Kufuzu AFCON 2021: Libya 2 - 1 Taifa Stars | Mchezo wa mzunguko wa pili Kundi J

kaka-blaza

Member
Nov 7, 2019
84
124
Ni dhahiri kuwa timu ya Taifa kwasasa ipo kwenye kiwango kizuri sana (kinavutia).

Leo tarehe 19.11.2019 majira ya saa 22:00 timu yetu ya taifa (taifa stars) itashuka dimbani kumenyena na Libya ni katika harakati za kuwania kufuzu kucheza fainali za AFCON mwaka 2021.

Taifa Stars ambayo ilimpiga Equatorial Guine katika game ya kwanza iliyochezwa nyumbani katika dimba la Mkapa, itakuwa ikitafuta kufuzu kwa mara ya pili mfululizo kushiriki mashindano hayo makubwa ya mpira wa miguu kwa ngazi ya mataifa katika ukanda huu wa Afrika.

Mungu Ibariki Tanzania , Mungu IBARIKI Taifa Stars..

UPDATES
CF2C5C2E-E701-4DD0-B6D2-F18F9AD94EF4.jpeg


69CC8B28-ECCF-44F4-BB4D-F68C817B65A1.jpeg

Msimamo wa Kundi J baada ya michezo ya leo
0B9501E8-0AB4-4517-BE40-DC4EFBC9A1EC.jpeg
 
As longer as Samatta na wenzake wapo fit tutegemee tu utekelezaji mwema wa ilani ya nchi ushindi daima kushindwa kwetu mwiko.
 
Nini kimekufanya useme kuwa Taifa Stars iko vizuri sana? Hebu jibu kwa kina hili swali kisha tuendelee.

Au kwa kuifunga equatorial Guinea 2 kwa 1 ?
 
Watanzania tukitoka nje ya mipaka yetu tunakuwa kama kuku mdondo..

Let's wait tuone kama tunaweza kufanya lolote..

Go go TStars
 
Namna gani hapa libya wanakosa bao la wazi kabisa baada ya mpira kugonga mwamba
 
Dakika ya 3 Samata anajaribu kupiga shuti lakini inakua ni goal kick
 
Hatarii kwenye lango la taifa stars lakini mpira unaondoshwa na mabeki kwenye hatari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom