Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,141
- 13,215
Mlezi wa Simba, Rahma Al Kharoosi, ametua jijini Dar es Salaam akiwa kwenye ndege kubwa yenye uwezo wa kubeba watu 150, lakini yeye akiwa ndiye abiria pekee ndani ya ndege hiyo.
Rahma, maarufu kama Malkia wa Nyuki, ametua na ndege hiyo aina ya Airbus 320 inayomilikiwa na Serikali ya Oman na anaitumia yeye kupitia cheo chake cha Balozi wa Heshima wa Oman nchini Comoro.