Elections 2010 Kufuta alama ya wino kwenye kidole

Mutensa

JF-Expert Member
Feb 20, 2009
421
90
Wanajamvi,
namshukuru Mungu nimepiga kura jumapili iliyopita. Samahani kuwasumbua katika hili lakini nadhani litawasaidia wengi katika kipindi hiki, je ule wino tuliowekewa kama alama ya kupiga kura tunaweza kuutoa kwa dawa/sabuni/ au kimiminika gani? Mpaka leo sijafanikiwa kusafisha kidole hicho.
 
Wanajamvi,
namshukuru Mungu nimepiga kura jumapili iliyopita. Samahani kuwasumbua katika hili lakini nadhani litawasaidia wengi katika kipindi hiki, je ule wino tuliowekewa kama alama ya kupiga kura tunaweza kuutoa kwa dawa/sabuni/ au kimiminika gani? Mpaka leo sijafanikiwa kusafisha kidole hicho.
Wino huu umenifanya niwafahamu wote waliokwepa kupiga kura
 
Fua majeans kama matatu ivi wino kushney

hahahaaaa mnatupoteza nyie, hii post haistahili hapa, si tunataka kujua namna ya kuishughulikia ccm, tumemchagua slaa toka jumapili lakini hadi leo hawajamtangaza rais
 
wengi hawakupiga kura waliuza shahada zao, ndio maana hawana wino. nasikia moto wa gesi unaondoa haraka huo wino:smile-big:
 
Asanteni kwa mchango wenu. Kimsingi bado natafuta jibu pamoja na kuwa bado mnafuatilia uchaguzi wakuu.
 
Halafu suala hili hata waandishi wa habari hawakukumbuka kulifuatilia. Ilitakiwa wote wanaoandamana, au kusherehekea ushindi wa mgombea yeyote wangekaguliwa kwanza vidole vyao kuona kama kweli walipiga kura. Wengine wanashiriki maandamano wakati hata kura zenyewe hawakupiga.
 
Simple!!!
Chovya kidole chako kwenye soda ya COCA COLA halafu wahi kupiga kura nyingine!!!!!!
 
wanajamvi,
namshukuru mungu nimepiga kura jumapili iliyopita. Samahani kuwasumbua katika hili lakini nadhani litawasaidia wengi katika kipindi hiki, je ule wino tuliowekewa kama alama ya kupiga kura tunaweza kuutoa kwa dawa/sabuni/ au kimiminika gani? Mpaka leo sijafanikiwa kusafisha kidole hicho.

kinyonye
 
Mimi kufikia leo ule wino umeanza kutoka wenyewe, lakini ajabu ni kwamba ngozi inabanduka , kama gamba la nyoka vile. Nami siilazimishi kutoka, nimeacha iwe hivyohivyo ili niendelee kukumbuka siku nilipomfuta mtu ajira, japo amechakachua na kurudi madarakani!
 
] Ivi sometime wachangiaji humu jf huwa akili mna weka pembeni alaf mnatoa maoniiii........ au ni nini kinakuwa kinawapata??
 
Kwa huyo anayetoka ngozi kuna mdudu anaitwa kaa (crab), anapatikana kwenye mito na baharini pia wapo. Mpasue huyo utumbo wake ni dawa ya kutoka ngozi mkuu!
 
Back
Top Bottom