Kufuzu AFCON 2021: Tanzania yapangwa na Tunisia na Libya

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,876
7,366
Kuelekea kufuzu AFCON 2021 yatakayofanyika nchini Cameroon, Tanzania imepangwa na Waarabu 2 Tunisia na Libya pamoja na Equatorial Guinea

Kumbuka Ni timu 2 za juu tu zinafuzu kwenda AFCON 2021 Kila kundi.
Tunisia
======
Shirikisho la Soka Barani Afrika limetangaza makundi kwa ajili ya kufuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2021 yatakayofanyika nchini Cameroon

EE05F454-52C1-477D-BCEB-AE0EF1EC3FA6.jpeg


Katika Kundi A zipo timu za Mali, Guinea, Namibia na mshindi katika mechi za awali kati ya Liberia na Chad huku katika Kundi B zipo timu za Burkina Faso, Uganda, Malawi na mshindi katika mechi za awali kati ya South Sudan na Seychelles

Kundi C zipo timu za Ghana, South Africa, Sudan na mshindi kati ya Mauritius na Sao Tome na katika Kundi D zipo timu za DR Congo, Gabon, Angola na mshindi kati ya Djibouti na Gambia

8FD10F1E-3065-4BED-9551-2B6CD73FDAC6.jpeg


Kundi E kuna Morocco, Mauritania, Central Africa na Burundi huku Kundi F zikiwepo Cameroon, Cape Verde, Mozambique na Rwanda; Kundi G linabeba Egypt, Kenya, Togo na Comoros Islands

Kundi H zipo Algeria, Zambia, Zimbabwe na Botswana; Kundi I zipo Senegal, Congo, Guinea-Bissau, Eswatini; Kundi J zipo Tunisia, Libya, Tanzania na Equatorial Guinea na katika Kundi K zipo Côte d'Ivoire, Niger, Madagascar, Ethiopia huku kundi la mwisho la Kundi L likiwa na Nigeria, Benin, Sierra Leone na Lesotho
 
Tunafuzu Cameron 2021..wakija Taifa wote wanakufa hakuna namna..Bashite aondolewe kuwa mwenyekiti kamati ya hamasa
 
Equtorial Guinea tunawapga nje ndan then tunisia na mwenzie tuna wapiga ndan hapo points znafka 12.. NJIA NYEUPE

Unawajua Equatorial guinea? Wale ni wahispania mkuu

Kama Lesotho mmeshindwa mtaweza kwa Equatorial Guinnea
 
Sisi tuanze tu kuwaandaa kina Pierre Liquid wengi kwaajili ya uhamasishaji na si vinginevyo,maana tunaongea sana kuliko vitendo
 
Unawajua Equatorial guinea? Wale ni wahispania mkuu

Kama Lesotho mmeshindwa mtaweza kwa Equatorial Guinnea
Hao jamaa weupe tu..zamani walikuwa wanachukua wachezaji mpaka nane wa kibrazil..CAF imewashitukia..Wana mchezaji mmoja Spain viligi vidogo hata Fsrid Musa yuko juu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom