Kufunguliwa kwa shule nchini: Wanafunzi wasisitizwe kuwa waonapo dalili hizi toa taarifa kwa walimu au wazazi

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Dalili za ugonjwa wa COVID19 ni homa, kikohozi na mafua, kubanwa mbavu na kupumua kwa shida, kuumwa kichwa, vidonda kooni, koo kukauka, mwili kuchoka na kupoteza uwezo wa kuhisi ladha na harufu

Kwa wanafunzi wanaotarajiwa kurudi mashuleni, ni muhimu kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kila mara, kuepuka michezo inayohusisha kugusana na kukaribiana na kuvaa barakoa muda wote shuleni

Endapo mtu atakuwa na dalili zilizotajwa hapo juu, ni muhimu kuwajulisha walio karibu nawe ikiwemo walimu, wazazi au kupiga namba 199

#IshiNaCOVID19
 

Attachments

  • Poster_revised final Shule 2 ccc.pdf.pdf
    316 KB · Views: 14
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom