Kugundua dawa au chanjo hatuwezi. Vipi kuhusu kutoa uthibitisho wa kitaalamu kuwa dawa hii au chanjo hii si salama?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Kuna madai kuwa chanjo ya corona si salama na maneno mengine mengi tu kuhusu dawa hiyo. Hata hivyo, ukiwaambia wahusika watoe uthibitisho juu ya madai hayo, kamwe hawawezi kufanya hivyo.

Swali nalojiuliza, kama tuhuma hizi ni za kweli, lakini tunashindwa kuzithibitisha na tuna ma-doctor na ma-proffesor kibao, huu si uthibitisho kuwa elimu yetu ni ya kwenye makaratasi tu?

Nilitarajia wasomi wetu waje na details za kitaalamu kuwaumbua wazungu kama tulvyowaumbua kwenye makinikia ila sijui tunakwama wapi!

Kingine: Vyuo vikuu vyetu vimefanya nini au vimefikia hatua gani katika kutafuta chanjo au dawa ya corona?

Na serikali hii inatenga/ imetenga fedha kiasi gani kugharamia ugunduzi wa dawa na chanjo ya corona?

Je, tunasubiri wazungu wagundue dawa/ chanjo then watuuuzie?

Je, hii si moja ya sababu kwanini sisi tutaendelea kuwa masikini huku wenzetu wakiendelea kuwa matajiri?
 
Mkuu mbona Tanzania tayari tumeshagundua?
 
Hao wa kuthibitisha uwezo wa dawa wamesomea huko kwao au wamesoma mitaala ya kwao.

Waafrica au Waswahili tusipokuwa makini tutabaki njia panda kwa mambo mengi sana maana upande mmoja tunatamani tuishi bila kutegemea Wazungu na upande mwingine Dunia wala haitusubiri, maana ok sawa tuseme chanjo sio salama sasa je ya kwetu tutatengeneza karibuni?

Si ajabu tunasubiri ya China ndio tuseme tunaiamini.
 
Hao wa kuthibitisha uwezo wa dawa wamesomea huko kwao au wamesoma mitaala ya kwao.

Waafrica au Waswahili tusipokuwa makini tutabaki njia panda kwa mambo mengi sana, maana upande mmoja tunatamani tuishi bila kutegemea Wazungu na upande mwingine Dunia wala haitusubiri, maana ok sawa tuseme chanjo sio salama sasa je ya kwetu tutatengeneza karibuni?

Si ajabu tunasubiri ya China ndio tuseme tunaiamini.
Ngozi nyeusi tulilaniwa na tutatawaliwa na ngozi nyeupe mpaka mwisho wa hii dunia.
 
Mwafrika ni mtu wa ajabu sana ana tia shaka juu ya chanjo ya Corona wakati huo huo anatumia chanjo ya magonjwa mengine toka kwa hao hao wazungu hopeless kabisa.
Kabla ya hapo tulitakiwa tuje na hoja kuwa corona ni nn? Ni ugonjwa kama magonjwa mengine au umetengenezwa na kusudi flan, je lengo lake ni nn na dawa yake ni ipi?

Je, tunakabiliana nao vipi bila kutegemea wazungu?

Hapo ndo tungekuja na hoja ya kutilia shaka chanjo yao.
 
Tazameni Hiii Video.
 
Mkuu , 'Salary', huu ndio ungepaswa kuwa mjadala wa nguvu, wa maana sana katika jukwaa hili la JF, pamoja na kwamba umeliweka kwenye siasa, kwa hiyo kama kutakuwepo na uchangiaji juu yake utakuwa ni ule ule wa aki"JohnBabtist' na watani wako wengine.

Nami nitaongeza machache katika mwonekano huo huo, hadi hapo itakapoonekana kwamba mjadala unakwenda kivingine.

Haya, nami nianzie hapa:

1. Kuhusu usalama wa chanjo hiyo - kwanza sisi haituhusu, kwa sababu tulishatangaza tayari kuwa Mungu wetu katuwekea kinga. Ni chanjo ipi itakayozidi hiyo ya muumba wetu aliyotuwekea baada ya kusikia maombi yetu? Tumeacha kabisa kupima na kuchukua tahadhari nyingine zozote zinazotakiwa kuchukuliwa ili maambukizi yasienee zaidi; kwa nini sasa tuhangaike na kinga. Jambo muhimu kwetu hapa sasa ni kuhimiza tu hilo, la Kinga kutokuwa salama, pengine uamini wetu huo unatokana na sala tulizompelekea Mungu wetu na yeye kutujibu tusithubutu kabisa kujihusisha na kinga hizo.

