Kufungua redio au TV kwa sauti kubwa ni kuvunja haki ya utulivu ya jirani yako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufungua redio au TV kwa sauti kubwa ni kuvunja haki ya utulivu ya jirani yako

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by sulphadoxine, Sep 23, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  KATIKA nyumba tunazoishi kila mtu anahitaji kuwa huru akijisikia kufanya atakalo yeye binafsi au pamoja na familia au jamaa yake. Hii ni pamoja na nyumba zile zenye wakazi au wapangaji wengi wa rika na tabia tofauti tofauti wakimiliki pia vifaa vyenye kutoa sauti kama redio, TV au mitambo ya muziki.


  Ufunguaji wa sauti wa vifaa hivi vya burudani na mawasiliano ya habari yafaa uwe ule wa kistaarabu na wenye kujali haki ya utulivu ya watu wengine hata kama kuna kutofautiana katika kupata ladha ya muziki.

  Kwamba kuna wanaodhani, na hasa vijana, muziki ukiufunguliwa kwa sauti kubwa tena ukiwa unatoka katika vikuza sauti (“speaker”au “amplifier”) vikitoa midundo mizito huleta burudani zaidi. Huwa hawakumbuki kwamba kuna majirani zao wanaathirika kwa sauti hiyo kubwa.


  Athari kwa majirani zinaweza kuwa za kukosa umakini katika kusoma, kupata usingizi ikiwa ni usiku, wagonjwa wa presha au hali nyingine yoyote ya kiafya kupata mshtuko au kuumia zaidi, kutokuwa na masikilizano ya namna nyingine kama vile watu wakitaka kuwasiliana kwa simu.
   
 2. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Yawezekana pia katika maeneo hayo kukawa na watu wengine wenye kuhitaji utulivu ili kufanikisha shughuli zao, zikiwemo za kiuchumi, kama vile kirekodi sauti, kurekodi video za filamu na kadhalika ambao huathirika na mara nyingine kushindwa kuendelea na mazoezi hayo kutokana na makelele ya nje yanayowaingilia.

  Kinachopaswa kuangaliwa mara nyingi sio tu mapenzi yetu ya kitu fulani, ila ni kuwa na kiasi katika kitu chochote kizuri tunachotumia au tukijumuika katika burudani. Upendo kwa jirani zetu ndio uongoze maamuzi yetu. Hii ndio maana hata walioamua kuwa na sheria za madhara katika kulinda kero au bughudha kwa watu wengine wanasema kanuni inayofaa ni ile ya "Kumpenda Jirani Yako Kama Nafsi Yako". Kwa lugha nyingine katika muktadha huu ni kwamba ni muhimu kujuliza mara kwa mara kama jambo unalolifanya linaridhiwa pia na majirani zao ama la.
   
 3. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2011
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Je ipo sheria ya kuwazuia wasiokuwa na kiasi katika kufungua sauti za redio, tv nk zao?
   
 4. P

  PSYCHOLOGY Senior Member

  #4
  Sep 28, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaani kila mtu/watu ni wavunjaji wa sheria ya nchi.

  Hakuna wasimamiaji wa hizo sheria.
   
 5. Mlamoto

  Mlamoto JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Nimewahi kusikia nchi za wenzetu wakiwafungulia wenye hizo tabia mashtaka, kulipwa fidia. Sijui kama kuna sheria maalum hapa kwetu, japo kuna sheria ya uvunjifu wa amani.

  Hapa kwetu kesi yoyote ile ni kupoteza tu muda na 'resources' kibao na mwishowe kukatishwa tamaa! Inasikitisha.
   
Loading...