Kufungiwa Mwanahalisi: Kwa msimamo huu hawa tuwaeleweje pamoja na kujifanya wasomi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufungiwa Mwanahalisi: Kwa msimamo huu hawa tuwaeleweje pamoja na kujifanya wasomi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Father of All, Aug 8, 2012.

 1. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  [h=3] Nimepokea ujumbe huo kwenye sanduku langu. Baada ya kuusoma nimestuka na kuona ni vizuri kushare na wenzangu hasa wana jamvi. TanzaniaJournalists’ Association[/h]
  (TAJA)
  [h=5] Malanga St. - Kinondoni, Duka la Habari House No. 102, Opposite OilCom Station[/h]


  THE PRESIDENT,
  P.O.BOX 7447,
  Dar es Salaam.
  Tel/Fax 255-222 760737
  [h=4] Mob:+255-764450000/719-222448[/h] +255-786450000.
  Email: tajahabari66@gmail.com
  KWA WAHARIRI

  WA
  2 Augosti 2012
  VYOMBO VYA HABARIMAKINI

  YAH: TAMKO LA KITAALUMA KWA UMMA KUHUSU SERIKALI KULIFUNGIA GAZETI LA MWANAHALISI KWA MUDAUSIOJULIKANA:

  NB: Kuandika habari bila ATTRIBUTION(kumtaja source WAKO) na kushindwa ku-BALANCE Habari yako kwa MTUHUMIWA katika HABARIunayoandika niukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya habari na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu –MCQUAIL (2005).  Kwa sababu hiyo yaMAADILI ya fani yetu,TAJA inalaani kwa nguvu zake zote gazeti laMWANAHALISI na SERIKALI kwa kuwa VIRANJAwa KUBINYA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI kwani hawa wawili ( MWANAHALISI NASERIKALI) ni MAADUI HATARI wa maendeleoya TASNIA YA HABARI na HADHI YAWaandishi wa Habari wasomi na makini hapaNchini.


  Aidha tunashangazwasana na wale wote wanaoilaumu serikali kwa madai ya kwamba inakandamiza uhuruwa habari na kutetea Gazeti la mwanahalisi eti wanadai linatumia uhuru wahabari kama unavyoelezwa katika katiba. TAJA tunaelewa watu hao wote wakiwemowanaodaiwa kuwa NGULI wa tasnia ya habari ni watu ambao elimu yao ya TAALIMU YAHABARI INA MASHAKA au ni ndogo kiasi kwamba hawaelewi maana ya uhuru wa vyombovya habari kitaaluma duniani kote MAANA YAKE.


  Duniani kote wasomiwa tasnia ya habari wanajua vigezo vya kuwepo uhuru wa habari misingi yakemikuu (1) Uandishi wa habari kwa kuzingatia misingi ya fani ya uandishi wahabari (Journalistic genre ethics) ambapo habari yoyote ni lazima iwe naATTRIBUTION na pili BALANCE isipokuwa inaruhusiwa kuandika bila kutaja jinakama kwa kufanya hivyo utahatarisha usalama wa mtoa habari (source). MWANAHALISIni MAHIRI katika kuandika habari za upande mmoja (UNBALANCED STORIES) na zinazohusutukio moja tu. MWANAHALISI kwakutozingatia maadili ya uandishi wa habari ni mvunjifu mkubwa wa uhuru wahabari hapa nchini na anadhalilisha fani ya UANDISHI WA HABARI NA WANAHABARIWENGINE MAHIRI (WATCHDOGS). TAJA Tuna wasiwasi na wale wote wanaounga mkonouandishi wa habari za MWANAHALISI zisizoattribution NA Balance. MWANAHALISI ukiwapa ushauri wa kitaaluma wepesikuitikia lakini HAWATEKELEZI- Rais waTAJA amewahi kuzungumza na Mhariri, ameishia kuitikia kimaelewano lakini hakunahatua aliyoichukua “kitaaluma” katika ku-BALANCE habari za upande mmoja wanazolalamikiwa.,
  Hivyo TAJA hatutafunimaneno na wala hatuoni haya kwamba wao ni WADHALILISHAJI WAKUBWA wa waandishi wa habari makini hapa Nchini nani WAVUNJAJI WAKUBWA WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI HAPA TANZANIA.Wanaowateteayawezekana wana AGENDA zao nyingine sioukiukwaji wa uhuru wa vyombo vya habari.

  UHURU WA VYOMBO VYAHABARI si ufunguo wa kuandika habari zisizozingatia maadili na weledi wauandishi wa habari. TAJA inawaomba wale wote wanaotoa mchango kuhusu jambo hiliwajiridhishe kwanza na kuijua fani hii wasivyamie tu kama wanavyofanya nduguzetu wa fani ya sheria eti wapeleke kesimahakamani(mbona waao mawakili wakivunja maadili ya uwakili hawawapelekiMahakamani ila wanawafukuza?),sisi tunawauliza kesi gani wakati MWANAHALISI habarizake hazizingatii maadili GAZETI hili pia ni mkosaji kama serikali yenye sheriaKANDAMIZI. Hawa wawili hawana tofauti wanalaumiana kwa makosa ambayo wote wanayafanya-wakandamizaji wa uhuruwa habari Tanzania kila mmoja kwa aina yake-hakuna wa KUTETEWA katika MGOGOROHUU.

  SERIKALI nayoTUNAILAANI kwa nguvu zetu zote, kwaniyenyewe inaongoza kwa ubinyaji UHURU WA HABARI hapa Nchini, ingawa washabiki waMWANAHALISI wanalalamikia sheria moja tu ya MAGAZETI YA MWAKA 1976 NO 3. Ukwelini kwamba hiyo inaoonyesha ufinyu wao katika kuelewa ukandamizaji wa Serikalikwa Uhuru wa Habari. HAPA NCHINI.

  SERIKALI YA TANZANIAni kandamizi sana ina zaidi ya sheria 20 ZINAZOBINYA UHURU WA HABARI NCHIN I, aidha hata ukiifuta hiyo sheria yamwaka 1976 ukaacha mlolongo nilioutajabado hujatatua tatizo la ukosefu wa uhuru wa vyombo vya habari Nchini. UTATUZIni kuandikwa sheria mpya ya upatikanaji habari na kufuta zote kandamizi zilizopo,lakiniSIO KUTETEA UANDISHI HOLELA WA AINA YA MWANAHALISI USIOZINGATIA JOURNALISTICGENRE ETHICS.

  TAJA tunasemawasiokuwa wasomi katika fani hii wasidandie HOJA HII NYETI yahitaji wasomi wafani hii ambao kwa sasa tupo na tumemaliza Vyuo vikuu sio mazoea eti mtu akiwamwandishi wa miaka mingi NGULI –mawazo hayo yamepitwa na wakati-TUSOME TUELEWEVYEMA MAANA YA UHURU WA HABARI ILI TUELEWEKE DUNIANI SIO KUTETEA WAVUNJAMAADILI YA FANI YETU-“TUNAJIAIBISHA WENYEWE MBELE YA WENYE WELEDI KAMA VILEJIRANI ZETU KENYA”

  TAJA TUNAWAOMBASERIKALI AMBAO NI WAONGOZAJI KATIKAUBINYAJI WA UHURU WA HABARI WAFANYE HIMA KUPITISHA SHERIA YA UHURU WA HABARI NASHERIA HIYO LAZIMA IWE NA KIPENGELE CHA KUFUNGIA CHOMBO CHOCHOTE CHA HABARIKISICHOZINGATIA MAADILI YA UA NDISHI WA HABARI

  Tunazungumza kisomina tunaomba tueleweke,TAJA haiungi mkono sheria ya magazeti ya mwaka1976,lakini kitendo cha kufungia gazeti lolote lisilozingatia maadili yauandishi wa habari hata baada ya kupewaushauri TAJA TUNAKIUNGA MKONO ili kuwekaheshima ya fani yetu,isiendelee kuchezewa kama kichwa cha MWENDAWAZIMU.

