Kufungiwa kwa wabunge: Katiba ya Tanzania inazuia haki za wabunge?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Kadhia ya wabunge kupewa adhabu ya kufungiwa kuingia kwenye vikao vya bunge kwa sababu wamevunja masharti ya kifungu cha 24 (c), (d) na (e) cha Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge imenifanya kuanza kuiangalia kwa umakini Katiba ya Tanzania na Kanuni za Bunge kwa upana zaidi. Inavyoonekana Katiba ya Tanzania inazuia au kuvunja haki za wabunge wa bunge la Tanzania kwenda kutafuta haki zao kama zilivyoainishwa kwenye ibara ya 107A(1) ndani ya Katiba yetu ya mwaka 1977.

Msingi wa mada yangu siyo kuchambua makosa yaliyotendwa au kama hukumu iliyotolewa ni halali au inaendana na kosa. Msingi wa mada yangu ni haki ya kikatiba katika kupata haki kwa wafanyakazi nchini kama ilivyoaninishwa na Katiba ya Tanzania.

Tunafahamu kuwa wabunge wamehukumiwa kwa kutumia Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge katika kifungu cha 24(c), (d) na (e) ambayo inasema;

24. Any person shall be guilty of an offence who-
(a) having been called upon to given evidence before the assembly or an authorised committee thereof refuses to be sworn or make an affirmation; or
(d) shows disrespect in speech or manner towards the Speaker, or
(e) commits any other act of intentional disrespect to or with reference to the proceedings of the Assembly or of a committee of the Assembly or to any person presiding at such proceedings.

Katiba ya Tanzania 1977 katika Ibara ya 107A(1) inasema;
‘’Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya Mahakama ya Zanzibar, na kwa hiyo hakuna chombo cha Serikali wala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki’’.

Katiba ya Tanzania 1977 katika Ibara ya 100(1) inasema;
‘’Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge’’.

Hii inatuambia kuwa, kwa upande mmoja Katiba inatuambia chombo cha mwisho katika kudai haki ni idara ya mahakama lakini pia kwa upande mwingine Katiba hiyo hiyo inawaambia wabunge hawana haki ya kwenda kudai haki yao kwenye chombo cha mwisho cha utoaji wa haki ambacho ni idara ya mahakama.

Ni haki yao Wabunge kuhukumiwa na chombo chochote lakini pia kwa mujibu wa Katiba yetu ni haki yao kupinga hukumu kwenye chombo kinachotambulika Kikatiba ambacho kimepewa jukumu la mwisho katika kuipata haki ya kupinga hukumu. Katiba inatuambia chombo cha mwisho cha kudai haki ni idara ya Mahakama.

Kama msingi wa Katiba katika Ibara ya 100(1) ni kutenganishwa kwa madaraka (The doctrine of the separation of powers) basi kwa nini wafanyakazi wa serikali na mahakama ambao wanatoka katika mihimili miwili tofauti wapewe fursa ya kuitafuta haki yao kwenye idara ya makahama lakini wabunge ambao wanahitimisha muhimili wa tatu wasipewe haki hiyo kwenye idara ya mahakama hasa kama ikichukuliwa ubunge pia ni kazi kama zilivyo kazi ndani ya serikali na mahakama.

Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 75 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2016, wabunge waliohukumiwa na bunge kwa sasa watakuwa wanatalipwa nusu mshahara na nusu posho zinazoambatana na mshahara huo katika kipindi chote wakitumikia hukumu zao na kwa maana hii, kwa nini wabunge hawapewi haki ya kwenda kudai haki zao katika mahakama ya Kazi kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine.

Mshahara ni haki ya mfanyakazi yoyote kama ilivyoainishwa katika Katiba kwenye Ibara ya 23(1-2) inayosema;
''23(1) Kila mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa aina yoyote, anayo haki ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watu wote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipo kulingana na kiasi na sifa za kazi wanayoifanya.
(2) Kila mtu anayefanya kazi anastahili kupata malipo ya haki''.


Ninachokiona ni Katiba kumpa haki mbunge kwa upande mmoja halafu hapo hapo inakataa kumruhusu kuitafuta haki yake.

Naomba tujadiliane
 
Msemakweli naona akili zimerudi na umetambua hatari iliyopo kutokana na kugukuzwa kwa wale wsbunge. In brief kufukuzwa kwao ni kmbkuwapa kick! Na jinsi Magufuli anavyofanya makosa kila siku basi anawapa ipinzani nguvu kubwa ya kipiga kelele!
 
Wafungiwe tu maana hamna namna sasa.

Hatuwezi kuwa na wabunge wazima kazi yao kulialia na kuzomea.
Mimi sina tatizo kuhusu wabunge kufungiwa lakini tatizo langu ni haki za wabunge katika kuitafuta haki yao kwa mujibu wa Katiba yetu.

Kwa nini katiba inajipinga yenyewe kuhusu haki za wabunge kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine wa serikali na mahakama.

Huoni kama kuna tatizo kwenye Katiba yetu?

Huoni kama kunahitajika marekebisho kwenye ibara zinazokinzana?
 
Msemakweli naona akili zimerudi na umetambua hatari iliyopo kutokana na kugukuzwa kwa wale wsbunge. In brief kufukuzwa kwao ni kmbkuwapa kick! Na jinsi Magufuli anavyofanya makosa kila siku basi anawapa ipinzani nguvu kubwa ya kipiga kelele!
Kurudi au kutorudi kwa akili zangu inategemea na mtazamo wako. Mimi ni yule yule uliyemfahamu toka siku ya kwanza.

Hatari ninayoiona ni Katiba kupingana yenyewe kuhusu haki za wabunge katika kuitafuta haki yao katika chombo cha mwisho katika kutoa haki.

Hakuna mtu mwenye akili timamu aliyechagua serikali ya Rais Magufuli akidhani anachagua maraika. Makosa yatatokea katika utendaji au kwa watendaji.

Kazi za wapinzani siyo kupiga kelele bali kujenga hoja mbadala itakayoisaidia serikali katika kazi zake au itakayowawezesha wapinzani kuaminika kwa wananchi ili wapewe nchi.
 
Back
Top Bottom