Kufungwa jela kwa Sabaya kutarudisha tafsiri sahihi ya kuwa wapinzani siyo Maadui, bali ni wadau wa maendeleo

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,765
2,000
Wakati wa utawala wa awamu ya 5, chini ya utawala wa hayati John Magufuli, tafsiri ya kuwa mpinzani ilibadilishwa na kuwa ni adui wa maendeleo, badala ya tafsiri sahihi kuwa wapinzani ni wadau wa maendeleo.

Utendaji kazi wa watendaji wengi Katika awamu hiyo walijibadilisha, badala ya kufanya kazi kwa weledi na kufuata viapo vyao walivyoapa kwa kuitii Katiba, wao walifanya kazi zao kwa kuwachukulia wapinzani kama ni Maadui wa maendeleo, wakifuata nyayo za mtu aliyewateua.

Ni Katika kipindi hicho ndipo walipoibuka akina Sabaya na kujifanyia mambo wanavyotaka, kama tulivyomsikia wenyewe, wakati akijitetea Katika kesi ya ujambazi wa kutumia silaha, alijitetea kuwa aliyafanya yote hayo, yaliyokuwa yakionekana kama uhalifu, kwa maelekezo maalum, kutoka kwa ngazi ya uteuzi wake!

Ingawa hajamtaja jina, lakini tunavyojua ni kuwa ngazi ya uteuzi wake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo kwa wakati huo alikuwa ni Hayati John Magufuli.

Licha ya malalamiko mengi Sana, kutoka kwa wahanga, wa vitendo hivyo vya kuteswa na kuibiwa fedha zao chini ya mtutu wa bunduki, lakini kijana huyo Sabaya, alikuwa ni "untouchable" wakati huo wa utawala wa Hayati Magufuli na hukuna mtu aliyethubutu kumchukulia hatua kwa vitendo vyake vya uovu.

Lakini mara tu alipofariki Magufuli, na nchi kuanza kuongozwa na Rais Samia Suluhu, tukaanza kuona mambo yameanza kumgeukia huyo kijana Sabaya, ambapo alisimamishwa kazi na uchunguzi ukaanza mara moja kuhusu malalamiko mengi ya wahanga wengi kuhusu uovu wake aliowafanyia hao wananchi.

Hatimaye majuzi tumeshuhudia mhimili wa Mahakama ukimuhukumu kwenda jela kwa miaka 30 baada ya kuthibitisha pasipo shaka yoyote kuwa kijana huyo akishirikiana na wapambe wake, alikuwa ni jambazi, aliyetumia nafasi yake ya ukuu wa wilaya kufanya uhalifu huo wa kutisha, dhidi ya raia wasio na hatia!

Tunapata somo moja kubwa Katika tukio hilo la Sabaya, kuwa unapopewa nafasi ya uteuzi, tekeleza majukumu yako kwa weledi na kwa mujibu wa "job descriptions" ya nafasi uliyoteuliwa na usifanye kazi huku ukivunja sheria, hata kama utakuwa umepewa maelekezo maalum na mtu aliyekuteua, kwa kuwa mtu huyo hata kama ana nguvu kiasi gani za kisiasa, lakini hawezi kuishi milele,kwa kuwa hatimaye atakufa na atakuacha "solemba" wewe uliyetekeza uovu huo!

Fundisho lingine kubwa Sana tunalolipata ni kuwa kuna haja kubwa ya kuibadilisha Katiba ya nchi hivi sasa.

Kwani tumejionea kwa Katiba tuliyo nayo hivi sasa ambayo tumempa madaraka makubwa mno ya ki-mungu mtu Rais wa nchi na kumwekea kinga ya kushitakiwa na Mahakama yoyote nchini, akiwa Madarakani na hata anapotoka madarakani!

Kwa kuwa sisi binadamu wote tunaamini kuwa hakuna binadamu yoyote aliye mkamilifu na Katika misahafu yote ya dini ya Biblia na Quran, tunaelezwa kuwa mkamilifu ni mmoja pekee, ambaye ni Mungu wetu aliyeumba Dunia hii na viumbe vyote tunaoishi Katika Dunia hii.
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,765
2,000
Kuna msemo maarufu unaosema, mtegemee Mungu pekee, kwani ukimtegemea "sponsor" kuna siku atakufa!

Ndiyo hayo yaliyomkuta Sabaya😁
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,892
2,000
Hukumu ndogo ya jana bado inaonesha wapinzani ni maadui kwa CCM, ndio maana wako radhi kufanya lolote ili wafungwe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom