Kufutwa kesi ya Mbowe ni ushahidi kuwa kila mhimili uko huru na imara hauingiliwi na mhimili mwingine

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,904
Kufutwa kesi ya Mbowe ni ushahidi kuwa kila mhimili uko huru na imara hauingiliwi na mhimili mwingine

Jaji Tiganga alisimama kidete kama mhimili huru kusema Mbowe na wenzie wana kesi ya kujibu waanze kujitetea kutokana ushahidi uliopatikana

Mhimili wa Serikali ukiwa huru ambao ndio washitaki wakasema hatuna mpango wa kuendelea na hii kesi.Jaji akasema sawa nyie si ndie washtaki.

Ingekuwa mahakama inaingiliwa na Serikali jaji Tiganga siku ya kuamua kama kuna kesi au la kama Serikali na mahakama ni kitu kimoja angemwachia Mbowe na wenzie kuwa ushahidi hautoshi hawana kesi ya kujibu

Wale mnaosema Serikali inamiliki mahakama jifunzeni kupitia hii kesi Mahakama imeonyesha kuwa iko huru haiyumbishwi na Serikali muhimili mwingine
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚,dah punguzeni basi kutetea the obvious!

Jaji anatoa taarifa kuwa Mbowe ni mgonjwa hivyo hataweza kufika mahakamani,wakati huo huo kumbe Mbowe ni mzima wa afya!
Hukuona pia namna ambavyo baadhi ya vielelezo vilitoka mahakamani na kuwafikia upande wa mashtaka bila utaratibu?
 
Uliambiwa anaumwa nini? Yaweza kuwa kichwa alisikia kinauma wakampa Hedex kikatulia
 
tukirekebisha katiba, tuweke kifungu cha Sheria cha kumbana DPP kidogo, kwamba kama akitaka kufuta kesi basi atoe na sababu za msingi za kufanya hivyo vingienvyo washitakiwa wapewe nafasi ya kumshitaki na kuomba fidia kwa Jamhuri.

Katiba imempatia DPP mamlaka makubwa mno ya kufungua ama kufuta kesi bila kutoa sababu na huna ruksa kuhoji.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚,yaani Mwamba siku zote za kesi hajawahi kuugua,aje kuugua siku ambayo anaachiwa huru!
Jiongeze!
Ugonjwa siri ya daktari na mgonjwa .Mbowe na Daktari wake ndio wajua vizuri kamuulize Mbowe
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚,yaani Mwamba siku zote za kesi hajawahi kuugua,aje kuugua siku ambayo anaachiwa huru!
Jiongeze!
Usiwe mtumwa wa historia kwa hiyo kama hujaumwa mwaka jana ni kuwa mwaka huu hutaumwa?
 
Haki imetendeka tunamshukuru Mungu Mbowe kawa huru hizo nyingine ni mbwembwe
 
tukirekebisha katiba, tuweke kifungu cha Sheria cha kumbana DPP kidogo, kwamba kama akitaka kufuta kesi basi atoe na sababu za msingi za kufanya hivyo vingienvyo washitakiwa wapewe nafasi ya kumshitaki na kuomba fidia kwa Jamhuri.

Katiba imempatia DPP mamlaka makubwa mno ya kufungua ama kufuta kesi bila kutoa sababu na huna ruksa kuhoji.
 
Jaji.Tiganga hakuwa na.option,ilibidi aseme kwamba wana kesi ya kujibu ili baadaye dpp aseme kwamba hana nia ya kuendelea kesi.Utashindwaje kuendelea na kesi wakati walidai kwamba mashahidi wao walikuja na ushahidi ulioshiba ?. Hii ilikuwa ya mchongo,jaji wa ...na mawakili wa ....pamoja na mashahidi wote wa....
 
Naunga mkono hoja, na aliyefuta kesi ni DPP, ofisi ya DPP iko huru, haiingiliwi.
P
Sijajua hasa shida ni nini hasa iliyosababisha uwezo wako umedondoka kama nazi. Jee ni uzee unakukabili au ulipoamua kuuza uhuru wako kwa kugombea Kawe kupitia chama kinachotoa nafasi kwa sharti la kuweka ubongo kabatini?
Mbona wapo waandishi wamekuwa wazee na umahiri ndio umeongezeka? (eg. Ulimwengu) na wapo waliogombea kupitia chama chako na bado afya ya akili ni imara?
Ndugu yangu Pasco, itunze heshima uliyoijenga siku nyingi kwa kuandika ukweli.
 
Back
Top Bottom