Kibosho1
JF-Expert Member
- Dec 12, 2017
- 2,491
- 3,998
Serikali kupitia TRA wao wamekaa maofisini tu wakisubiri kuwakamua wafanyabishara wanaokuja kulipa kodi. Sasa kumekuwa na wimbi la ufungaji biashara kwa kasi sana hasa baada ya janga la Corona kuikumba Tanzania.
Jambo la kushangaza huwezi kukuta Afisa wa TRA akijaribu kuchunguza changamoto alizopata mfanyabiashara mpaka akafunga biashara yake.
Leo hii ukiandika barua ya kufunga biashara yako TRA watapokea na kusitisha ulipaji kodi wako hawataki kujua kwanini unafunga.
Wafanyabishara wengine wameamua kufunga biashara na kuwa wamachinga ili kufanya biashara kwa uhuru zaidi. Kama serikali ingekuwa makini ingechukua kwa uzito sana hiyo changamoto na kuitatua mara moja iwe ni kupunguza kodi au la.
Sasa hapo hasara kwa serikali tu mana mapato yatapungua na huenda wakaelemewa na mzigo wa madeni.