Kufutwa kwa vipengele vya ukomo wa ubunge wa miaaka 15 kwenye rasimu ya katiba

Muk

JF-Expert Member
Sep 4, 2012
547
70
Inasikitisha sana kwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba kufuta kwa vipengele vya mbunge kuwajibishwa na wananchi walio mchagua kwa kushindwa kutimiza majukumu yake na kile kipengele cha ukomo wa ubunge kwa miaka 15 chanzo itv news saa mbili usiku
ihi kweli wale walio out ya bunge hilo na walio ndani ni nani mwenye uloho wa madaraka? Inasikitisha sana.
 
Wajumbe wabunge hilo ambalo kimsingi limejaa wanasiasa,kamwe hawawezi kukubali kunyang'anza tonge mdomoni.Hata issue ya kuondolewa viti maalumu hakika itapingwa vikali.Hawakawii kusema hayo si maoni ya wananchi ila niya WARIOBA.Shame on them!
 
Inasikitisha sana kwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba kufuta kwa vipengele vya mbunge kuwajibishwa na wananchi walio mchagua kwa kushindwa kutimiza majukumu yake na kile kipengele cha ukomo wa ubunge kwa miaka 15 chanzo itv news saa mbili usiku
ihi kweli wale walio out ya bunge hilo na walio ndani ni nani mwenye uloho wa madaraka? Inasikitisha sana.

Mkuu ile Hotuba ya Rais siku ya ufunguzi wa Bunge ndio msimamo wa CCM, pia ndio katiba yenyewe
 
Watasema hayo si mahitaji ya watanzania.Kwamba watanzania wanataka maji,barabara na bei ya mazao.
 
Watanzania hawana mtetezi bali waganga njaa.
Umaskini wa viongozi wetu ni janga la kitaifa.

Mtu anaingia madarakani akiwa maskini anatoka akiwa milionea unategemea atatamani kutoka madarakani kwa kelele za washika vibendera.

Aliyefikiri kwamba CCM itazungumzia maisha ya watanzania maskini amejidanganya .Katiba inayotungwa na viongozi huwa ni ya kuwalinda na sio kuwahukumu.
Hii nchi tatizo ni watanzania kukosa elimu ya kujitambua.Wanaamini kwamba katiba itawaletea maji.
 
Dah mbona majanga sasa wanateyea wananchi gani kama wanachakachua maoni ya wananchi ama kweli tumepoteza dira kama taifa kwa kuendekeza masilahi ya wachache wenye kujiona wana hati miliki na nchi sasa hapo ni katiba ya wananchi au ya wenye tamaa wachache na ndo mana hatuendelei kwa kuendekeza upuuzi badala ya kuweka masilahi ya taifa mbele
 
Wakuu kinachofanyika dodoma ni uchakachuaji na sio kingine! Katiba ya ccm ipo kwenye hotuba ya jk wakati akizindua bunge la katiba kule dodoma. Mambo yote aliyoyapinga ndo yanaondolewa kwenye rasimu!
 
Nawasubiri kwenye akidi ya maamuzi tu!!!!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Back
Top Bottom