  1). Tunaomba serikaliIUNDE jopo la wasomi wa fani ya habari kutoka CHUO Kikuu HURIA, UDSM, SAUT na TUMAINIIringa tukae na hao wanaotetea MWANAHALISI NA kulaumu SERIKALI peke yake iliUMMA ueleweshwe jambo hili linavyopotoshwa na wanaojiita NGULI wa habari,matatizo ya tasnia ya Habari Nchini imevamiwa na watu wasio Wataalamu wa Fanihii na wengine hawana hata Diploma tu za fani ya Uandishi wa habari auMawasiliano ya UMMA lakini wamejipa majina ya NGULI (expert- kawaida mtu expertanategemewa kuwa angalau na M.A kama si PhD na kadhalika kwani tulio nao hawanahata Diploma zinazotambulika katika fani),ndio wanatupa taabu katikakuharibuTasnia hii Nchini kwa kujifanya kwamba wanafahamu sana UHURU WA VYOMBOVYA HABARI,KUMBE WANACHOFAHAMU NI KINYUME.

  2) Tunaomba wale wotewanaojitokeza na kujitambulisha kuifahamu fani ya habari na dhana ya uhuru wahabari wasiwe wanazungumza kiholela hii ni fani yenye wasomi, hivyo piawatutajie C.V zao ili tujiridhishe na maoni yao tujue ya kitaalamu au ya ainaya kijiweni?

  “MWANAHABARI MSOMIHAWEZI HATA KIDOGO KUTETEA “UNETHICAL WRITTEN NEWS PAPER”


  TAJA TUNARUDIA KULAANI WOTE, MWANAHALISI NA SERIKALI KWA MATENDO YAO YA UKANDAMIZAJI MKUBWA WAUHURU WA KUPATA HABARI NA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA.


  NI MATEGEMEO YA TAJA KWAMBA,MAADUI HAWAWAWILI WALIOJITAMB ULISHA WAZI WAZI WATAJIREKEBISHA KWA SERIKALI KUPELEKA SHERIAYA UHURU WA VYOMBO YA HABARI BUNGENI NA KUANCHANA NA AHADI ZISIZOTEKELEZEKA(HEWA)KILA MWAKA NA MWANAHALISI NAO WAJIENDELEZE KITAALUMA ILI WAJUE DUNIANI HAKUNAPOPOTE KWENYE UHURU WA HABARI USIO MIPAKA.
  MWISHO. TAJA tunampongeza Mhe. Saed Kubenea Mkurugenzi waMWANAHALISI, kwa kuongeza elimu yake Nje na kurudi nchini.Tunamshauri atumie elimu hiyoaliyoipata kuweka heshima ya TASNIA yetu badala ya kuidhalilisha kwa kuandikahabari zisizo, ATTRIBUTIO, BALANCE,TRUTH –Sisi tunadhani anaweza kulisaidia gazeti lake ambalo KITAALUMA kwa sasa linajitambilisha kwa pwaya halizingatiiMAADILI .
  (YEYOTE YULE MWENYEHOJA NASI TUNAYOSEMA AITE JOPO TUYACHAMBUE KISOMI KWA FAIDA YA WATANZANIA)


  HAMZA KONDO

  RAIS CHAMA CHAWAANDISHI WA HABARI TANZANIA (TAJA)

  MWANACHUO WA SHAHADAYA UZAMIVU MAWASILIANO YA UMMA(PhD inMass Communication) OUT.-mwaka wa tatu.
  Mob: 0786450000.

  CC-Mitandao ya Jamiina vyuo vikuu.
   
 2. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,491
  Trophy Points: 280
  .. Hivi kweli taarifa hii imeandikwa na mwanafunzi wa shahada ya Uzamivu? Sina tatizo na ujumbe, bali mpangilio wa hoja na matumizi ya lugha. Kweli shahada zimekuwa nyingi nchi hii! Kuna watakaoshangaa kwanini watu wanashahada lakini hawana kazi-jibu lipo kwenye makala hii!
   
 3. M

  MKALIMOTTO Senior Member

  #3
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiukweli tukiacha ushabiki wa kisiasa, Mwanahalisi ilishafika mahali ikawa kishabiki zaidi. Najua wengi mtakataa ukweli huu lakini Kubenea alilewa masifa ingawa ni kweli hata mimi naunga mkono kuwa uhuru wa habari hapa bongo bado sana. Kubenea anajisikia raha sana kwenye gazeti lake pakisomeka usalama wa taifa, kikwete, polisi, ccm, lowassa, rostam n.k hata kama hakuna haja ya kutaja watu hao.
   
 4. t

  thatha JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hoja mnazo tatizo ni uandishi tu.
   
 5. Bartazar

  Bartazar JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 805
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Well said mkuu, kama shahada zenyewe za uzamivu ndo hizi, nchi inakwenda arijojo!
   
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kwa wafuatiliaji wa mambo na watu makini hupati shida kujua lengo la sadist kubenea wafadhili wake.walichokipata ni haki yao ili wajifunze na kujirekebisha.asiefunzwa na mamae hufunzwa na dunia
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mimi ndio maana nishasema wazi. mwanafunzi anaemaliza OUT akija kwenye interviwe nampiga chini. haiwezekani elimu inagaiwa kama hivi. Kuna elimu gani inayosomwa kwa kubabaisha? Hichi chuo ni cha wanasiasa wanaohonga pesa na kupewa mitihani. HII NDIO OUT PUT YAO
   
 8. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Duh!Mimi sijaelewa kitu
   
 9. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,135
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  Kujua kwingi nako ni matatizo,ndicho kilichomtokea mtoa hoja apo juu,mpangilio mbovu sana wa mawazo,ila alichokizungumza kuhusu mwanahalisi kina ukweli fulani hivi.
   
 10. t

  thatha JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hoja za haja,inabidi zisambazwe kwenye mitandao mingine pamoja na magazeti.
   
 11. Prisoner 46664

  Prisoner 46664 JF-Expert Member

  #11
  Aug 8, 2012
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Nilidhani ninakuwa biased nilipoona hili mkuu,huyu jamaa yuko chini sana kwenye hili suala la uandishi..ninadhubutu kabisa kujilinganisha naye ingawa sijawahi kusomea habari maisha yangu yote.

  Idiocy!!
   
 12. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #12
  Aug 8, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Elimu ya bongo ya kumeza.
   
 13. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #13
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,151
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Hv uzamivu ni PHD? Na uzamili ni Masters?
   
 14. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hivi ni kweli mwandishi wa makala hiyo ni msomi wa PHD?
  Nacheka ninapoona anajisifia kama msomi tena mwandishi anayeandika sawa na mtoto wa darasa la tatu. Tofauti kaandikia computer tu!
  Nchi iko matatizoni
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Aug 8, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  KAma kweli wasomi wetu ndo hawa basi kazi bado tunayo hata baada ya miaka mia!
   
 16. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,730
  Trophy Points: 280
  Eti msomi!
   
 17. TETILE

  TETILE Member

  #17
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hana kozi ya communication skills anachanganya herufi kubwa na ndogo hata mwalimu wake wa darasa la pili (wa-mwandiko) hamkumbuki wasomi wa bongo ama kweli!!!!!!!!!!!!!
   
 18. Rapherl

  Rapherl JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 3,308
  Likes Received: 1,489
  Trophy Points: 280
  Hv huyu jamaa kasoma kweli mbona hawez kutenganisha maneno,alafu anaonekana ana CHUKI,smh
   
 19. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  lakini ujumbe umefika mkuuu
   
 20. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  umeeleweka,ila wewe ni mwandishi wa gazeti gani hapa nchini ?au makala zako ili niweze kukufatilia vizuri na shaada ya uzamivu wako na uandishi unaoufanya au utakao kuja kuufanya
   
Loading...