Kufungua biashara ya vifaa vya ujenzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufungua biashara ya vifaa vya ujenzi

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Parachichi, Mar 25, 2010.

 1. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2010
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wakuu poleni na shughuli!

  Ee bana kuna ndugu yangu ameniahidi kunitoa kwenye umasikini,kaniahidi kunikopesha USD 15,000 ili nifungue biashara ya kuuza vifaa vya majenzi.

  Sasa nauliza wakuu kwa kiasi hicho kinatosha kuanzia?au ntakua najitia pressure tuu manake hela ndogo?

  Maeneo ninayotarajia ni tegeta,Boko,Bunju.

  Naombeni ushauri tafadhali wenye ujuzi na hii kitu manake naamini JF ni zaidi ya mtandao.

  NAWASILISHA WAKUU
   
 2. Fighter

  Fighter JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Weza jalibu unune bidhaa kidogokidogo tatizo ya biashara hiyo ina vitu vingi sana.
   
 3. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  Acha uoga nenda kafanye kazi Baba, pesa huwa haitoshi
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  kama unaona unaweza kufanya biashara pls go 4 it bwana ..usiogope
   
 5. babalao

  babalao Forum Spammer

  #5
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ukitaka kufanya biashara ya vifaa vya ujenzi kwa ufanisi mtafute mtu ambaye amefanikiwa katika biashara hiyo. Mimi ninaye rafiki yangu ambaye amefanikiwa sana katika biashara hiyo anaweza kukupa basics. Kama uko serious nipigie simu 0755394701 nikuunganishe naye.
  CHARLES
   
 6. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi mwanzo ni mgumu sana na hukatisha tamaa pia. Na hasa hii mifumo yetu ambayo unatakiwa ulipe mapato kabla ya kuanza biashara. Lakini kwa maoni yangu mimi naona 15,000,000 to 18M ambayo ndio makadirio ya pesa unayotegemea kuwa kama initial capital sio mbaya kwa sababu ukishaanza biashara ndipo utajua wateja wako wanahitaji bidhaa gani kwa wingi kwa hiyo uwingi wa bidhaa katika fani ya ujenzi kama alivyochangia mdau mmoja hapo juu isikutishe.

  Pia ukishaanza biashara kuna kitu kinaitwa mali kauli (maana yake kwa kuaminiwa na mtu ambaye wewe hufanya whole buy kwake anaweza kuwa ana kukopesha mzigo kiasi fulani nje ya cash yako) hii husaidia sana watu wanaoanza shughuli kwani ghafla tu tutakuona una duka kuuubwa ajabu kumbe mali zingine ni ada ya uaminifu wako na sio lazima ziwe zako, ingawa faida ni yako na ndio itakayo kutoa mapema kwenye shughuli uliyo buni.

  Kaza buti anza shughuli hakuna kisichowezekana chini ya jua, naamini utapiga bao hasa kwa maeneo uliyo yalenga kwa sababu bado ni endelevu ki ujenzi.
   
 7. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  we jaribu tu bahati yako, biashara ni risk na ukitaka kufanikiwa lazima ukubali kurisk hiyo pesa kidogo utakayo azimwa anza na bidhaa ndogondogo then uongeze zile kubwa kadri mtaji unavyoongezeka!
  nakutakia mwanzo mzuri
   
 8. I

  Issangous Member

  #8
  Dec 28, 2014
  Joined: Apr 14, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Uzuri wa biashara ya vifaa vya ujenzi ni kwamba vinapanda thamani hata vikiwa dukani. Mwanzo ni mgumu, chamsingi zingatia uaminifu na uvumilivu, pia usisahau kumshirikisha Mungu wako kwa imani yako. Yote yanawezekana.
   
 9. Bill of Quantity

  Bill of Quantity JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2014
  Joined: Dec 2, 2014
  Messages: 1,250
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Jamani mi naulizia bei za bati hizi wanazosema zinatoka south africa, bei zake zikoje wadau??

  Je, nikichukua bati 20 naweza maliza nyumba ya vyumba vitatu na sebule yake??

  Naombeni pia ushauri katika comparison hasa bati hizi za kawaida na hizo wanazoita za S.A.

  Nina Tshs mil. 6 nataka nikajenge nyumbani kwetu kijijini kabisa ambako bei ya tofali ndogo ni tshs 100, hiyo ni ya kuchoma.

  Naombeni msaada wenu.

  cc Zanzibar Spices Issangous Mom, Jayfour_King, babalao , FirstLady1, Mokoyo, Fighter, na wengineo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2014
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,061
  Likes Received: 8,546
  Trophy Points: 280
  Anatakiwa alete kilishanyuma(feedback),leo mwaka wa nne huu.
   
 11. Zanzibar Spices

  Zanzibar Spices JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2014
  Joined: Jul 14, 2013
  Messages: 7,543
  Likes Received: 2,021
  Trophy Points: 280
  Shake Money hoja yako ni nzuri na umeipanga vizuri,lakini umepost kwenye uzi ambao kidogo hauendani na hoja zako za msingi.Nakushaur anzisha thread mpya ili iwe inajitegemea na hapoa utapata michango zaidi
   
Loading...