yote bado ushindi upo pale pale na nina amini hata kama wapo hivyo walivyo, umasikini, elimu duni, imani n.k bado tuna kula za wananchi ambao kwa hekima ya mungu tu wanaweza kujadili na kuona uongo, uzandiki, upuuzi na unyama wa haya mbwa koko, mbwa mwitu, vibaka, wanyang'anyi majambazi na wevi walio kosa hata chembe ya huruma jumlisha na aibu. Hukumu yao ni juu ya matendo yao......Mapinduzi tayari yamefika ni jukumu letu kuyakubali na kuyapokea kwa mikono miwili kwa maana ya kuleta mustakabari wa taifa hili.
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  dr wa ukweli fika pale songea mjini. nenda peramiho. mbinga, nyasa, namtumbo, namabengo ng'oa mizizi yote iliyooza ya ccm pandikiza mizizi mipya yenye matumaini na nguvu ya chadema. tuletee ushindi na matumaini mapya ktk maisha mapya bila ccm.
   
 7. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Weee huko hafiki, unataka akaaibike? Wacha tu kule kuna wenye akili wasioshawishika na makanisa.

  Kanisa limetoa taarifa kuwa kazi ya kuwadanganya watu wa huko haijakamilika sasa aende kufanya nini?

  Sijui pengine tar 30.10.
   
 8. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2010
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  Ha ha haaa! Zawadi, naomba date.
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Uko wazee wa vibarakashia wako lukuki huwa hawabadiliki hao ni either CCM au CUF.
  Mbaya zaidi ni wa mwisho kimaendeleo na bado wanakomaa na chama tawala
   
 10. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2010
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Chonde chonde jamani tunaomba sana afike na huku kwetu Tandahimba(MTWARA),wananchi wanamsubiri kwa hamu!Taarifa zilizozagaa huku ni kuwa atakuja 25 Octoba,naomba mwenye uhakika wa ratiba hii anijuze.
   
 11. F

  Fanfa JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 25, 2009
  Messages: 538
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni kweli mkuu.
  Ushauri wako ni muhimu sana ukazingatiwa. Hata kama atatumia siku 1 kwa kila mkoa yaani Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani na Dar itasaidia sana kutibua kampeni ya Kiwete aliyofanya juzijuzi katika mikoa hiyo.

  Zenji hata asipoenda haitakuwa ni tatizo
   
 12. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  kuna madrasa al rasul na wajinga
   
 13. r

  robert_m Member

  #13
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Haya ni mambo ambayo sisi tunafikiria juu watu wa mikoa ya kusini, ila nao ni watanzania wanaoumia kama watu wengine. Wapo wajinga na werevu, lakini ni muhimu katika ushindi wa Dr. Slaa (for that matter), hilo ndilo la msingi!

  Napenda kutambua nafasi ya watu wa mikoa ya kusini kimsingi bila kujali background na tamaduni zao, na natumaini kuwa wao pia wanashauku ya kuona maendeleo kama watu wengine, wawe werevu au la.

  Hivyo bado ningali namatumaini makubwa na kuona ziara hiyo kuwa ni ya muhimu sana. We can be enthusiastic with him moving to that side.
   
 14. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2010
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,971
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Yes, ni vizuri sana akienda. Hiyo itasaidia sana kwa watu wale wasijione kuwa wametengwa.
   
 15. R

  Rugemeleza Verified User

  #15
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Dr. Slaa atakuwa Raisi wa nchi yetu yote na kwa hiyo kila kura itakayoweza kupatikana kutoka kila pande zote za nchi ni muhimu. Ninafurahi kuwa anakwenda katika mikoa ya kusini katika wiki ya mwisho licha ya njama chafu za Ikulu na NEC za kuvuruga uchaguzi.
   
 16. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  sick and vomiting
   
 17. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #17
  Oct 24, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Andaeni mapokezi kuanzia j3 atakuwa mikoa ya Lindi na Mtwara, fuatilia ofisi za Chadema Lindi na Mtwara mjini.
   
 18. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #18
  Oct 24, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Huko hana umaarufu, na alivyopiga mahesabu kaona ni bora aahirishe kwenda huko na badala yake arudie maeneo mengine aliyokwishapita ili kujiongezea kura huko, kuliko kupoteza muda kusini.

  Kimsingi hata akienda hatabadili sura yeyote ile ya wapiga kura, hata hivyo atakwenda kama ushahidi tu, ili huko mbele wasije mbeza.

  Mnapopiga mahesabu ya kura, toeni kura za Ruvuma, Lindi, Mtwara na Pwani. Nilisahau, na Zanzibar. Halafu, eti mnawaambie wapenzi wa CHADEMA kuwa Mh Slaa ATSHINDA. Napigwa na bumbuwazi!!!!!!
   
 19. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #19
  Oct 24, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Inabidi aende bse Sla atakuwa raisi wa wote
   
Loading...