Kufungiwa kwa wimbo wa chura ni muendelezo na uthibitisho wa uzembe

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
11,495
24,212
Kitukio la kufungiwa kwa wimbo wa chura kumeendelea kuonyesha ni kwa kiasi gani hili taifa wenye mamlaka wamekosa umakini ( watu wasio na uwezo) kwenye taasisi muhimu na sehemu mbali mbali za kiutendaji.

Huu wimbo umepigwa marufuku ukiwa na zaidi au karibia ya mwezi kwenye media, watoto wameshauona na kuusikiliza vya kutosha kama maadili au saikolojia zimeshaharibika kwa kiasi gani? Hatujui.
Hivi hakuna chombo kinachotakiwa kuziona video au kusikiliza hizi nyimbo kabla hazijafika kwenye jamii na kuziizinisha au kumshauri msanii husika, nini cha kufanya? , kwa hili lililotokea maana yake hicho chombo hakipo na kama kipo hakiwajibiki. Ukilaza ni tatizo kubwa kwenye taifa
 
KTukio la kufungiwa kwa wimbo wa chura kumeendelea kuonyesha ni kwa kiasi gani hili taifa lilivyo na vilaza ( watu wasio na uwezo) kwenye taasisi muhimu na sehemu mbali mbali za kiutendaji.
Huu wimbo umepigwa marufuku ukiwa na zaidi au karibia ya mwezi kwenye media, watoto wameshauona na kuusikiliza vya kutosha kama maadili au saikolojia zimeshaharibika kwa kiasi gani? Hatujui.
HIVI HAKUNA CHOMBO KINACHOTAKIWA KUZIONA VIDEO AU KUSIKILIZA HIZI NYIMBO KABLA HAZIJAFIKA KWENYE JAMII NA KUZIIZINISHA AU KUMSHAURI MSANII HUSIKA, NINI CHA KUFANYA? , kwa hili lililotokea maana yake hicho chombo hakipo na kama kipo hakiwajibiki. UKILAZA NI TATIZO KUBWA KWENYE TAIFA HILI.
Hicho chombo kinachohusika nacho ni jipu, mbona ile video ya yule mbongomuvi iliyotarajiwa kulikashfu kanisa fulani ilizuiwa hata kabla haijaingia sokoni?
 
Cha ajabu ngoma ya high school ya Minaj inapigwa mpaka kesho!Ile ngoma ina maneno mazito sana,nyeti za mwanamke zimetajwa zaidi ya mara 5.
 
zinatajwa kwa lugha gani? ndo maana haina shida. je kuna video yake? ikoje? hapo ndo pa kufikiria.

Hadi kwenye sherehe kama Harusi inapigwa tatizo ni lugha, ule wimbo pamoja na Anaconda kwa kiswahili ni matusi kwa kwenda mbele.
 
Cha ajabu ngoma ya high school ya Minaj inapigwa mpaka kesho!Ile ngoma ina maneno mazito sana,nyeti za mwanamke zimetajwa zaidi ya mara 5.
Wanasema labda kwa sababu wameongea In English tena ile slang....
Hapa nyumbani kuna dogo ana miaka 7 ana upenda sanaa wimbo wa Nick Minaj ile anaconda... Sasa tukijiuliza ameangalia saa ngapi hatuna majibu...
Na anasema kabisa MY Anaconda Don't..
Je akijua hizo matusi alizo imba nick kwenye High School si ndo balaa tupu.. Leo wanamfungia chura,, je matusi gani ametukana kwenye chura..
Video ya chura vs Anaconda..
Leo Anaconda anashika chati kwenye television za Bongo.. Haha
 
Back
Top Bottom