2. Ukweli wa tuhuma: njia pekee ya kujua ni kufanya utafiti juu ya kinga hiyo na kuona matokeo yake. Kama hujafanya hivyo, soma tafiti za waliofanya ugunduzi na uendelezi wa chanjo hizo na mamlaka za nchi mbalimbali kuhusiana na hizo chanjo. Wasomi wa kusoma na kuelewa maandiko ya namna hiyo sasa tunao Tanzania, pamoja na kwamba hatuwapi nafasi na fursa nzuri za kuendeleza utaalamu wao.
Katika hili, hapa ndipo tutakapoachwa kwenye mataa hasa na wenzetu, majirani zetu. Wao angalau wanashiriki na kushirikiana na taasisi nyingi toka nje na kupata uzoefu mkubwa, sio katika nyanja kama hizi pekee, lakini sasa ni kama tumejitoa kabisa katika nyanja zote, hasa hizi zinazoinukia kama technology, na maeneo mengine.
Tutajutia sana kupoteza muda huu tunaopooteza kwa kujiweka pembeni.

Kwa hiyo; juu ya tuhuma - sisi badala ya kujishughulisha na kutafuta ukweli, tutakazana kueleza "ukweli" wetu (feki) ili tuendelee kuonekana kuwa taifa lililobarikiwa na Mungu. Ni mtaalam yupi atafanya kinyume cha matamko ya mtawala?

3. Ma-dokta na ma-profesa? Wewe huoni wanavyopigana vikumbo kutafuta teuzi? Ni dokta/profesa gani asiyependa kuteuliwa, ili abaki kwenye maabara akicheza na mapanya?

Miaka hii zaidi ya 60, tumekuwa na taasisi nzuri tu za kutufundishia wataalam wa aina hii, na wengi wamepelekwa nje kusomea mambo haya haya, halafu useme hatuna wataalam. Tafuta wanakoishia hao wataalam, hapo ndipo utakapopata jibu sahihi.

Vyuo na taasisi mbalimbali vimefanya nini, sio kutafuta tu majibu juu ya corona, uliza maeneo yetu yote tulikoweka juhudi ya kufumbua matatizo ya wananchi, si kilimo, si Afya, si elimu, n.k., matatizo kote huko ni yale yale unayotafuta majibu yako juu ya hili janga la corona.
Kwani hatuna matatizo ya "kutu' kuharibu au kufifisha ufanisi wa mitambo yetu? Kuna mTanzania mwenzetu alifanya utafiti wake, ukampa hadi Ph.D. yake katika eneo la kuzuia kutu kwa kutumia mafuta ya maganda ya korosho. Ulishasikia habari nyingine yoyote kuhusu kunufaika kwetu kutokana na juhudi zake hizo?

Sitaendelea kujibu hayo maswali yake mengine yaliyobaki huko chini, kwa sababu majibu yake yanafanana na hayo niliyokuandikia hapo juu.

Kinachokosekana: ni utashi wa kisiasa.
Hawa wenye madaraka, wakiamua kwamba wanataka kusimamia na kuona mafanikio katika eneo lolote tunaloweza kulipa kipaumbele, tutapiga hatua mbele. Miaka mitano inatosha kabisa, kwa mfano, tukiamua kwamba tunataka kuwa na "Chemical industry" yetu hapa itakayozalisha kemikali mbalimbali zinazohitajika maeneo mengi tu duniani na hasa kwenye nchi zetu hizi za kiafrika. Hiki kitakuwa ndio kitovu cha viwanda vingine muhimu kama viwanda vya madawa, mbolea n.k. Mali ghafi za kufanya hivyo tunazo, ambazo hatuna tutaagiza.
Wataalam ambao taifa hili lilikwishawasomesha na wengi wao hata kufikia kustaafu bila ya kuitumia elimu yao hiyo, wengi wapo, ni swala tu la kuwa-'organize' na kuwapa nyenzo za kufanyia kazi. Miaka mitano utaona mabadiliko makubwa. Huu ni mfano tu mmoja.

Corona sisi tuliishinda, na vile vipimo tuliwaeleza dunia nzima kwamba sisi havitufai, baada ya kupima mapapai na mbuzi. Halafu kuna watu kama akina 'Salary' wanaleta maswali yasiyoeleweka na yeyote hapa!

Najua utachoka sana kusoma haya mkuu wangu, lakini uchokozi unaoufanya na kuumiza utulivu wa mawazo hapa sio kitu kizuri.
Nakutakia Heri ya Mwaka Mpya 2021.
 
Kabudi2.jpg
 
Usingemjibu huyo amerukwa na akili...!
Hapo CHADEMA inahusikaje, je haitoshi kuchangia kwa busara kwa kuwa mada ina mantiki?
Watu wakikosoa ni shida,mnawaua
Wakishauri ni taabu, mnawabambikia kesi za uhujumu.

KIPI CHEMA KWENU, HALI HII INALETA UADUI
 
Back
Top Bottom