Kufungiwa MwanaHalisi Watanzania Tumewezwa

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
Ndugu wana JF Serikali kwa Kulifungia gazeti la MwanaHalisi naona imefanikiwa Lengo lake la kuzuia uvujaji wa Habari za ndani za Serikali, Nimejitahidi kufuatilia habari mbalimbali katika magazeti yaliyopo sasa hakuna habari za kusisimua na zenye kuonyesha mambo ambayo kwa ufahamu wa kawaida tusingeweza kuyasoma au kuyasikia.Mfano juu ya sakata la fedha za Uswiss Mwanahalisi lingekuwepo leo kila kitu kingekuwa hadharani.

My Take
- Haya magazeti yaliyopo sasa kama Tanzania Daima, Raia Mwema na mengine yenye muonekano unaoshabihiana kidogo na Mwanahalisi kwa nini yanashindwa kufuata nyayo za MwanaHalisi? je ni woga na yenyewe kufungiwa? au waandishi wake hawana uwezo wa kupata Taarifa muhimu ambazo watanzania tunahitajika tuzijue? au mianya ya uvujaji wa Taarifa serikali imezigundua na kuziziba?

- Ndugu yangu KUBENEA toka kivingine ili tuendelee kupata uhondo kama hawa wengine wameshindwa tuna imani na wewe na Mungu atakulinda.
 
hawajaamua kuweka kampeni kupiga kelele magamba walifungulie, sasa wanadhani nao watapona.SIku inakuja kwao mwanahalisi litakuwa ktk level yake.
 
Back
Top Bottom